Kuharakisha Katiba Mpya tuunde 'Coalition of the Willing'

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kupata Katiba mpya haiwezi kuwa lelemama.

Tutapata katiba mpya mapema kwa kuidai kupitia chombo ambacho kitaulenga upatikanaji wake kama agenda pekee.

Vyama vya siasa wana agenda zao. Watu binafsi nao wana agenda zao pia zinazoweza kuwa zaidi ya hii.

Ni vyema vyama siasa, watu binafsi na asasi mbalimbali wakawa wajumbe humo kwenye chombo hiki wao kama vyama, asasi au watu binafsi.

Hii itasaidia kuondoa unyanyapaa Kwa washiriki, kupanua wigo wa ushiriki na ku focus kwenye hoja za msingi pekee za kulenga kumfunga Paka kengele.

Tuunganishe nguvu katiba mpya ni sasa na inawezekana.
 
Huwa naona huu mfumo uliotulea chini ya katiba mbovu tuliyonayo umetubana sana, hasa kwa watu binafsi na taasisi za kiraia, umetulazimisha wengi { kama sio wote}tuwe watumwa wa serikali iliyopo madarakani bila kupenda.

Tunaogopa kutoa maoni yetu kwa kuhofia kuwaudhi wenye nchi, na kwa namna walivyopewa madaraka makubwa na hii katiba mbovu iliyopo, basi ndio tunajikuta tunazidi kuwa waoga na kuzidi kutawaliwa indirectly [kimawazo].

Tumeshaona mifano jinsi watu binafsi wenye ushawishi kwa jamii waliojaribu kujiunga na upinzani, au kuwa na mawazo huru kinyume na mapenzi ya watawala, walivyofanywa na dola/mamlaka, ikiwemo kubambikiwa kodi nk.

Sasa ni kwa namna gani tunaweza kujinasua kutoka kwenye huu mkwamo, ili kila mmoja wetu aweze kutoa maoni yake kwa uhuru, bila hofu yoyote, hasa ya kuwakera wakubwa wenye nchi?

Muhimu tukumbuke jambo, japo kuwa wengi tunaitaka Katiba Mpya, lakini bado tunaishi kwenye kivuli cha katiba mbovu ya sasa, ni kwa vipi tutatoka kwenye hiki kivuli na kuwa huru kutoa maoni yetu bila hofu yoyote? kwangu huu ndio mtego tulionao kwa sasa.
 
Huwa naona huu mfumo uliotulea chini ya katiba mbovu tuliyonayo umetubana sana, hasa kwa watu binafsi na taasisi za kiraia, umetulazimisha wengi tuwe watumwa wa serikali iliyopo madarakani bila kupenda.

Tunaogopa kutoa maoni yetu kwa kuhofia kuwaudhi wenye nchi, na kwa namna walivyopewa madaraka makubwa na hii katiba mbovu iliyopo, basi ndio tunajikuta tunazidi kuwa waoga na kuzidi kutawaliwa indirectly [kimawazo].

Tumeshaona mifano jinsi watu binafsi wenye ushawishi kwa jamii waliojaribu kujiunga na upinzani, au kuwa na mawazo huru kinyume na mapenzi ya watawala, walivyofanywa na dola/mamlaka, ikiwemo kubambikiwa kodi nk.

Sasa ni kwa namna gani tunaweza kujinasua kutoka kwenye huu mkwamo, ili kila mmoja wetu aweze kutoa maoni yake kwa uhuru, bila hofu yoyote, hasa ya kuwakera wakubwa wenye nchi?

Muhimu tukumbuke jambo, japo kuwa wengi tunaitaka Katiba Mpya, lakini bado tunaishi kwenye kivuli cha katiba mbovu ya sasa, ni kwa vipi tutatoka kwenye hiki kivuli na kuwa huru kutoa maoni yetu bila hofu yoyote? kwangu huu ndio mtego tulionao kwa sasa.
Hii Katiba ni kwa ajiri ya wote lakin ni wazi wenye guts za kuidai by hooks and crooks ni wachache!
Katiba si kwa ajiri ya wanasiasa lakin hakuna namna ya kwenda mbele bila wanasiasa!
Sasa tume abuse chances za kuwatumia wanasiasa, hatutafika popote.
Maana siasa na wanasiasa ndo gari la wabeba wadai Katiba!
Nahofia hata Bw Freeman amechoshwa na kufia misukule. Huenda anaimba "...if you can't conquer them ......"
Lisu ndo amebaki ananata na beats mana ni ajira.
Kila reasonableman , ajijibu anawajibika kiasi gani kutia shinikizo?
Zaid ya huu u keyboard warriorship! Mimi niko tayari kwa lolote lisilozid mtari wa maombi, sala na dua!!!!
( joke.Naamin ndugu zetu waisram wakitaka Katiba itapatikana, maana Kudai haki ni ibada na kutokudai haki ni kufuru!
Wale wa unafiki ....akupigaye shavu la kushoto.... sidhan watasaidia!)
".....UKITAKA AMANI JIANDAE KWA VITA...."
 
Huwa naona huu mfumo uliotulea chini ya katiba mbovu tuliyonayo umetubana sana, hasa kwa watu binafsi na taasisi za kiraia, umetulazimisha wengi { kama sio wote}tuwe watumwa wa serikali iliyopo madarakani bila kupenda.

Tunaogopa kutoa maoni yetu kwa kuhofia kuwaudhi wenye nchi, na kwa namna walivyopewa madaraka makubwa na hii katiba mbovu iliyopo, basi ndio tunajikuta tunazidi kuwa waoga na kuzidi kutawaliwa indirectly [kimawazo].

Tumeshaona mifano jinsi watu binafsi wenye ushawishi kwa jamii waliojaribu kujiunga na upinzani, au kuwa na mawazo huru kinyume na mapenzi ya watawala, walivyofanywa na dola/mamlaka, ikiwemo kubambikiwa kodi nk.

Sasa ni kwa namna gani tunaweza kujinasua kutoka kwenye huu mkwamo, ili kila mmoja wetu aweze kutoa maoni yake kwa uhuru, bila hofu yoyote, hasa ya kuwakera wakubwa wenye nchi?

Muhimu tukumbuke jambo, japo kuwa wengi tunaitaka Katiba Mpya, lakini bado tunaishi kwenye kivuli cha katiba mbovu ya sasa, ni kwa vipi tutatoka kwenye hiki kivuli na kuwa huru kutoa maoni yetu bila hofu yoyote? kwangu huu ndio mtego tulionao kwa sasa.

Ni wazi kuwa siku zote wanaotaka katiba mpya watakuwa ni wengi kuliko wenye guts za kuidai. Kudai katiba mpya si lelemama. Kuna gharama za kulipa.

Kutegemea kuwa hii itakuja bure bure au kwa wepesi ni kujidanganya.

Badala ya kubakia kulaumiana, kunyapaana, kuitana majina kwenye jitihada hizi, "coalition of the willing" ingeweza kutufaa zaidi. Ikawa wazi kwa kila mwenye kutaka kuwamo.

Katiba mpya haihitaji watu wote. Opportunists wapo kila mahali. Wenye kudhamiria haswa pia wapo na tunatosha sana. Isitoshe pia kuwamo humu haisimamishi kuidai vyamani.

Wengine watatukuta tutakapokuwa tumefikia.

Lissu, Mpina, Slaa, Zitto, Lipumba, Chadema, CUF, Zitto, wewe na yule wenye kuona inafaa wakakaribishwa.

Jitihada zozote za kudai katiba mpya haziwezi kuwekewa kizingiti na yeyote aliyedhamiria hasa kwenye mpambano huu.
 
Hii Katiba ni kwa ajiri ya wote lakin ni wazi wenye guts za kuidai by hooks and crooks ni wachache!
Katiba si kwa ajiri ya wanasiasa lakin hakuna namna ya kwenda mbele bila wanasiasa!
Sasa tume abuse chances za kuwatumia wanasiasa, hatutafika popote.
Maana siasa na wanasiasa ndo gari la wabeba wadai Katiba!
Nahofia hata Bw Freeman amechoshwa na kufia misukule. Huenda anaimba "...if you can't conquer them ......"
Lisu ndo amebaki ananata na beats mana ni ajira.
Kila reasonableman , ajijibu anawajibika kiasi gani kutia shinikizo?
Zaid ya huu u keyboard warriorship! Mimi niko tayari kwa lolote lisilozid mtari wa maombi, sala na dua!!!!
( joke.Naamin ndugu zetu waisram wakitaka Katiba itapatikana, maana Kudai haki ni ibada na kutokudai haki ni kufuru!
Wale wa unafiki ....akupigaye shavu la kushoto.... sidhan watasaidia!)
".....UKITAKA AMANI JIANDAE KWA VITA...."
Katiba ni kwa ajili ya wananchi, ile ndio sheria mama ya nchi ambayo kila mwananchi anatakiwa kuifuata, unaposema ni kwa ajili ya wanasiasa unakosea.

Haya mawazo ndio yanafanya wengi wabaki nyuma na kuwaaachia wanasiasa wafanye kila kitu, ndio maana mbele umeandika unahofia hata Mbowe anaweza kuwa amechoka kuwapigania wasiojielewa, anafikiria if you can't conquer...

Huko chini ulipoingiza misimamo ya kidini naona ndio umevuruga kabisa, kwasababu umeonesha vile dini mbili tofauti, zilivyo na mitazamo tofauti kwenye kudai haki, kundi la kwanza la wanafiki [kwa mtazamo wako] linaamini ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la kulia, na kundi la pili la kudai haki kwa mapambano.

Sasa haya makundi mawili tofauti, yenye mitazamo tofauti, yataunganishwa vipi kwenye kuidai Katiba Mpya ya watanzania?

Binafsi, naamini ili tuweze kulifikia lengo letu mapema, vyema.hiyo mitazamo miwili tofauti ya makundi mawili tofauti ifutwe, twende tukaitafute Katiba Mpya tukiwa kama watanzania tunaounganishwa na dhamira zetu kwenye kudai haki zetu, kwasababu maumivu ya Katiba mbovu iliyopo, yanatuumiza sote bila kujali dini zetu.
 
Ni wazi kuwa siku zote wanaotaka katiba mpya watakuwa ni wengi kuliko wenye guts za kuidai. Kudai katiba mpya si lelemama. Kuna gharama za kulipa.

Kutegemea kuwa hii itakuja bure bure au kwa wepesi ni kujidanganya.

Badala ya kubakia kulaumiana, kunyapaana, kuitana majina kwenye jitihada hizi, "coalition of the willing" ingeweza kutufaa zaidi. Ikawa wazi kwa kila mwenye kutaka kuwamo.

Katiba mpya haihitaji watu wote. Opportunists wapo kila mahali. Wenye kudharimia haswa pia wapo na tunatosha sana. Isitoshe pia kuwamo humu haisimamishi kuidai vyamani.

Wengine watatukuta tutakapokuwa tumefikia.

Lissu, Mpina, Slaa, Zitto, Lipumba, Chadema, CUF, Zitto, wewe na yule wenye kuona inafaa wakakaribishwa.

Jitihada zozote za kudai katiba mpya haziwezi kuwekewa kizingiti na yeyote aliyedhamiria hasa kwenye mpambano huu.
"Wengine watatukuta tutakapokuwa tumefikia"

Hii kwangu ndio pointi ya msingi.
 
Katiba ni kwa ajili ya wananchi, ile ndio sheria mama ya nchi ambayo kila mwananchi anatakiwa kuifuata, unaposema ni kwa ajili ya wanasiasa unakosea.

Haya mawazo ndio yanafanya wengi wabaki nyuma na kuwaaachia wanasiasa wafanye kila kitu, ndio maana mbele umeandika unahofia hata Mbowe anaweza kuwa amechoka kuwapigania wasiojielewa, anafikiria if you can't conquer...

Huko chini ulipoingiza misimamo ya kidini naona ndio umevuruga kabisa, kwasababu umeonesha vile dini mbili tofauti, zilivyo na mitazamo tofauti kwenye kudai haki, kundi la kwanza la wanafiki [kwa mtazamo wako] linaamini ukipigwa shavu la kushoto, geuza na la kulia, na kundi la pili la kudai haki kwa mapambano.

Sasa haya makundi mawili tofauti, yenye mitazamo tofauti, yataunganishwa vipi kwenye kuidai Katiba Mpya ya watanzania?

Binafsi, naamini ili tuweze kulifikia lengo letu mapema, vyema.hiyo mitazamo miwili tofauti ya makundi mawili tofauti ifutwe, twende tukaitafute Katiba Mpya tukiwa kama watanzania tunaounganishwa na dhamira zetu kwenye kudai haki zetu, kwasababu maumivu ya Katiba mbovu iliyopo, yanatuumiza sote bila kujali dini zetu.

Nimeangalia pote alipoandika mjumbe Rwaz, sijaona popote aliposema katiba ni ya wanasiasa.

"Nishauri kumrejea tena huyu ndugu."

Kuhusu dini hapo naona ni angalizo tu kuonyesha tukiitaka katiba mpya hata kesho mbona inapatikana Kwa kujifunza kutoka kwa dini hizo 2?

"Zingatia msimamo wa moja kudai haki ni ibada wakati kutodai haki ni kufuru!"

Kwa hakika huyu bwana ana hoja.

Tukumbuke ukweli siku zote ni mchungu.

Ninakazia:

Paragraph yake ya pili, ameandika; "Katiba si kwa ajili ya wanasiasa, lakini hatuna namna kwenda mbele bila ya wanasiasa"

Hapo kwangu nimetafsiri alichoandika ni sawa na kusema, bila wanasiasa hakuna Katiba Mpya, mategemeo yetu yote yapo kwao, ndio maana nikamtaka afute huo mtazamo kwa kumwambia, Katiba ni ya watanzania wote bila kujali kundi lolote.
 
Kupata Katiba mpya haiwezi kuwa lelemama.

Tutapata katiba mpya mapema kwa kuidai kupitia chombo ambacho kitaulenga upatikanaji wake kama agenda pekee.

Vyama vya siasa wana agenda zao. Watu binafsi nao wana agenda zao pia zinazoweza kuwa zaidi ya hii.

Ni vyema vyama siasa, watu binafsi na asasi mbalimbali wakawa wajumbe humo kwenye chombo hiki wao kama vyama, asasi au watu binafsi.

Hii itasaidia kuondoa unyanyapaa Kwa washiriki, kupanua wigo wa ushiriki na ku focus kwenye hoja za msingi pekee za kulenga kumfunga Paka kengele.

Tuunganishe nguvu katiba mpya ni sasa na inawezekana.
Hiyo katibampya yako ikoaje? Ina muonekano upi? Ina nini na nini ambacho hakimo leo kwenye katiba? Na ilipitishwa au itapitishwa na bunge lipi?
 
Paragraph hiyo ya pili kwa mawazo yangu amekuwa wazi kuwa katiba si Kwa ajiri ya wanasiasa.

Ila nadhani hili la kwenda mbele amemaanisha vyama kama driving force ilikuwa muhimu kama fursa au mbaraka.

Vyama vya siasa vilikuwa katika nafasi njema zaidi ya kuongoza harakati hIzi.

Tunafikiria chombo kingine hatimaye kutokana na kuwa kila mtu anapomwachia mwingine hatimaye kinakuwa hakuna kinachoendelea.
 
Kupata Katiba mpya haiwezi kuwa lelemama.

Tutapata katiba mpya mapema kwa kuidai kupitia chombo ambacho kitaulenga upatikanaji wake kama agenda pekee.

Vyama vya siasa wana agenda zao. Watu binafsi nao wana agenda zao pia zinazoweza kuwa zaidi ya hii.

Ni vyema vyama siasa, watu binafsi na asasi mbalimbali wakawa wajumbe humo kwenye chombo hiki wao kama vyama, asasi au watu binafsi.

Hii itasaidia kuondoa unyanyapaa Kwa washiriki, kupanua wigo wa ushiriki na ku focus kwenye hoja za msingi pekee za kulenga kumfunga Paka kengele.

Tuunganishe nguvu katiba mpya ni sasa na inawezekana.
USHAURI MZURI NAUNGA MKONO HOJA
 
Hiyo katibampya yako ikoaje? Ina muonekano upi? Ina nini na nini ambacho hakimo leo kwenye katiba? Na ilipitishwa au itapitishwa na bunge lipi?
Kwenye katiba iliyopo unayajua haya:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Tunataka katiba nyingine kuyarekebisha ya namna hiyo. Yako mengi tu mjomba.

Wewe huoni hivyo?
 
Paragraph hiyo ya pili kwa mawazo yangu amekuwa wazi kuwa katiba si Kwa ajiri ya wanasiasa.

Ila nadhani hili la kwenda mbele amemaanisha vyama kama driving force ilikuwa muhimu kama fursa au mbaraka.

Vyama vya siasa vilikuwa katika nafasi njema zaidi ya kuongoza hakati hIzi.

Tunafikiria chombo kingine hatimaye kutokana na kuwa kila mtu anapomwachia mwingine hatimaye kinakuwa hakuna kinachoendelea.
Asante kwa ufafanuzi. Tukubaliane tu kwamba hali yetu kijamii tunahitaji kundi la wanasiasa kama wachezaji muhimu kiharakati.
Katiba na siasa haviachani sana.
Hata katika sheria tunasema wanatunga wabunge lakini draftsmen wana kazi nyeti sana ili sheria itafsirike ipasavyo!
Kila mara huwa nasubiri mwongozo wenye afya na unaomaanisha kweli tuipate katiba kama hali hii itaendelea ya baadhi ya wanufaika wa mapungufu ya katiba hii wataendelea kushupaa isibadirike.
BInafs nina iman ndogo na kinachoitwa majadiliano na mchakato tangu miaka 30 iliyopita had leo.
Naona tunaogelea kwenye delay tactics.
Nataman kuskia plan B.
 
Hakika, katiba mpya haitakuja kirahisi.
Huwa naona huu mfumo uliotulea chini ya katiba mbovu tuliyonayo umetubana sana, hasa kwa watu binafsi na taasisi za kiraia, umetulazimisha wengi { kama sio wote}tuwe watumwa wa serikali iliyopo madarakani bila kupenda.

Tunaogopa kutoa maoni yetu kwa kuhofia kuwaudhi wenye nchi, na kwa namna walivyopewa madaraka makubwa na hii katiba mbovu iliyopo, basi ndio tunajikuta tunazidi kuwa waoga na kuzidi kutawaliwa indirectly [kimawazo].

Tumeshaona mifano jinsi watu binafsi wenye ushawishi kwa jamii waliojaribu kujiunga na upinzani, au kuwa na mawazo huru kinyume na mapenzi ya watawala, walivyofanywa na dola/mamlaka, ikiwemo kubambikiwa kodi nk.

Sasa ni kwa namna gani tunaweza kujinasua kutoka kwenye huu mkwamo, ili kila mmoja wetu aweze kutoa maoni yake kwa uhuru, bila hofu yoyote, hasa ya kuwakera wakubwa wenye nchi?

Muhimu tukumbuke jambo, japo kuwa wengi tunaitaka Katiba Mpya, lakini bado tunaishi kwenye kivuli cha katiba mbovu ya sasa, ni kwa vipi tutatoka kwenye hiki kivuli na kuwa huru kutoa maoni yetu bila hofu yoyote? kwangu huu ndio mtego tulionao kwa sasa.
 
Asante kwa ufafanuzi. Tukubaliane tu kwamba hali yetu kijamii tunahitaji kundi la wanasiasa kama wachezaji muhimu kiharakati.
Katiba na siasa haviachani sana.
Hata katika sheria tunasema wanatunga wabunge lakini draftsmen wana kazi nyeti sana ili sheria itafsirike ipasavyo!
Kila mara huwa nasubiri mwongozo wenye afya na unaomaanisha kweli tuipate katiba kama hali hii itaendelea ya baadhi ya wanufaika wa mapungufu ya katiba hii wataendelea kushupaa isibadirike.
BInafs nina iman ndogo na kinachoitwa majadiliano na mchakato tangu miaka 30 iliyopita had leo.
Naona tunaogelea kwenye delay tactics.
Nataman kuskia plan B.

Penye wengi hakuharibiki jambo. Coalition of the willing haiwezi kukosa majibu:

Screenshot_20230212-170519.jpg

Mwendelezo huu ulikuwa mwema.

Tudai katiba kama movement kama Vipi isiyokuwa na utambulisho wa kivyama. Vyama vinaweza kuwa wajumbe kama walivyo wajumbe wengine kwenye huo mwamvuli.
 
Kupata Katiba mpya haiwezi kuwa lelemama.

Tutapata katiba mpya mapema kwa kuidai kupitia chombo ambacho kitaulenga upatikanaji wake kama agenda pekee.

Vyama vya siasa wana agenda zao. Watu binafsi nao wana agenda zao pia zinazoweza kuwa zaidi ya hii.

Ni vyema vyama siasa, watu binafsi na asasi mbalimbali wakawa wajumbe humo kwenye chombo hiki wao kama vyama, asasi au watu binafsi.

Hii itasaidia kuondoa unyanyapaa Kwa washiriki, kupanua wigo wa ushiriki na ku focus kwenye hoja za msingi pekee za kulenga kumfunga Paka kengele.

Tuunganishe nguvu katiba mpya ni sasa na inawezekana.
Nakuunga sana mkono, na hata mguu! Tuwasiliane na kupeana mikakati
 
Asante kwa ufafanuzi. Tukubaliane tu kwamba hali yetu kijamii tunahitaji kundi la wanasiasa kama wachezaji muhimu kiharakati.
Katiba na siasa haviachani sana.
Hata katika sheria tunasema wanatunga wabunge lakini draftsmen wana kazi nyeti sana ili sheria itafsirike ipasavyo!
Kila mara huwa nasubiri mwongozo wenye afya na unaomaanisha kweli tuipate katiba kama hali hii itaendelea ya baadhi ya wanufaika wa mapungufu ya katiba hii wataendelea kushupaa isibadirike.
BInafs nina iman ndogo na kinachoitwa majadiliano na mchakato tangu miaka 30 iliyopita had leo.
Naona tunaogelea kwenye delay tactics.
Nataman kuskia plan B.
Umechambua ukweli mtupu
 
Kwenye katiba iliyopo unayajua haya:

1. Katiba iliyopo haiwawajibishi baadhi ya watendaji wakuu kwa kuikiuka, na hii ni kwa mujibu wa katiba yenyewe?
2. kwa katiba iliyopo pana watu hata kama wakiiba, wakipora, wakiuwa, wakidhulumu nk hiyo ni halali kwa mujibu wa katiba yenyewe?
3. katiba iliyopo inawapa baadhi ya watu mamlaka ya kujifanyia lolote bila kuhojiwa au hata kuwajibishwa tu?
4. Katiba iliyopo haitoi haki sawa kwa watu wote ndani ya nchi?
5. Kuna mianya mingi katika katiba hii ambayo inaweza kuifanya mihimili mingine hata kupoteza uhuru wake wa kiutendaji kwa mujibu wa katiba yenyewe?
6. Kuna utitiri wa nafasi za uongozi wasio na tija wala ridhaa ya wananchi ambao pia ni mzigo mkubwa kwa mlipa kodi?
7. Kuna rundo kubwa la vigogo wasio na tija na wasiolipa kodi wanaopata uhalali tokea katika katiba yenyewe?
8. Nk, nk.

Tunataka katiba nyingine kuyarekebisha ya namna hiyo. Yako mengi tu mjomba.

Wewe huoni hivyo?
Hakika ni Katiba mbaya mno kwa taifa!
 
Kupata Katiba mpya haiwezi kuwa lelemama.

Tutapata katiba mpya mapema kwa kuidai kupitia chombo ambacho kitaulenga upatikanaji wake kama agenda pekee.

Vyama vya siasa wana agenda zao. Watu binafsi nao wana agenda zao pia zinazoweza kuwa zaidi ya hii.

Ni vyema vyama siasa, watu binafsi na asasi mbalimbali wakawa wajumbe humo kwenye chombo hiki wao kama vyama, asasi au watu binafsi.

Hii itasaidia kuondoa unyanyapaa Kwa washiriki, kupanua wigo wa ushiriki na ku focus kwenye hoja za msingi pekee za kulenga kumfunga Paka kengele.

Tuunganishe nguvu katiba mpya ni sasa na inawezekana.
Bandiko mujarabu kabisa Thank you brazaj
 
Back
Top Bottom