Kufuru ya Katiba ya Nchi kuitwa 'kijitabu' inayoitesa nchi

Kufuru ya Katiba ya Nchi kuitwa 'kijitabu' inayoitesa nchi

inchaji

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2019
Posts
2,671
Reaction score
5,476
Tatizo lilianza siku alipoidharau Katiba ya nchi kwa kuiita kwa maneno yake mwenyewe kuwa 'kijitabu'.

Na kuna siku atashitakiwa kwa kuikashifu Katiba ya nchi.

Namna pekee ya kupona ni kwa yeye kutoka hadharani na kuhutubia kama alivyofanya juzi lakini badala ya kuongea mipasho aombe radhi kwa kosa la kuikashifu Katiba ya nchi na pia aanzishe mchakato wa kupatikana kwa Katiba mpya.

Watu wanatekwa kwa sababu ya 'kijitabu'.

Watu wanauliwa kwa sababu ya 'kijitabu'.

Wapinzani wanateswa kwa sababu ya 'kijitabu'

Hakuna chaguzi huru na za haki kwa sababu ya 'kijitabu'

Haupo uhuru wa vyombo vya habari kwa sababu ya 'kijitabu'.

Tatizo si kina WHO ARE YOU. Tatizo ni Katiba ya Nchi kutwezwa na kudharauliwa kwa kuitwa 'kijitabu'
 
Back
Top Bottom