Kufunguliwa na kuangaziwa nuru ya kweli (Spirit Science)

Kufunguliwa na kuangaziwa nuru ya kweli (Spirit Science)

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,887
Nawasaliamia wana JF wote kwa pamoja,

Sayari yetu imeishi sasa mda mrefu. Kuna viumbe vingi sana vilivyo kwenye hii dunia. Kuna theory mbali mbali za uwepo wa hii dunia. Kuna moja inahusika na kuwa dunia iliumbwa na mungu.

Na kunanyingine inaongelea kuwa dunia imetokana na big bang. Ilikuweza kusonga mbele na kujua ukweli ni hakika lazima kuwepo na theory mbali mbali halafu wanasayansi wanazitumia hizo theories kufanya researches na experiments.

Sitaki nichukue mda mrefu sana kuelezea hizi theory. Nitajikita katika kuongelea hiki kitu cha Kuangaziwa nuru na kufunguliwa. Wanadamu asilimia kubwa sana duniani wamefungwa na kongwa la kidini na kisiasa.

Na wamekuwa hawajui nini cha kufanya. Wanadamu wamekuwa hawapo tayari kujifunza na kujua kwanini wapo hivyo na kwanini wapo duniani. Wamefungwa na kifungo kikubwa sana na kuwafanya wawe vipofu wanaopapasa papasa.

Dini imekuwa ndio kifungo kikubwa sana. Na wanasiasa wamekuwa wakikitumia kifungo hicho kuwateka na kuwafanya mateka. Lakini kwa pamoja tukijua kweli na kusimama kwa pamoja. Dunia itakuwa sehemu salama ya kuishi binadamu wote.

Mashindano, tamaa, woga wa kesho umewafanya watu kuwa na roho mbaya sana. Wapo tayari kufanya machafuko kwa manufaa yao, wapo tayari kuua kwa manufaa yao. Hawa sikilizi mtu na wala hawana mda wa kujari.

Ni wakati sasa wa kusimama pamoja na kujua sisi ni nani. Wanadamu sio watumwa, wanadamu sio wajinga, wanadamu sio dhaifu. Sisi ni roho inayoishi milele. Sisi ni waumbaji, Si tuna nguvu kubwa.

Wanajua kuwa Binadamu tunanguvu kubwa sana, na hawataki tujue hivyo. Wanataka tuwe mateka miaka yote. Wameifungia dunia ili pasiwepo na anayeweza kujua kuwa yeye anauwezo.

Lengo lao ni kuangamiza watu wote kwa manufaa yao.Tunauwezo wa kubadili, na tunauwezo wa kusimama na kuipigania sayari yetu. Ndugu usidhani katika ulimwengu huu upo pekee yako.

Kuna viumbe wengi tu kutoka kwenye Sayari zingine. Wapo na wanauwezo mkumbwa sana. Technolojia yao ipo juu sana. Sisi Human Kind tuna uwezo wa kuilinda sayari yetu.

Wamepandikiza DNA zao kwa watu. Watu wawe na roho mbaya. Human kind asili ya ni Upendo na furaha. Tunatakiwa kurejesha upendo. GOD IS LOVE. Tukipendana wote bila kujali siasa, dini, rangi nk. Tutakuwa na uungu.

Sisi ni MUNGU. Lazima tukumbuke wapi tumejikwaa, na tusimame kwa pamoja. Sisi ni kitu kimoja hakuna wa aliyetofauti na mwingine. Tunafanya kazi moja ya kujenga sayari.

Tuanze kubadilisha mitazamo yetu, tusimame kwa miguu yetu, tuungane, upendo ndio kila kitu.
 
Ashee!
Umenena mkuu, sababu watu wajifanya wakristo ukiamini Yesu umeokoka moto wengine wakiamini Allah wataepuka jehanam na kujipakulia bikira saba, na fix zinginezo.
Huo ni uongo mazee me nilikuwa naamini hivo ila nimejifunza and i'm 101% sure hayo ni mafix matupu na yanasaidia kutufanya wapumbavu haswaa na inawasaidia kutuexploit bila ya kutumia nguvu. Hiyo conspirancy inaitwa willie lynch, go google dat shit and many many more and know thy self.
 
Mhhhh mkuu sisi ni MUNGU
Duuuuuu aseeeee wapi pameandikwa hivyooo
Jamanii!!
Ni swali zuri sana. Kwa sababu watu wamekuwa vipofu na hawajui wao ni akina nani hata maandiko yao wanayoyasoma yaliyoandikwa hapo zamani hawawezi kuyaelewa.

Swali lako hilo inaelekea wewe ni mkristo. Imeandikwa Ninyi dio Miungu(Ninyi ni wingi). Imeandikwa hakuna amri iliyo kubwa kupita hii (UPENDO)

Yesu akesma Ufalme wa Mungu hauji kwa kutazama upo kule upo hapa. Ufalme wa mungu upo ndani yenu.

Yesu walimuua kwa sababu alisema yeye ni mungu.
Tena Yesu akasema: Kaeni dani yangu nami dani yenu kama mimi na baba yeye ndani yangu nami ndani yake.

Hapa haujui nini kimeandikwa kwenye maandiko yenu?
 
uko sahihi japo kuna sehemu zingne umechanganya changanya
 
Hii thread nayo haina tofauti na hiyo theory ya utumwa wa kifikra. Umeongelea utumwa wa kidini lakini mwisho wa mada umerudia kuikumbatia dini. Tukueleweje? Huo udanganyifu ulioutaja kule juu kuhusu dini kwa nini umetumia dini hiyohiyo kuhitimisha mada yako? Tumekushtukia........huna lolote zaidi ya kuutangaza ukristo hapa!!! Umejifanya kutumia akili sana ili watu wasigundue kuwa unatangaza ukristo. Pole sana....hapa ndio umefika mkuu watu tumesoma kuliko unavyoweza kufikiri.....
 
Mkuu umeongea vema lakini hapo kuhusu uungu wa Yesu ndio umeharibu! Ni kwamba hakuna andiko hata moja katika biblia Yesu anasema yeye ni Mungu. Bali ni watu ndio wanaompandikizia maneno mdomoni. Umeharibu sana mkuu. Soma vizuri biblia tena kwa makini.....
 
Ni vyema ukawa mwepesi wa kusikiliza na unajibu baada ya kuelewa. Ukijibu kabla hujaelewa ndio matokeo ya hapa ulipo comment. Hebu nakuomba soma kwa umakini kidogo thread hii.
 
Ndugu yangu ni vyema ukasoma kwa umakini na kuelewa ni nini kinazungumiziwa hapa. La sivyo utajikuta unajibu kitu ambacho sijakiongea. Mimi nimesema Human Kind is GOD.
 
Annael

Tuanzie kwako kwa kuondoa hiyo nembo yako ambayo inatia kichechefu kama vile kwa lugha ya kiingereza wanasema "to preach water and drink wine" maanake hiyo nembo ilitafsiri kuwa chama kilikuwa cha wakulima na wafanyakazi sasa hivi ni kinyume na zaidi!
 
Last edited by a moderator:

Hilo ndilo tattizo lako. Kunajambo ambalo nadhani huelewi. "Je tukubali kutofautiana au tukatae kutofautiana". Ukipata jibu sasa katika swali hili hakika utakuwa na furaha na upendo wa kweli.
 
Hilo ndilo tattizo lako. Kunajambo ambalo nadhani huelewi. "Je tukubali kutofautiana au tukatae kutofautiana". Ukipata jibu sasa katika swali hili hakika utakuwa na furaha na upendo wa kweli.

Tatizo hautaki kuwa objective! Nimekuambia kwa kukupa mfano ya kuwa hiyo nembo uliyoiweka inakwenda kinyume na upendo unaousema ndo nikakushauri anza kwako kujisafisha kwa kuwa na furaha ya kweli ndani chupa mpya( simaanishi alama ya chama chochote) kama ni furaha unaipata huko hauwezi kumuambia asiyeamini huko ulipo afuate unachokiona huko. Nikupe mfano; kuna wanaoamini kwa reincarnation na kuna wasioamini kwenye ilo jambo je utawafanya wote wakubaliane na wewe unachokiamini?
 
Annael

Inaonekana zamani ulikua mtu mcha Mungu lakini sasa umekua mtu wa Shetani.
 
Last edited by a moderator:
Tatizo hautaki kuwa objective! Nimekuambia kwa kukupa mfano ya kuwa hiyo nembo uliyoiweka inakwenda kinyume na upendo unaousema ndo nikakushauri anza kwako kujisafisha kwa kuwa na furaha ya kweli ndani chupa mpya( simaanishi alama ya chama chochote) kama ni furaha unaipata huko hauwezi kumuambia asiyeamini huko ulipo afuate unachokiona huko. Nikupe mfano; kuna wanaoamini kwa reincarnation na kuna wasioamini kwenye ilo jambo je utawafanya wote wakubaliane na wewe unachokiamini?
Hapa kwa kweli sijakuelewa unaongelea nini. Na inaonesha unasupport nilicho quote kwenye comment yako.
Nimesema ni bora Kukubali kutofautina ili kuwe na amani kuliko kukataa kutofautina.
 
Ni vyema ukawa mwepesi wa kusikiliza na unajibu baada ya kuelewa. Ukijibu kabla hujaelewa ndio matokeo ya hapa ulipo comment. Hebu nakuomba soma kwa umakini kidogo thread hii.

Thread nineshaisoma. Ujumbe anaotaka tuujue ni kwamba tuepuke minyororo ya kifikra za kidini. Lakini wakati huohuo anataka tumwamini Mungu. Sasa kipi sijamwelewa hapo?
 
Ndugu yangu ni vyema ukasoma kwa umakini na kuelewa ni nini kinazungumiziwa hapa. La sivyo utajikuta unajibu kitu ambacho sijakiongea. Mimi nimesema Human Kind is GOD.

Human kind is God....Yes it is! Can somebody have God without belief? And can somebody have belief without religion?
 
Mkuu Annael hii mada ni ngumu sana, hasa kwa watu ambao wanasoma wakiwa bado kwenye miamvuli ya dini. lakini ukweli mkubwa ni kwamba Mungu yu ndani yetu na si vinginevyo, kama uluvyosema sisi ni Mungu. huko kwenye dini tunashikiliwa tu kama misukule.
 
Thread nineshaisoma. Ujumbe anaotaka tuujue ni kwamba tuepuke minyororo ya kifikra za kidini. Lakini wakati huohuo anataka tumwamini Mungu. Sasa kipi sijamwelewa hapo?
Mimi kwenye thread yangu sijaelezea hata sehemu moja kuhusu kumwamini mungu. ndio maana nina sema hujasoma vizuri.
 
God is Good all the Time.
Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo ndiye nimtumikiaye.
Yeye yu Ndani yangu,Yeye huongea nami wakati wote.
Ukiitafuta kweli hakika utaipata na ukiipotosha kweli Hakika Laana i juu yako.
Jesus is the right path!
 
Back
Top Bottom