Nikwambie Best. Usipoteze muda wako fanya mambo ya maendeleo. Ila kama una hamu zaid ya kujua ni kazi nzuri sana ya kizalendo na inayoheshimika kila nchi kama idara ya ujasusi na ya siri sehemu nyingi na hufanya kazi kwa maslahi ya wananchi na kulinda viongozi wake na kwa hapa Tanzania inawajibika kuwalinda Top Five, yaani Rais wa JMT. Rais wa Zanzibar, Makamu wa Rais , Waziri Kiongozi wa Zanzibar na Waziri Mkuu. Na pia wanahusika na kufanya mauji ya mtu au kiongozi yoyote anayeonekana kuwa tishio la serikali hasa iliyoko madarakani kwa mfano kama alivyofanyiwa aliyekua mkurugenzi wa idara hiyo Kombe na pia Kolimba Prof. Mwaikusa na wengine kibao.
Kwa kifupi wamegawanyika katika maeneo na idara mbalimbali kama vile kwenye taasisi za dini, mashuleni, vyuoni,sekta binafsi, makazini nk. na wengine kuchunguza uozo wa viongozi kuanzia kijiji, kata mpaka Taifa.
Tukija kwa sasa hapa kwetu kwa nyakati hizi hiyo siyo idara ya kujivunia tena imejaa dhuluma na vitisho, majungu, kujuana na wengi walioko huko ni watoto wa wakubwa fulani aidha jeshini, polisi, au kwenye idara yenyewe hiyo na hapo ndipo panapopoteza utamu na ladha halisi ya TISS.
Sikumbuki au kuwahi kuona kazi hii inaombwa mahali popote zaidi ya wao kuangalia uwezo wako binafsi na uzalendo wa nchi yako watakufuata wenyewe na kukupa baadhi ya kazi za majaribio na kukupa maelekezo machache na namna ya kutunza siri
NB: Nimetumika na idara hii kwa takribani miaka saba kama UC. Kwenye maeneo mbalimbali kama makazini mitaani, sehemu za ibada tena bila malipo ya maana zaid ya kupewa eti posho ambayo unaweza kupewa mkononi tu bila kusaini popote na na usihoji maana utawadhi wakubwa wako na jina lako likawa la chaki miaka yote bila kupata usajili unaoeleweka na utaishia kuonewa huruma na wenzako watasema mbona fulani amepata usajili na hana lolote na huyu mchapa kazi ameachwa kifupi nina maumivu yasiyo na idadi ya vitu nisivyopenda.
Kwa mfano Tanzania hakuna kazi nyingi lakini ili uonekane unafanya kazi inabidi upeleke taarifa (repot) hata kama ni ya uongo ambayo inaandikwa kufuata mtiririko wa (W5) Yaani.
When
Where
What
Who
Why
Kitu ambapo kama ukizingatia na kufuatilia vizuri mfumo huu hauwezi kuandika report ya majungu kitu ambacho hawakipendi wanataka uandike taarifa ya majungu na kumchafua mtu hasa yule ambaye kamati ya ulinzi na usalama inataka kumtoa kafara kama vile kumhamisha mtu fulani kutoka sehemu moja kwenda nyingine mfano ma RPC,RCO,RC.DC,DED,OCD na wengine kibao kama taarifa yako itakua safi sana imefuata taratibu zote utasifiwa na kupongezwa na wenye uzalendo wachache na lakini yatakupata ya yaliyompata Sitta.
Kwa kifupi niko kwenye hii idara nateseka na majungu, urasimu,dharau,bifu zisizo na maana yaani natamani kama utawala ubadilike labda itatuona wanyonge wa chini tutakalitumikia Taifa hili kwa uadilifu na haki sawa kwa kila.
Thnx. JF. Hatutambuani kwa majina halisi ingekuwa kazi kweli yangenikuta yaliyomkuta Kombe.