Kuhamasishwa au kuhamasika kufanya kitu ni kama cheche, kinachohitajika ni nidhamu yako juu ya unachikifanya

Kuhamasishwa au kuhamasika kufanya kitu ni kama cheche, kinachohitajika ni nidhamu yako juu ya unachikifanya

Victor Mlaki

JF-Expert Member
Joined
May 1, 2016
Posts
4,151
Reaction score
4,277
Kuhamasishwa au kuhamasika kupitia wahamasishaji "motivational speakers" au njia nyingine yoyote ile ni kama cheche ya kuwasha moto ndani yako na kitakachokufanya uendeleze moto uliowashwa siyo kuhamasishwa ila ni nidhamu yako "discipline" juu ya unachokifanya.

Wahamasishaji hufanya kazi ya kuanzisha cheche "to start the spark" ndani ya mtu ila jukumu la kuifanya cheche hiyo kuwa moto yaani kufikia matokeo ni la mhamasishwaji.

Ikumbukwe mtu yeyote yule ana nguvu au ni nguvu na nguvu hiyo Inaweza kuwa nguvu tuli "potential energy" kinachofanyika katika uhamasishwaji ni kuifanya nguvu tuli kuwa nguvu mtembeo "kinetic energy". Hapa ndipo ilipo kazi ya wahamasishaji "motivational speakers" ila kiuhalisia kazi kubwa haipo kwao ila kwa wahamasishwaji.

Nidhamu ndiyo inayoweza kumfanya mtu kuendelea mbele hata kama akikutana na changamoto. Ukihamasishwa na kuhamasika bila kuwa na nidhamu ekewa umepiga hatua moja tu bado nyingine muhimu zaidi kwa sababu tatizo siyo kuanzisha moto ndani yako ila kuuendeleza moto huo.

Haisaidii sana kupenda kupewa hamasa au kutiwa moyo kama hautajiwekea nidhamu juu ya matamanio yako. Changamoto na matatizo ni njia muhimu sana za kumsaudia mtu kujifunza. Mwanadamu hujifunza vizuri sana anapokutana na changamoto.
 
Back
Top Bottom