Mimi nasema hivi kuna wengi hawapendi maendeleo yetu kwa nini kila mechi hasa hizi tunazocheza na waarabu lazima ianzie TZ na kumalizia ugenini? Kulikoni. Sijaiangalia hii mechi ziwezi kusema mengi
We ni mkiya eeeh.
Aibu sana, kwa kuweka rekodi kwa timu yetu tangu tuhaza kushiliki kwenye kufuzu kumbe la dunia. Dah kweli kocha hajiuzulu kabsa. Hapa kazi tu yaan tumefungwa sijui kazi hijafanyika uwanjan.
Kama unajua unajua tu, haijalishi unaanzia wapi, tusitafute sababu, lazima tukubali uwezo wetu bado sana kushindana na timu kama algeria, Shaffi daudi kuna siku alisema ukweli kuwa tusidanganyane hatuna uwezo wa kushindana na timu kubwa kubwa hizi, weee alishambuliwa sana, eti sio mzalendo wa nchi yake!!! Hata leo julio amesema, sasa tunapenda kufarijiana tu, na leo kama wasingeanza ubishoo tungekula 15!!!!.wewe malawi tu kumfunga ni shida unazungumzia algeria!!! Eti hizo ranking za fifa ni namba tu!!!!!
Hadi mtakapoacha fitna, majungu, unafiki na kuongea sana. Ifikie mahali siasa iwekwe kando, tuwekeze kwenye michezo.
Wa Tanzania tunaongea kupitiliza, ujuaji mwingi, wengine hawajui kitu lakini uropokaji mwingi kana kwamba tunajua sana. Tusipojitambua hatifiki popote.