Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

Kufuzu AFCON-2019: Stars yashindwa kufunga mahesabu mapema! Yakubali kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Lesotho

walifanya makusudi, uwanja wa nyasi badia za kiwango cha chini kabisa, wamejaza yale ma rubber uwanjani na kufanya mpira unakosa uelekeo.
Kwani wao Lesotho walicheza uwanja tofauti na huo? tukishindwa tunatafuta vichaka vya kuficha udhaifu wetu.
 
Wanajamii ya michezo

Leo Tanzania imepoteza mchezo wake muhimu katika kuelekea kufuzu Afcon

Uwanja uliotumika katika mchezo huu ni tatizo na imechangia kwa kiasi kikubwa sie watanzania kupoteza mchezo huu

Hivi ni kweli lesotho haina kiwanja bora zaidi ya hiki kilichotumika leo au ni figisu tu zimetumika kuiangamiza stars?
Attitude ya 3000 metres, kwani kiwanja hatukujua
 
Hivi kocha mnaigeria nao wanaeenda Afcon mtegemee awapitishe! Nchi imeshindwa kumpata kocha mzalendo, au kumsomesha mzalendo,pia tff hawana mpango wa mda mrefu, mipango yao mingi ni ya zimamoto tu.
 
Nakumbuka Bwana Mkubwa alisema kucheza mpira ni rahisi sana sasa sijui wanafungwaje, na akasema sio lazima tuwategemee wale Wachezaji wanaotoka nje, ushauri mzuri sana ule.
 
Kwa kilichotokea Maseru, namuunga mkono Rais wetu kwa wazo lake la kuchagua vijana, wapelekwe jeshini, wafundishwe nidhamu, uzalendo, mpira na ukakamavu alaf wawakilishe Taifa katika mashindank mbalimbali. Kilichotokea Jana na aib na hasara kwa Taifa
 
BADO HATUJAJUA SOKA LETU LINAUMWA UGONJWA GANI

Tatizo la TWAFA STARS si kiwanja, si kocha. wala si hela. Mkapa alidhani ni kiwanja akawaleta wachina wakajenga kiwanja kizuriii, JK akadhani ni kocha akatuletea Maximo toka nchi ya football samba, sasa JPM amedhani ni pesa akawaita ikulu akawapa mabulungutu!!! Mawe! Lesotho kanchi ka wanywa pombe 24 hours kametubonda na mabulungutu yetu tena mbele ya waziri wetu!

Hakika raisi ambaye unaweza kudai alilijua tatizo la soka letu ni Mzee Mwinyi. Alitambua sie ni kichwa cha mwendawazimu akaamua kutopoteza muda wake. Akaacha tunyolewe na kila mlevi. Bora mara alfu!

Nimemsikiliza Waziri akihojiwa pale Lesotho anadai bado ana matumaini! Aisee! Tuna roho ya paka?

Ukweli ni huu: tumetoka!!!

Lakini kwa kuwa mpaka na raia au wapenzi hatujajua tatizo tumeanza zile hesabu zetu. Eti Cape Verde akimfunga Lesotho na sisi tukimfunga Uganda tunapitaaaa!!!! Abunuwasi mathematics!

Sasa watu weshaanza kudai ni makosa ya kocha! Eti hakumpanga fulani au kampanga fulani! Wangependa awapange wanaowataka wao. Moja ya tatizo letu ni kila mtu kujifanya kocha! Maximo yalimshinda!

Tunao wachambuzi kibao wa soka lakini nao ukiwasikiliza unapata kinyaa!!

Je soka letu linaugua ugonjwa gani? Tukaeni chini tumwangalie mgonjwa vizuri. Tusikimbilie kutoa dawa ilhali hatujaujua ugonjwa. Tutampa mgonjwa wa kipindupindu klorokwini!

Kama raia, mchezaji wa zamani na mpenzi Wa soka naomba nitoe mchango wangu wa mawazo kuhusu hili gonjwa sugu.

Kwanza nianze kwa kusema kuwa enzi za Mwalimu tuliwahi kuwa na timu ya taifa iliyokuwa ikitupa raha kwa kiasi Fulani. Kwa hiyo kama kweli tunamuenzi Mwalimu turudi kurizama alifanya mini kwenye michezo hadi tukawa tunaogopwa? Vijana wengi hawajui tuliwahi kuogopwa! Nichepuke kidogo kuelezea kosa! Niliwahi kuwepo Cairo kikazi mwaka 2002. Siku moja nikaenda mtaa wenye maduka karibu na msikiti maarufu wa Al Azhar. Pale kilipo chuo kikuu cha kiislamu. Nilikuwa nimevaa jezi ya yanga. Kuna vijana waliponiona tu wakaja wakishangilia! Yanga! Yanga! Yanga! Kumbe ni Wa klabu ya All Ahly! Ghafla wakatokea wengine wakishangilia Simba, Simba, Simba! Kumbe Wa Zamalek! Ndio nikajua kumbe Hawa ni wapinzani Wa jadi. Kumbe Yanga ikicheza misri inashangiliwa na All Ahly na Simba ikicheza inashangiliwa na Zamalek! Basis tukalonga sana kuhusu vilabu hivi. Ndipo nikajua historia zao. Zamalek ya watoto Wa mjini wezi wavuta bangi na wenzao watoto Wa matawi ya juu! Kwa hiyo kuna muda tuliwika Afrika!

Je siri ya enzi ya mwalimu ilikuwa mini?

Ilikuwa GOOD FOOTBALL ADMINISTRATION! Hakuna jingine! Ni enzi za kina Paul West Gwivaha, Said Ahmad All Maamry, Meja Mirisho Sarakikya na wenzao. Hakukuwa na kiwanja cha maana, makocha Wa taiga toka nje wala mabulungutu kwa wachezaji!

Ni vyema wizara husika na serikali ikajiuliza what is good football administration? Nyerere aliwezaje kuisimika? Ndipo huyu mwendawazimu atapata Tiba stahiki. Lakini tukiendelea kudhani tatizo ni kiwanja, kocha au mabulungutu basi tujiandae na ugonjwa wa moyo kitaifa maana TWAFA STARS hatapona!

Tuache ujinga wa kudai Amunike ndio kasababisha tufungwe! Tuache ujinga Wa kudhani tuba ni kurejesha mabulungutu au kuwapeleka wakabangue korosho! Kama sivyo TUTAPATA TABU SAAAANAA.

Binafsi naamini kwa dhati hatutacheza AFCON 2019 Cameroun.

TAARIFA: Jana hapa Lome Togo (Eperviers) wamebugizwa 4-1 na Algeria! Mchezaji Nyota Ema Adebayor Chei alicheza. Hii ni baada ya kugoma kuichezea Epirvier mechi zilizopita. Kwa mechi akatangaza lazima achezee kwa kuwa ni muhimu na akapangwa! Sasa kwa Mara ya kwanza Jana washabiki wamemimina mvua ya mawe baada ya 4-1!! Mvua hiyo ilimnyeesgea Adebayor kuliko wenzake! Washabiki wametangaza rasmi hawatahudhuria mechi ikiwa Adebayor atapangwa! Wendawazimu wenzetu! Ili ujue fedha sio tatizo wachezaji woote Wa Togo ni professionals! Hawana njaa!
.
 
Wakuu leo naona tunapigwa kabisa kwakweli tujipange kuvumilia maumivu
=====


UPDATES

View attachment 938796

Kikosi cha timu ya Taifa cha Tanzania 'Taifa Stars' leo kimeshindwa kuandika historia ya kukata tiketi ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika(Afcon) baada ya kupoteza pointi tatu mbele ya Lesotho kwa kufungwa bao 1-0.

Stars wapo kundi L lenye timu ya Uganda iliyofuzu baada ya kufikisha pointi 13 huku timu ya Lesotho ikifikisha pointi 5 sawa na Stars, Cape Verde ina pointi 4

View attachment 938798

Kwa kupoteza mchezo wa leo matumaini ya ya timu itakayoungana na Uganda Afcon Cameroon mwakani kwa kundi L yamebaki kwenye mechi za mwisho zitakazofanyika mwakani

Stars watacheza na Uganda nyumbani mwezi Machi mchezo wa marudiano, huku Lesotho wakicheza na Cape Verde wenye pointi 4

Ikumbukwe kuwa mara ya mwisho Stairs kufuzu kucheza michuan hiyo ni mwaka 1979

View attachment 938797
Hakuna jinsi wazitapike tu zile million 50
 
Kichwa cha mwendawazimu
IMG_20171013_221846_350.jpeg
 
Makosa ya Aishi Manula kutufungisha yamefichwa na kivuli cha watu kulalamikia upangaji kikosi Wa Amunike. Kiukweli Manula alifanya makosa mawili yanayofanana amabapo la kwanza alipangulia mpira kwa maadui wakaachia mkwaju mkali ambao Yondani aliu clear akiwa kwenye mstari Wa goli huku Aishi yeye akigalagala kusikojulikana. Kosa la pili aliwapangulia mpira maadui wakatandika hedi Nyoni na Kichuya wakiwa kwenye mwamba mpira ukawapita viunoni. Pamoja na hayo yote Aishi ajifunze zaidi kucheza krosi na kona kwa ushupavu Mkubwa siyo anatoka kiajabu ajabu na kupangua mipira kilegelege na kiajabu ajabu
 
Back
Top Bottom