Uchaguzi 2020 Kuhamisha Magoli ndiyo mbinu mpya ya CCM

Uchaguzi 2020 Kuhamisha Magoli ndiyo mbinu mpya ya CCM

Lord denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
15,819
Reaction score
33,255
Anaandika Lord Denning wa JF,

Leo nimecheka sana!

Kuna clip watu wa CCM wameitengeneza na wanaisambaza ikimuonesha Tundu Lissu akiwa kwenye kampeni akiongelea suala la Bunge na wabunge hawajui bei wala mikataba ya ndege!

Kwenye clip hii wana CCM wameunganisha na scene ya Halima Mdee akijadili bungeni kipengele kinachoonesha serikali wametenga fedha za kununulia ndege! Kwa mwaka uliopita bilioni 500+ na mwaka aliokuwa akichangia bungeni bilioni 400+ na na wana CCM wameunganisha zile clips ili kumaanisha kuwa Bunge linajua bei za ndege na wabunge wanajua bei za ndege, Huu ni upotoshaji mkubwa sana unaofanywa na CCM na watu wao!

Hoja ya Lissu ni ipi hapa?
1.
Hoja ya Lissu ni kuwa hakuna popote pale serikali ilipeleka bungeni mikataba ya manunuzi ya hizo ndege kuonesha serikali walinunua kila ndege kwa shilingi ngapi?

2. Serikali kusema bungeni imetenga bilioni 400 au bilioni 500 kwa ajili ya ununuzi wa ndege haimaanishi kuwa hiyo ndo bei halisi ya ndege moja au mbili. Wananchi kupitia wabunge wao wana haki ya kuona mikataba halisi ya ununuzi ili kujiridhisha kama kweli ndege zilinunuliwa kwa bei tajwa! Hadi leo haijulikani kwa wabunge wala wananchi bei ya kila ndege ilikuwa ni shilingi ngapi kwa sababu mikataba waliosaini ya mauziano haijaoneshwa popote na wala haikupelekwa bungeni?

Lissu anamaanisha nini?
Anachomaanisha Lissu ni kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa Tanzania kuwa tumepigwa au kuibiwa kwenye ununuzi wa ndege hizi Kwa sababu inafahamika kuwa kwenye maeneo ambayo kuna ufisadi mkubwa ni kwenye manunuzi ya serikali!

Inawezekanaje mtu anadai amenunua ndege kwa cash na mikataba ya manunuzi ya ndege hizo haikupelekwa bungeni ili wananchi wapate kuridhika na matumizi ya kodi zao?

Share na watu wengi zaidi ili kuzuia upotoshaji wa CCM na watu wao!!

Asanteni!
 
Back
Top Bottom