Masaningala
JF-Expert Member
- Nov 19, 2010
- 543
- 199
Ndugu wanaJF, Nimeipitia Rasimu ya Katiba mpya kwa haraka haraka na nikagundua kitu kimoja muhimu sana kinakosekana. Rasimu ya Katiba katika utangulizi wake imeshindwa kumtambua muumba wa ardhi ambae tunamtaja kwa ndimi zetu. Kwanza wimbo wetu anaanza kwa maneno: "Mungu ibariki Tanzania,.............." Bunge linapokutana linaanza kwa kusoma dua na kutamka: Ewe Mwenyeenzi Mungu ulieziumba mbingu na nchi, libariki bunge hili............." Mkuu wa nch anapohutbia taifa humalizia kwa kutamka, Mungu ibariki, Afrika, Mungu ibariki Tanzania". Mimi mara nyingi hujiuliza huyu ni Mungu gani mbona kwenye Katiba hajatajwa? Usikute hata mabalaa mengi tunayoyapata ni kwamba Katiba yetu haitamki kwa uwazi uwepo wa Mungu. Wazo hili nililipendekeza kabisa kwa kuzungumza mbele ya tume lakini nilipopitia sikuliona. Bado sijakata tamaa, naomba walioteuliwa kwenye Mabaraza walichukue hili. Napendekeza kwenye Utangulizi, kitu cha kwanza maneno haya: "SSI WANANCHI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WENYE DINI NA IMANI MBALIMBALI, TUNATAMBUA UWEPO WA MUNGU ALIYEZIUMBA MBINGU NA NCHI PAMOJA NA WANADAMU NA VIUMBE VINGINE VYOTE VILIVYOMO ARIDHINI, BAHARINI NA ANGANI. TUNATAMBUA PIA KUWA WANADAMU WAMEPEWA MAMLAKA NA MUNGU YA KUTAWALA VIUMBE VINGINE NA KUITUNZA ARDHI NA MIMEA YOTE BILA UCHAVUZI WA MAZINGIRA" Baada ya Katiba kutamka haya sasa iendelee na matamko mengine yaliyopo kwenye Katiba. Je mnaonaje hili. Nawasilisha.