GE2025 Kufungwa kwa mitandao kuelekea uchaguzi mkuu je hii ndio demokrasia tunayoipigania kama nchi?

GE2025 Kufungwa kwa mitandao kuelekea uchaguzi mkuu je hii ndio demokrasia tunayoipigania kama nchi?

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

iZulu

Senior Member
Joined
Feb 2, 2013
Posts
135
Reaction score
166
Kwa muda mrefu tumeshuhudia kuzorota kwa ufanisi wa network katiak social media ikiwa lengo la kudhibiti utoaji wa uhuru wa maoni katika majukwaa mbalimbali kama Twitter, ClubHouse, na sasa kwenye YouTube hasa pale watu wanapotaka kujadili hali ya siasa nchini

Hali hii sio tu inakiuka katiba ya JMT na misingi ya demokrasia kama ilivyoshajiishwa katika dira ya maendeleo ya 2050 iliyozinduliwa hivi karibuni lakin pia inadhorotesha biashara za watu ambao wamesajiliwa na mamlaka kuendesha online media; biashara za mitandao...!

Kwasasa imekua desturi wengi wanapotaka kuingia kwenye mitandao ya kijamii kutumia VPN; ajabu ni kwamba hata hao waliofungia wanatoa matangazo yao kupitia mitandao waliyoifungia...sasa unajiuliza wanawahabarisha akina nani wakati wameifungia? Je na wao wanatumia VPN?

Tatizo la kufungia media tajwa hapo juu limekua kubwa nchini na limeanza kuvuka mipaka katika nchi nyingine ambazo zinaonekana kutumia mbinu hii kudhibiti uhuru wa maoni...je, kwa hili bado tunajisifia ni taifa la demokrasia?
Nawasilisha hoja.
 
Polepole mwenyewe ameshasema CCM ni Chama kilichoundwa kwa misingi ya kisocialist, vyama vya kijamaa kama CCM na kile Cha kicommunist Cha China (CCP) huwa vinaendeshwa kidikteta kwa hiyo swala la demokrasia huwa halipogo kwenye DNA yao
 
Shida Iko ,mbona watashinda tu...
Watuache mitandao yetu ....hii ndio kila yetu na furaha yetu!
 
Kila kitu limeshikiliwa na CCM, ila sijui wanachoogopa ni Nini?
 
CCM hawakubaliki na wanalijua hilo ndio maana hawajiamini
Chadema hawagombei lakini bado wako roho juu.
Lissu yuko Ukonga, chadema hawafanyi siasa, mahakama na polisi ni zao lakini bado tu hawana usingizi
 
Back
Top Bottom