Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

mtzmweusi

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
8,658
Reaction score
8,994
Wakuu leo naona tunapigwa kabisa kwakweli tujipange kuvumilia maumivu
=====


UPDATES



Kikosi cha timu ya Taifa cha Tanzania 'Taifa Stars' leo kimeshindwa kuandika historia ya kukata tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika(Afcon) baada ya kupoteza pointi tatu mbele ya Lesotho kwa kufungwa bao 1-0.

Stars wapo kundi L lenye timu ya Uganda iliyofuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku timu ya Lesotho ikifikisha pointi 5 sawa na Stars, Cape Verde ina pointi 4



Kwa kupoteza mchezo wa leo matumaini ya ya timu itakayoungana na Uganda Afcon Cameroon mwakani kwa kundi L yamebaki kwenye mechi za mwisho zitakazofanyika mwakani

Stars watacheza na Uganda nyumbani mwezi Machi mchezo wa marudiano, huku Lesotho wakicheza na Cape Verde wenye pointi 4

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Stairs kufuzu kucheza michuan hiyo ni mwaka 1979

 
tutatupia viwili kipindi cha kwanza kuanzia dk 10 na 30... baada ya hapo ni kuziia mwanzo mwenga... kipindi cha pili tutamalizia goli letu la mwisho na kufunga idadi ya magoli matatu bila.... ili tukija tupokelewe ikulu
 
Hivi mtu unaamka tu na kuandika hatutashinda, hivi mbona kwa arsenal mlikua die hard fans mnashindwaje kwa timu yenu ya Taifa, hata kwa kuipa benefit of the doubt. Au ndio kujihami roho isiume, tukifungwa whether ulisema tutafungwa au la as long as ni shabiki wa mpira na ni mtanzania roho lazima ikuume. Tuache kutengeneza mazingira ya lawama kama ni kuandaa timu watanzania wote tuna nafasi na yako ikiwa ni kuwapa moyo sio kuwavunja moyo.
 
Wakuu,

Leo Tanzania inaweza kuingia kwenye historia muhimu sana kwenye ulimwengu wa michezo. Tunatakiwa kuishinda Lesotho kwa namna yeyote ili tuweze kushiriki michuano mikubwa kabisa barani Africa ambayo tulishiriki Zaidi ya miaka 38 iliyopita.

Watanzania wote tusimamishe kila kitu na kuonesha kila namna ya kuiunga mkono timu yetu ya Taifa. Masaa haya machache tuchafue mitandao ya kijamii na mitaani kuonesha mshikamano wetu nyakati muhimu kama hizi.

Hii mechi ya leo si ya kawaida bali ni vita ambayo tukishindwa ni taifa limeshindwa na tukishinda ni taifa limeshinda. Heshima ya ushindi wa leo itaiweka nchi kwenye ramani kubwa Zaidi kimichezo na Zaidi itabadili uelekeo wa michezo na hasa nafasi ya wachezaji wetu kupata fursa Zaidi kwenye Nyanja za kimataifa.

Kila lakheri timu ya taifa ya Tanzania, nendeni mkapiganie nchi kwa nguvu zenu zote. Wanajeshi wetu wengi wamemwaga damu zao kuipigania heshima ya taifa letu na nyie mtambue mnawajibu sawa na huo kwaajili ya Tanzania.

Taifa zima leo limeweka matumaini yote mikononi mwenu, kaipiganieni Tanzania na mlete heshima ambayo vizazi vyote vitawakumbuka kuwa nyie ndio mliorudisha heshima ya nchi baada ya miaka 38 kushindwa kushiriki michuano hii mikubwa.

"We will stand and fight here. If we can't stay here alive, then let us stay here dead." General Sir Bernard Montgomery

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Taifa Stars ….
 
Tena waangalie zile 50m zisiwatokee puani! Presidaa alisha waonya!

MUNGU IBARIKI TAIA STARS; MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Unawekeza kwa wazee waliobalehe unategemea ushindi

Tengenezeni Timu za watoto, mafanikio yatapatikana tu wewe ukiwa umezeeka

Tatizo mnataka mambo ya haraka muonekane mmefanikiwa kwenye kipindi cha uongozi wenu, Ulaya haipo hiyo

Wanajadili uchumi Wa miaka 100 ijayo hawaogopi atasifiwa nani

Bongo Kila Mtu ataka sifa haraka
 
Mkuu hayo leo hayasaidii. Tujifunze kujua tuseme nini wakati gani. Lolote litakalotokea leo huko nje itakuwa ni sura ya Tanzania wala si TFF wala nani. Pamoja na mapungufu yote lakini tukishinda ni ushindi wa Tanzania.
 
Ila hii post ingewekwa kwenye jukwaa husika la sports and entertainment ingependeza sana!
 
Lawama na maneno yote itakuwa vyema baada ya mechi. Nchi ikiwa vitani huwezi kuanza kubeza jeshi lako na hasa majenerali kuwa hawakujiandaa vizuri kwa vita.

Mkiwa vitani mtatoka na mlichonacho hata kijiko na mwiko lakini lengo kuu ni kushinda alafu mengine yatafata.

Leo tuwatakie kheri wenzetu tuliowapa jukumu zito kutuwakilisha.
 
Reactions: Tui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…