Kufuta sherehe za Uhuru wa Tanganyika huku sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar zikiachwa ni ishara ya kuiua kabisa Tanganyika. Hatutakubali kirahisi

Umeishia darasa la ngapi?! Lini Uhuru wa Tanganyika ulibadilishwa na kuitwa eti Uhuru wa Tanzania?! Na kama wamebadilisha kwanini Ikulu iliweka bandiko la HERI YA MIAKA 63 YA UHURU? Au 1964 hadi 2024 ni Miaka 63? Hivi unafahamu maana ya Muungano wa 1964 hata uhusishe na Uhuru wa Tanganyika?!
 
Umeishia darasa la ngapi?! Lini Uhuru wa Tanganyika ulibadilishwa na kuitwa eti Uhuru wa Tanzania?! Hivi unafahamu maana ya Muungano wa 1964 hata uhusishe na Uhuru wa Tanganyika?!
Uhuru ni wa Tanganyika kuanzia mwaka 1961-64, kuanzia 64 na mpaka sasa ni unaitwa uhuru wa Tanzania, darasa nililoishia halihusiani na hii mada.
 
Uhuru ni wa Tanganyika kuanzia mwaka 1961-64, kuanzia 64 na mpaka sasa ni unaitwa uhuru wa Tanzania, darasa nililoishia halihusiani na hii mada.
Darasa uliloishia linahusika sana kwa sababu hata aliyeishia Darasa la VII tayari alishafundishwa kuhusu Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya Zanzibar, na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar lakini unaonekana yote hayo unayachanganya!
 
Wewe umeishia la ngapi?. Akili zile zile nyepesi za kitanzania zenye kumpima mtu kwa uelewa wa darasani.

Nina shahada ya pili ya Public Administration ya chuo kikuu cha Kharkov ya mwaka 2001.

Mada ni Rais anayo haki ya kuifuta sherehe ya uhuru kwa mamlaka yake aliyonayo. Wapo wanaopoteza muda kumpinga na wapo wanaokubaliana nae.
 
Una shahada ya pili halafu bado unashindwa kutofautisha kati ya Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?! Hakika walimu wako walikuwa na kazi hasa!!
 
Mbona Mwenge bado unakimbizwa kila mwaka??
 
Una shahada ya pili halafu bado unashindwa kutofautisha kati ya Uhuru wa Tanganyika, Mapinduzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar?! Hakika walimu wako walikuwa na kazi hasa!!
Wewe una elimu gani mbona unatanguliza dharau bila ya kujitambulisha kwanza wewe mwenyewe?.

Uhuru wa Tanganyika, mapinduzi ya Zanzibar na Muungano ni mambo ninayoyafahamu kwa miaka zaidi ya 40 sasa. nashangaa watoto humu jukwaani kuhoji vitu vidogo sana kisa chuki waliyonayo kwa Rais Samia.
 
Unazungumzia suala la dharau wakati wewe ndo wa kwanza kuniambia nina mawazo ya kitoto sana?! Na kama ulikuwa unafahamu hayo kwanini ulikuwa unachanganya madesa, na mbaya zaidi kila unapojaribu kuambiwa ndo kwanza ukawa unajiona upo sahihi ila sie wengine tuna mawazo ya kitoto!!!
 
Ni mkakati mzito.
Unafuta za tanganyika za wazanzibari unauudhuria!
Back Tanganyika ya
 
Hiyo ndo hasara na hatari ya kutawaliwa na expert na gabacholi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…