Kuhisi nganzi, maeneo ya tumboni

kALEnga kidamali

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2015
Posts
542
Reaction score
735
Habari enyi wana jf

Kuna rafiki yangu ambaye ni kijana (ME) mwenye umri wa above 25 age, huwa ikitokea kapatwa na homa mara nyingi pia lazima maeneo ya tumbo huwa anahis kama kuna uzito flani hivi kwa ndani kama ganzi hivi ambayo huendelea kwa mda kidogo hata baada ya kupona homa lakin baadae hiyo hali hupotea.

Ila kwa kipindi hiki hiyo hali ya kuendelea kupata hali ya ngazi maeneo ya tumboni kwa ndani imekuwa ikiendelea kwa mda kidogo

Mbali na hilo tatizo kuna tatizo jingine limejitokeza katikati ya miguu upande wa mguu wa kulia kuna kauvimbe mithili ya kipele hivi ambako hakana maumivu ingawa huwa anahis kama mguu unapata ganzi fulani hivi. Ni mda wa wiki mbili sasa hili tatizo lipo.

Naombeni ushauri wenu enyi wadau na wajuvi wa masuala ya afya mumsaidie huyu.

Ahsanteni
 
"Ukipatwa na homa" unamaanisha nini?
Wa tz mna shida sana yaani mkibadilisha mazingira kidogo tu mna anza mikogo na ku pretend hamjui baadhi ya vitu, hivi kuna mtanzania yeyote asiyeijua homa, tuache kuigiza bana...... Hapo una cheti cha unesi na ukiwa daktari itakuwaje... Hao madaktari wenyewe wanaelewa mgonjwa akisema hivo... Eti wewe hujui mmmmmhhh..
 
Mrejesho, nimepona kabisa na niko vizuri na ngangari kiafya. Ila kwa mtaalamu yeyote anaejua anaweza kuelezea tu hilo tatizo kwa faida ya wengine.
 
Msaada umetumia dawa gani? Msaada basi nami nasumbuliwa na suala la ganzi tafadhar
 
Duuuh... mgonjwa hii ilikua ni kwa faida yako mbona, ila sio kesi kikubwa umepona basi MTUKUZE MUNGU wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…