Sam Seaborn
Member
- Aug 20, 2011
- 98
- 39
Naona wote wanakukatisha tamaa lakini wazo lako linawezekana maana kilimo sio mjini.. wamejisahau na kukupa mashaka ya mjini wakati wewe unazungumzia kilimo. Mashamba yapo hasa maeneo ya Kiteto (kuna uhakika wa mvua), Makuyuni (mvua ni haba) na pia unaweza kuelekea Kilimanjaro (West Kilimanjaro) kuna mvua za kutosha na ardhi nzuri ya kilimo lakini tayari inamilikiwa na ma-settler ila wapo wanaouza.. Kazi kwako..Jamani mimi nafkiria kununua shamba ili nihamie Arusha nikaishi kama farmer/settler kule kama wale wa Zimbabwe au Kenya Je kuna maoni gani? Maeneo gani? nafkiria kununua shamba la eka kama 500 au 1000 hivi....
Jamani mimi nafkiria kununua shamba ili nihamie Arusha nikaishi kama farmer/settler kule kama wale wa Zimbabwe au Kenya
Je kuna maoni gani? Maeneo gani? nafkiria kununua shamba la eka kama 500 au 1000 hivi....
Kama una mtaji wa kutosha hamia tu ila kwa ukubwa huo unaotaka sidhani kama utapata kwa hapa Arusha. Piajiandae kununua heka moja mil 40.
Mimi nakushauri kama unataka kweli kuwa settle hamia Iringa, Njombe hasa Ludewa, Rukwa au Katavi. Huko bado kuna ardhi nzuri kwa kilimo na tena kwa bei nafuu.