Kufungwa na Simba mechi iliyopita ilikuwa ni blessing in diguise kwa Yanga

Tango73

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2008
Posts
2,180
Reaction score
1,291
Kufungwa na simba mechi ilopita ilikuwa ni blessing in diguise. Yanga baada ya kufungwa mechi hiyo na watani wake wa jadi kocha alichambua udhaifu wa timu kiufundi kuanzia idara ya ulinzi, midifida mpaka washambuliaji.

Kwa Utaalamu huo wa kusoma ufundi wa timu, kocha kainoa timu kimbinu bora sana za kujilinda na kushambulia mpaka kuwezesha kuifunga timu ya river united uganini.

Hivyo kufungwa na simba kulikuwa ni kupewa kioo cha kujitazama makosa yetu kiufundi ili kocha ajue aboreshe idara zipi na jinsi ya kucheza kupata ushindi.

Hongera sana yanga kwa ushindi wa leo. Hongera sana benchi la ufundi.
 
Kazi ya Nabi hiyo Simba anahusikaje hapa, huko kote alikotoka alikuwa akifungwa na Simba? Kila siku?
 
Mnajidanganya. Wale jamaa walikosa umakini tu pale mbele, wamewakosa goli nyingi sana na nyie hamkuwa tishio maana inaonyesha waliwasoma vizuri. Wakijirekebisha watakapokuja Dar hawawezi kosa goli mbili.

Na nimeshtushwa na kitendo chenu cha kupiga mpira nje ulipoanza tu.
 
Mkuu gori gani hizo walizotukosa nauku hawakupata hata shuti mojo lililolenga gori(on target) kwa dk zote 90 za mchezo? Au ndo ilimradi uchangie.
 
Ndo maana nimesema walikosa umakini. Sichangii mada kama sina cha kusema.
 
Mnajaribu kupuliziza kinyesi marashi,ila ukweli ni kwamba TULIWAKANDA SANA
 
Mnajidanganya. Wale jamaa walikosa umakini tu pale mbele, wamewakosa goli nyingi sana na nyie hamkuwa tishio maana inaonyesha waliwasoma vizuri. Wakijirekebisha watakapokuja Dar hawawezi kosa goli mbili.

Na nimeshtushwa na kitendo chenu cha kupiga mpira nje ulipoanza tu.
On target 0 alafu wewe unasema nini!?.
 
Mnajidanganya. Wale jamaa walikosa umakini tu pale mbele, wamewakosa goli nyingi sana na nyie hamkuwa tishio maana inaonyesha waliwasoma vizuri. Wakijirekebisha watakapokuja Dar hawawezi kosa goli mbili.

Na nimeshtushwa na kitendo chenu cha kupiga mpira nje ulipoanza tu.
Wewe nilishakuambiaga mpira unafosi tu kuushabikia ila umekukalia kushoto. Timu haina hata shots on target halafu unasema wamewakosa magoli mengi. Kitendo cha Yanga kuupiga mpira nje ni kitu cha kawaida sana kwenye mpira wa miguu hata ulaya timu zinafanya hivyo. Anza kufatilia mpira usiishie kuangalia mechi tu za Simba na Yanga. Angalia mechi pia za ulaya uongoze ufahamu wa mchezo wa mpira wa miguu.
 
Ninachosema Rivers walikuwa bora ila walikosa umakini eneo la mwisho, yaani hadi maneno hayo yanawakwaza? Mnataka niseme mliwashika kila idara na hawakufurukuta? Mashuti yao mengi yalikuwa yanawababua mabeki wa Simba na hiyo ndiyo kukosa umakini ninakosema.
 
Lete takwimu zao kuonesha walikuwa bora kuliko Yanga.
 
Ninachosema Rivers walikuwa bora ila walikosa umakini eneo la mwisho, yaani hadi maneno hayo yanawakwaza? Mnataka niseme mliwashika kila idara na hawakufurukuta? Mashuti yao mengi yalikuwa yanawababua mabeki wa Simba na hiyo ndiyo kukosa umakini ninakosema.
Kama unazungumzia rivers vs Simba, basi sawa hiyo ilikuwa ni mechi uliyoangalia peke yako na mashabiki wenzako wa Simba labda.
 
Kazi ya Nabi hiyo Simba anahusikaje hapa, huko kote alikotoka alikuwa akifungwa na Simba? Kila siku?
Wako obsessed na Simba.Ndio kipimo chao.Wakishiba mihogo, Simba wakicheua Simba basi tabu tu.
 
Back
Top Bottom