Kuharibika Meno

Kuharibika Meno

Gefu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2010
Posts
6,930
Reaction score
2,565
...tatizo ni nini... ?? napiga mswaki minimu twice aday ! kinywa kisafi lkn baado naona dalili za meno kuoza..! is there any other option ? kung'oa mmmmh..kibogoyo..!? help,help,help
 
...tatizo ni nini... ?? napiga mswaki minimu twice aday ! kinywa kisafi lkn baado naona dalili za meno kuoza..! is there any other option ? kung'oa mmmmh..kibogoyo..!? help,help,help
Je unatumia sukari sana?mfano sukari ya kawaida kwenye vyakula,vinywaji au soda?
 
Je unatumia sukari sana?mfano sukari ya kawaida kwenye vyakula,vinywaji au soda?

in addition; chocolates and biscuit tm sn pia sio mzr

...ni mnywaji mzuri wa soda na chai,ila chocolate na biscuits situmii na hata nikila sitafuni namung'unya tu,vyakula vya sukari si mlaji sana...
 
suala la kuharibika kwa meno ni kubwa sana kwa sasa hii haijarishi kinywa chako ni kisafi vipi, meno huharibika kutokana na acid inayozalishwa na bacteria wanaotumia sukari kama chakula chao, wakati wanatumia sukari hiyo, fermentation hutokeo na kusabisha acid kuongezeka kinywani ambayo kitalaamu tunasema inashusha noma pH Ambayo ni around 7. PH ikishuka meno huanza kupoteza minerals ili kubalance ile pH NA kumbuka meno yameundwa kwa inorganic minerals, hii process huenda polepole mpka unaanza kuhisi tobo kwenye jino. kwa ufupi basi tunashauri kwamba mtu apige mswaki mara mbili kwa siku yaani asubuhi na jioni kabla ya kulala kwa kutumia dawa ya mswaki yenye madini ya fluoride na kwa tanzania inaonesha kuwa colgate ndio yenye fluoride ya kutosha, madini ya fluoride ndio kila kitu katika kuzuia meno kutoboka na sio usafi tu wa mdomo kwan research nying zimeonesha kuwa mtu anaweza kuwa anatumia vyakula vya sukari lakin bado asipate matizo ya meno kama atafuata utumiaji sahihi wa dawa yenye fluoride ya kutosha na zingatia kuwa ukisha piga mswaki na dawa usisukutue na maji kwa nguvu acha ile pofu lifanye kazi, sukutua kidogo tu ili dawa iendelee kufanya kazi
 
...mkuuu 198 nashukuru kwa shule yako nzuri, je hakuna kitu kingine zaidi ya colgate ninachoweza kupata hii fluoride..?
 
Last edited by a moderator:
Je unajua sukari kiasi gani imo kwenye chupa moja tu ya soda(0,5liter)?
Hio biskuti haimati kama unatafuta au unamungunya coz mabaki ya biskuti yatakuwepo kwenye mdomo na meno!
Chupa moja ya coke ina 53 grams za sukari.
1.Kunywa maji baadala ya kunywa soda na badilisha biskuti na matunda kama unajihisi una ham ya sukari
(maembe,mananasi,ndizi n.k)
2.Epuka kula kirejareja yaani uwe mfano na milo minne kwa siku.Sio kila unapojisikia kula unakula tu.
3.Tumia uzi wa kusafishia meno(pamoja na dawa ya meno)kuondoa mabaki ya chakula/sukari katikati ya meno sehemu zote zenye upenyo
4.Tumia dawa ya mswaki yenye FLOURIDE na anza kula FLOURIDETABLETS kama zinapatikana.
5.Nenda kwa daktari wa meno akakusafishe hayo meno.
 
ni tatizo la kutokupiga mswaki vizuri tumia listerine kuua vijidudu
..napiga almost twice a day, ila ngoja niitafute hiyo listerine labda itanisaidia..
 
... mimi49 nashukuru,nafanyia kazi ushauri wako...
 
Last edited by a moderator:
fluoride inaweza kupatikana katika vitu vingi lakini cha msingi ni kwamba fluolide ambayo inatakiwa ni ile ambyo ipo katka ionic form na ambayo mtu anaweza kutumia kwa njia ya kupiga mswaki au kwa nchi za wenzetu serikali imeona umuhimu wake wameiweka kwenye system ya maji ya nyumbani au kwenye chumvi tunaita water fluoridation au fluoridated salt. lkn kwa bongo hatujaweza kufika hapo.ushauri kama utapata dawa ya mswaki nyingine zaidi ya colgate itakua vzr lkn kimsing bongo dawa zingine wameamdika fuoride ipo ukweli haimo, kwan kuna stdz zmeonesha ukweli huo.
 
Back
Top Bottom