'Pseudocyesis' ni muonekano wa dalili zote za ujauzito anazopata mwanamke wakati kiuhalisia hana ujauzito. Mwanamke anaweza kuwa na dalili zote za ujauzito kama kutapika mara kwa mara, shida ya kulala na hata kukosa hedhi lakini vipimo vikaonesha kutokuwepo kwa ujauzito.
Hali hii husababishwa na Tamaa kali ya kuwa mjamzito, kuharibika kwa mimba nyingi, kupoteza mtoto, ugumba, hofu kubwa ya kupata mimba, unyogovu au wasiwasi, jeraha la kihisia, unyanyasaji wa kijinsia na mvurugiko wa vichocheo mwilini (Hormonal imbalance).