Kuharakisha Katiba Mpya tuunde 'Coalition of the Willing'

Kuharakisha Katiba Mpya tuunde 'Coalition of the Willing'

Ni wazi kuwa siku zote wanaotaka katiba mpya watakuwa ni wengi kuliko wenye guts za kuidai. Kudai katiba mpya si lelemama. Kuna gharama za kulipa.

Kutegemea kuwa hii itakuja bure bure au kwa wepesi ni kujidanganya.

Badala ya kubakia kulaumiana, kunyapaana, kuitana majina kwenye jitihada hizi, "coalition of the willing" ingeweza kutufaa zaidi. Ikawa wazi kwa kila mwenye kutaka kuwamo.

Katiba mpya haihitaji watu wote. Opportunists wapo kila mahali. Wenye kudharimia haswa pia wapo na tunatosha sana. Isitoshe pia kuwamo humu haisimamishi kuidai vyamani.

Wengine watatukuta tutakapokuwa tumefikia.

Lissu, Mpina, Slaa, Zitto, Lipumba, Chadema, CUF, Zitto, wewe na yule wenye kuona inafaa wakakaribishwa.

Jitihada zozote za kudai katiba mpya haziwezi kuwekewa kizingiti na yeyote aliyedhamiria hasa kwenye mpambano huu.
Umenena vema
 
Nakuunga sana mkono, na hata mguu! Tuwasiliane na kupeana mikakati

Tutafutane mkuu.

Coalition of the willing haiwezi kuwa na nafasi ya unyanyapaa kwa yeyoye.

Screenshot_20230129-162205.jpg


Hii shughuli inahitaji watu.

Mwamvuli kama huu unayo majibu yetu ya njia ya kuipata katiba mpya sasa kama kipaumbele pekee.
 
Back
Top Bottom