Kufuzu AFCON 2023 | Taifa Stars 0-2 Algeria | Uwanja wa Benjamin Mkapa

Mwamnyeto kasababisha tena lakini sio mbaya tumejitahidi hii hii moja tuliyopigwa twende nayo hivyo hivyo.

Japo pia hata sammata na msuva pale walichezea nafasi pia.

Dickson job amejitahidi sana
Mimi ni Yanga! Lakini kwenye ukweli, nitasema. Mwamnyeto anabebwa sana na Bangala! Ni beki anaye jisahau sana kwenye kufanya marking!

Anahitaji golikipa wa kumpigia kelele muda wote! Bahati mbaya Aishi Manula hawezi kufanya hivyo.
 
kipindi cha pili imeanza mabadiliko upande wa Tanzania

Kibu Denis anaingia badala ya Kibabage
 
Upo sawa kabisa mkuu, Mwamnyeto kimeo sana aiseeh.
Mwamnyeto mchezaji aliyejaliwa kila kitu! ana umbo zuri! Umri unamruhusu!

Tatizo lake kubwa ni kuzubaa, na kutochukua maamuzi ya haraka awapo uwanjani. Sehemu ya kuruka ili kuokoa, unakuta anautazama tu mpira kwa macho!

Yaani anatakiwa kufanyia kazi huu udhaifu wake, kabla mambo hayaja haribika kabisa.
 
Kiukweli Msuva na yeye anatakiwa kupumzishwa. Angeingia George Mpole na Kibu Dennis, hala Msuva na Kibabage wangepumzishwa.
Shot on target zao 2 moja imekuwa goli, jamaa wanacheza vizuri na nafasi.
 
Bora hata mngenipa mimi timu aisee! Ningekuwa nadesa mawazo yenu wakati mpira unaendelea, na kuyafanyia kazi faster.
Kabisa kaka. Sasa timu haichezi tupo nyumbani, kila mtu anategemea sie kufungwa, kwa nini tusishambulie tuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…