Na kwa nini uhame? Ina maana unajaribisha fani hujui unapenda nini maishani? Tabia mbaya hiyo. Kaa chini uliza wazoefu kabla hujaamua utumikeje. Ukifanya ufikiriiavyo unaoa leo halafu kesho unataliki na kuoa mwingine kisha unataliki na ....... Nilipokuwa mdogo baba yangu aliniasa nifikiri kabla ya kuamua mambo magumu nisifuate upepo. Aliniambia mke wako wa kwanza ndie mkeo halisi, wengine ni photokopi, kwa sababu tabia ya kuwa popo haijengi kwa binadamu. Ukianza kutaliki utataliki sana. Mwalimu Nyerere alisema katabia ka ubaguzi na kutokuwa na msimamo ni sawa na kula nyama ya ntu. Ukimla asumani leo utaendelea tu kula wengine. Kwa hiyo ndugu yangu unahitaji counselling kabla hujaamulia carear yako. Utapoteza muda mwingi na kujikuta unastaafu hujatimiza ndoto halisi ya kwako. Leo Anglikana, kesho Katholic, keshokutwa Shia, halafu kesho Suni, halafu unarudi TAG halafu Pentekoste, mara kwa Kakobe mara kwa Mwingira, mpaka utajikuta mapepo tu yanakuingia na wale majamaa wa kanumba watakufuatilia, angalia Diamond anavyofuatiliwa sasa. Simama amua , nenda mbele. Ila ukiwa na kimoja hicho unaweza kujisomea fani za nyongeza maana ni ruksa kuongeza value.