Wewe ungepaswa kuanza kutueleza ungependa fani gani kuisomea. Kwa maana kati ya hizo taaluma za SUA zote ni nzuri na mahitaji yake ni makubwa sana, hapa nchi na kwenye nchi za jirani.
Kuhusu kuhama chuo (facult sio sawa na course, facult ni sawa na college, usiitumie kimakosa); chuo unaweza kuhama kwa kufuata taratibu za TCU, lakini kwa uchache wa nafasi zilizopo SUA (ina tegemea kama course hizo kama bado zinahitaji watu au dirisha limefungwa) sidhani kama TCU watakupeleka, kama utaweza nenda direct ukafanye maombi (sidhani kama wamefunga admission), ila ujue, ukienda Direct mkopo hupati. Kwa hiyo pima hapo.