Kufutwa kadi nyekundu ya Mkude tafsiri yake nini?

Kufutwa kadi nyekundu ya Mkude tafsiri yake nini?

mwembemdogo

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2016
Posts
2,282
Reaction score
1,252
Katika mechi ya Simba Na Yanga mchezaji Mkude wa Simba alionyeshwa Kadi nyekundu Na Refa Saanya.Kitendo hicho kiliifanya Timu ya Simba kucheza pungufu Na Yanga kufaidika Na upungufu huo.Ninacho jiuliza ni kwamba Kwa hiyo mchezaji Mkude hakutenda kosa Na hakustahiri kuonyeshwa hiyo kadi.Kwa matokeo hayo Bodi Ya Ligi inawambia nini Simba Kwa yaliyoyapata Kwa mchezaji wake kuonyeshwa kadi bila kosa?Kwanini Bodi ya Ligi ilimpanga Refa aliyetoka kifungoni hata haijapata uhakika kama amejirekebisha?
 
Hapa sijui nani anamhukum nani.
Ile kadi ni haki yake kwa kosa lile
Na TFF na bodi zao hizo ndio janga la soka nchini.Hii bodi yenyewe inabidi ifungiwe

Ushauri wangu kwa Simba:
Huu mchezo wa kufanya mechi hizi kuw akama Bonanza
Wawapeleke Mahakamani kwa kuwapa Hasara na ikiwezekana matokea yabadilishe wapewe ushindi Simba,maana Kadi ilitolewa mwanzo sana na uwezo wa Simba kushinda ungekuwepo.Bila watu kupigwa Faini kubwa hizi bodi zitazoea,maana kubadili ratiba kila siku,kuwa na maamuzi tata kila siku..mpira wenyewe wa kuunga unga

Huu ujanja ujanja ndio hata kwenye Mashindano ya Kimataifa kwa wenzetu waliojipanga bado wanatufunga kipumbavu kila siku huku tukijifanya Nchi ya Amani na Utulivu.Kuna Nchi hazina amani miaka teleee,na tukicheza nazo wanatufunga tena wao hukusanya tu wachezaji kama bonanza na kutuchapa.Aibu tupuuu
 
ingekuwa ni vizuri ile bodi ya 'wahuni' ikafuta matokeo ya sare na kuamuru mechi ile irudiwe ndani ya masaa 72 ili 'mshindi' wa halali apatikane........
 
ingekuwa ni vizuri ile bodi ya 'wahuni' ikafuta matokeo ya sare na kuamuru mechi ile irudiwe ndani ya masaa 72 ili 'mshindi' wa halali apatikane........
Manji hawezi kukubali, ujue ile timu ni yake rasmi anaweza kuamua chochote hata ikiwa uamuzi wake utapelekea timu kufungiwa
 
Kupunguza presha za wale mashabiki wang'oa viti
 
Simba na Yanga wakicheza refa atoke ulaya.. Wachezaji wa simba vilaza watashindwa kumzonga wataongea lugha gani
 
Katika mechi ya Simba Na Yanga mchezaji Mkude wa Simba alionyeshwa Kadi nyekundu Na Refa Saanya.Kitendo hicho kiliifanya Timu ya Simba kucheza pungufu Na Yanga kufaidika Na upungufu huo.Ninacho jiuliza ni kwamba Kwa hiyo mchezaji Mkude hakutenda kosa Na hakustahiri kuonyeshwa hiyo kadi.Kwa matokeo hayo Bodi Ya Ligi inawambia nini Simba Kwa yaliyoyapata Kwa mchezaji wake kuonyeshwa kadi bila kosa?Kwanini Bodi ya Ligi ilimpanga Refa aliyetoka kifungoni hata haijapata uhakika kama amejirekebisha?

Hizi bodi zinaua mpira wa Tanzania, maamuzi ya refa uwanjani yaheshimiwe
 
Zinafutwa kadi za Simba tu. Mara wanachagua mechi ya kutumikia adhabu baada ya kadi tatu za njano. Mara baada ya Simba kuitumia kanuni hiyo, ikaondolewa.
 
Back
Top Bottom