Kugombania hivi iko siku tutaja toana roho wallahi

Kinyonyoke

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2016
Posts
3,498
Reaction score
13,138
Ni kituoni Simu2000 ama hupendelea kukiita zaidi Mawasiliano, tumeketi vyema tukisubir daladala mbali kidogo na hapo tulipoketi kimesimama kibao wima mithili ya mwanajeshi achezaye kwata juu yake kukiwa na maandishi T\Kimanga, T\Segerea hii ikimaanisha kuwa abiria hawa walioko busy na simu zao wooote wanaelekea moja kati ya maeneo hayo.Swadakta tunaendelea kusubiri huku mara kwa mara shingo zikigeuka kutazama kule 🚃 dala dala zinapoingilia,kwa matarajio makubwa.Lakini dala dala hazikutokea kwa muda tuliohitaji zitokee, basi ikawa kila mtu anapambana na hali yake alimuradi muda usonge, wengine macho yao yalitazama screen za simu zao, na yaliamuliwa kunyanyuka pale tu muungurumo wa gari uliposikika,wengine walipiga miayo hovyo wengine walikuwa wakipiga soga za umbea,wengine walizungumza na simu zao, huku wengine kama mimi walijikunyata kimya kama vile hawana habari na yale yanayoendelea duniani wakizama sawia katika dimbwi zito la fikra pevu, Ghafla mtoto wa Vuuup! aliibuka mara baada ya daladala inayoelekea Tabata Segerea ilipowasili, kukuru kakara na vurumai la ajabu lilivudumka pale, na watoto Amani na nduguye Usalama wakatoweka ghafla huku mtoto ustaarabu akitimka na asitake kujua kinachoendelea nyuma.Sasa kile nilichowahi kukisoma shuleni na kukizika kwenye daftari langu la biology kiitwacho Survival for the fittest yaani wenye nguvu ndio watakaopona(si tafsir yke) kile kitu kilifufuka na nikawa nakishuhudia kwa macho, si kina mama wala baba, wazee,wala watoto aliyekuwa nyuma kila mmoja alikuwa mbele akitaka kuingia kwenye daladala na kupata siti.Cha ajabu watu walilazimisha kuingia kabla ya wakushuka hawajashuka, ikawa kimbembe mlangoni, katika seke seke hili mzee mmoja aliejiona mwamba alisimama mlangoni akizuia waingiaji wasiingie, ili watokaji watoke sasa unaambiwa sekunde kumi nyingi toka yule mzee alipoamua kufanya kitendo hiki ambacho waingiaji walikitafsiri kama cha kifedhuli, asalaale! Mzee mwamba alijikuta mita kadhaa toka mlangoni pale akigaa gaa chini duh ama kweli watu wamevurugwa.Kitendo hiki kiliamsha cheko kubwa toka katika umati ule hata mzee mwamba nae aliyepigwa kumbo nae akajikuta anajichekea, hata waliokuwa wamefumba vinywa vyao kwa muda mrefu huu ukawa wasaa mubashara wakuvifumbua, watu wakasahau shida zao kwa muda.Naam dakika mbili mbele umati ule uliokuwa nje wote uliishia ndani ya dala dala hili, waastaarabu wote hawakupata siti😁😀.Vicheko navyo vilikuwa vinaishia huku waliokalia siti wakiendelea kufuta jasho, naye dereva bila ajizi huyooo akaondoa gari.

Baada ya stori sasa turudi kwenye kichwa jamani ustaarabu umeelekea wapi kwani ukisubiri watu wengine washuke utakatika miguu au itaingia tumboni?
Kwani ukisimama kwenye daladala utateseka?mbona umesimama mara kibao tu kwenye daladala? Ndo nn hii kujivua ustaarabu kwa kitu
Kisichokua na maana yeyoye?
Tafakari.lakini kugombania dala dala is very funny, its lifetime experience 😁😁😁
 
Poleni sana,mi huwa nawaacha wagombaneee kishanaingia nasimama,cha ajabu hao wanaogombania wengine wanashuka tu kituo kinachofuata,hivyo hunipisha
 
Ni kituoni Simu2000 ama hupendelea kukiita zaidi Mawasiliano, tumeketi vyema tukisubir daladala mbali kidogo na hapo tulipoketi kimesimama kibao wima mithili ya mwanajeshi achezaye kwata juu yake kukiwa na maandishi T\Kimanga, T\Segerea hii ikimaanisha kuwa abiria hawa walioko busy na simu zao wooote wanaelekea moja kati ya maeneo hayo.Swadakta tunaendelea kusubiri huku mara kwa mara shingo zikigeuka kutazama kule [emoji588] dala dala zinapoingilia,kwa matarajio makubwa.Lakini dala dala hazikutokea kwa muda tuliohitaji zitokee, basi ikawa kila mtu anapambana na hali yake alimuradi muda usonge, wengine macho yao yalitazama screen za simu zao, na yaliamuliwa kunyanyuka pale tu muungurumo wa gari uliposikika,wengine walipiga miayo hovyo wengine walikuwa wakipiga soga za umbea,wengine walizungumza na simu zao, huku wengine kama mimi walijikunyata kimya kama vile hawana habari na yale yanayoendelea duniani wakizama sawia katika dimbwi zito la fikra pevu, Ghafla mtoto wa Vuuup! aliibuka mara baada ya daladala inayoelekea Tabata Segerea ilipowasili, kukuru kakara na vurumai la ajabu lilivudumka pale, na watoto Amani na nduguye Usalama wakatoweka ghafla huku mtoto ustaarabu akitimka na asitake kujua kinachoendelea nyuma.Sasa kile nilichowahi kukisoma shuleni na kukizika kwenye daftari langu la biology kiitwacho Survival for the fittest yaani wenye nguvu ndio watakaopona(si tafsir yke) kile kitu kilifufuka na nikawa nakishuhudia kwa macho, si kina mama wala baba, wazee,wala watoto aliyekuwa nyuma kila mmoja alikuwa mbele akitaka kuingia kwenye daladala na kupata siti.Cha ajabu watu walilazimisha kuingia kabla ya wakushuka hawajashuka, ikawa kimbembe mlangoni, katika seke seke hili mzee mmoja aliejiona mwamba alisimama mlangoni akizuia waingiaji wasiingie, ili watokaji watoke sasa unaambiwa sekunde kumi nyingi toka yule mzee alipoamua kufanya kitendo hiki ambacho waingiaji walikitafsiri kama cha kifedhuli, asalaale! Mzee mwamba alijikuta mita kadhaa toka mlangoni pale akigaa gaa chini duh ama kweli watu wamevurugwa.Kitendo hiki kiliamsha cheko kubwa toka katika umati ule hata mzee mwamba nae aliyepigwa kumbo nae akajikuta anajichekea, hata waliokuwa wamefumba vinywa vyao kwa muda mrefu huu ukawa wasaa mubashara wakuvifumbua, watu wakasahau shida zao kwa muda.Naam dakika mbili mbele umati ule uliokuwa nje wote uliishia ndani ya dala dala hili, waastaarabu wote hawakupata siti[emoji16][emoji3].Vicheko navyo vilikuwa vinaishia huku waliokalia siti wakiendelea kufuta jasho, naye dereva bila ajizi huyooo akaondoa gari.

Baada ya stori sasa turudi kwenye kichwa jamani ustaarabu umeelekea wapi kwani ukisubiri watu wengine washuke utakatika miguu au itaingia tumboni?
Kwani ukisimama kwenye daladala utateseka?mbona umesimama mara kibao tu kwenye daladala? Ndo nn hii kujivua ustaarabu kwa kitu
Kisichokua na maana yeyoye?
Tafakari.lakini kugombania dala dala is very funny, its lifetime experience [emoji16][emoji16][emoji16]

Kwa uandishi wako mkuu unafaa kua msimulizi
Unaweza kutumia peni

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hata siku moja sijawahi soma uzi post ndefu hivi katika hili jukwaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom