Kuna faida nyingi za kuwa na kampuni kama walivyogusia wengine...mimi niongezee hizi;
1. Limited Liability.
Kampuni ina ukomo wa kuwajibika kwa wanahisa wake...linamkinga member wa kampuni na mali zake binafsi zisitumike kufidia madeni ya kampuni isipokuwa ktk kiwango cha hisa ambazo nember wa kampuni hajazilipia.
Mfano kama member ana hisa 50 na alilipia hisa 30 tu, ikitokea kampuni inavunjwa na kuna madeni, huyu member atalipa thamani ya hisa 20 tu ambazo hajazilipia...wala mali zake hazitatumika kufidia madeni ya kampuni.
Kampuni inamiliki mali zake yenyewe, inashitakiwa au kushitaki yenyewe na si members. Kampuni ni mtu kisheria anayejitegemea. Kampuni na wanahisa/members si kitu kimoja.
2. Going concern.
Kampuni inaweza ku survive miaka mingi, ikarithishwa vizazi na vizazi...hata founders wa kampuni wakifa, bado kampuni itaendelea kuwepo....ila mifumo mingine ya ufanyaji kazi ina disadvantage fulani...mmiliki wa biashara binafsi akifa na biashara imekufa. Kwenye ubia, akifa mbia mmoja, basi partnership nayo imekufa. Cocacola na Pepsi, Ford, n.k ni kampuni zenye umri wa zaidi ya miaka 100.