Naomba nielezee
1. Masuala ya usajili, gharama na uendeshaji wake
2. Changamoto zake
3. Uzoefu wangu
1. Usajili, Gharama na Uendeshaji wake
A: Utangulizi
Biashara ya udalali ie Commission agent ni biashara kama biashara yoyote ile inayoingiza kipato halali na ni ya heshima tu. Dalali ananufauka na kiasi cha pesa au asilimia fulani sio lazima bhasi kila biashara inayopita mkononi mwako iwe ni lazima upate 10%. Kuna mambo mengi ya kibiashara ya kuangalia ili mteja umchaji kiasi fulaninikiwa pamoja na hali halisi ya kiuchumi. Changamoto kubwa imekuwa kwa wanaoifanya wengi kutokuwa waadilifu au kutaka hela kubwa sana kutokana na tamaa au kutokuwa na weledi nk. Hali hii imefanya biashara ya udalali kuwa ya kitapeli na watu wasioaminika katika jamii
A: Kusajili kampuni vs Jina la biashara
Unaweza kusajili kampuni au kusajili jina la biashara - BRELA. Faida za kusajili kampuni ya udalali ni kuwa inakuongezea thamani ktk kazi zako hasa unapoomba tenda katika makampuni mengine. Gharama za usajili kwa kampn inategemea na mtaji uliotaja ktk Memart
Ukishapata cheti cha usajili cha kampuni au vyeti vya jina la biashara utaenda TRA. Kama kampuni ina maana utapewa TIN ya kampuni baada ya kuwasilisha vielelezo vyote vinavyohitajika na kama jina la biashara TIN kama unayo tyr itaongezwa jina ulilosajili la biashara na kulipia kodi uliyojikadiria (kampuni) au kukadiriwa (binafsi). Utaomba Tax Clearance kwenda BRELA kwa ajili ya leseni ya udalali ie Commission Agent ambayo ni laki 3 na kuomba online ie TNBP
Then utaanza kuoperate biashara yako
Ili kufikia malengo yako vema na kujitofautisha na madalali wengine ni vema ukafanya haya:
1. Kuwa na ofisi nzuri inayoeleweka na kuwa siriasi kuepuka ofisi yako kuwa kijiwe cha madalali
2. Andika wasifu wa kampuni ie company profile
3. Andika barua za maombi ya kazi za udalali kutokana na unachofanya huku ukiambatanisha na wasifu wa kampuni
4. Acha mazoea ktk biashara hii
5. Kuwa na mashine ya EFD kwa ajili ya kutoa risito kwa malipo stahiki unayolipwa
2. Changamoto za biashara ya udalali
1. Utoaji wa risiti
Hili kuwa makini maana ukishaaminiwa na wateja malipo ya jumla yanakuwa yanapita kwako hvy hakikisha unatoa risiti ya kile kiasi tu unachonufaika nacho ww na mhusoka mkuu anatakiwa atoe kiasi chake husika. Mfano: kuna kazi ya mil 2 lkn hela yako ni laki 1 basi toa risiti ya laki 1. Kukosea kutoa hapo ina maana mauzo yk yatakuwa juu hivyo kupelekea kuja kulipa kodi ya mapato kubwa. Lkn pia kuna kodi ya huduma ya 5% usiisahau
2. Uaminifu
Madalali wengi ktk jamii wamekuwa na wanaonekana si waaminifu. Unatakiwa ujue kuwa ktk biashara hii jamii inakuangalia kwa sura ya kutokuwa mwaminifu. Basi jitahidi uweke mazingira ya uaminifu
3. Kuletewa wateja na madalali wenzako
Sio jambo baya ila hakilisha umejiridhisha na mteja hy na mqelezw kuwa hy aliemleta kwako hahusiki kwa lolote na kampuni yk kwn kutofanya hayo ipo siku atatapeliwa huko na msala kurudi kwako. Chukua tahadhali hii
Nk hizi ni za haraka haraka
3. Uzoefu ktk biashara ya udalali
Hii biashara nimeifanya sana hsa upande wa malori ya mizigo upande wa TRANSIT CARGO. Inalipa sana lkn lazima uwekeze sana hasa technolojia ndiyo utaweza kuimudu vema kuanzia
1. Kupata mikataba ya malori ambayo wao wanakuwa wanaleta docs ofisini kwako masua yote ya kutafuta mizigo i abaki kwako
2. Kuwa na mikataba na makampn ya clearing and forwading kukupa mikataa ya uhakika ya mizigo
3. Ulipaji usio wa kusumbua japo hali si hali
4. Kwa na connections za mizigo ya kurudi toka nje ya Tz
5. Kuhakikisha unafanya daily tracking ya malori yote uliyopakia mizigo na kuwasilisha ripot asbuhi na jioni kwa walengwa nk
6. Kuwa na mtaji wako ambapo iwapo kuna chnagamoto imetomea bhasi unaimaliza then unakuja kudai ktk utaratibu stahiki wa kihasibu nk nk
Kwa kuyafanya haya nilijitofautisha kabisa na madalali wa mizigo woote na kufanya biashara vema kabisa
Kwa haya machache kuna yenye manufaa kwako yafanyie kazi
Sent using
Jamii Forums mobile app