Dr Matola PhD
JF-Expert Member
- Oct 18, 2010
- 60,050
- 104,466
Pete mbona zimejaa kwa masonara, kama huo ndio msimamo wako jifikirie mara mbili, ni afadhali mtu asiepropose ndoa kuliko msanii anaekuingilia kwa gia ya kukuoa.Ni kama vile wanatufanyia Interview! hapo hujanipata. Hayo nitafanya ukinivisha pete wangu. kama inakushindaa
kwaheri
Nimeshindwa mtihani bana kanitolea nje eti sina vigezo alivyovitaka
sio kwamba wamama wana matatizo sema la life cycle inachangia mama kushindwa kumudu majukumu ya nyumbani mfano mama unatakiwa kazini saa moja na nusu na upo dar inamaana unatakiwa uondoke home saa kumi na moja na kurudi umewai sana saa 2 sasa hapo majukumu yanaenda kwa housgirl ndo maana mimi sidhani kama mwanaume ananioa ili nimfanyie kazi za nyumbani na siwezi kuishi na mwanaume eti nimsaidie kazi za home atafute mtumishi.mimi nikiishi nae ni mambo mengine maana automatically kama lengo lake ni kumfanyia kazi za nyumbani,naeza kushindwa kuzifanya sio kwamba sipendi ila ni kutokana na situation tu ya maisha
Halafu kama wewe kwa kuangallia tu picha yako tayari nimesha-kudisqualify hata nafasi ya interview ya kuwa hose wife sikupi... Labda Ceremonial wife pia kwenye 6*6 nakupa 100% .... Jikoni najua 0%, Jeans najua hufui 0% .....kunyoosha najua ni dobi ... mh! labda niwe fisadi ....
Pete mbona zimejaa kwa masonara, kama huo ndio msimamo wako jifikirie mara mbili, ni afadhali mtu asiepropose ndoa kuliko msanii anaekuingilia kwa gia ya kukuoa.
Utavimba bichwa kwa kuvalishwa pete kumbe kuna wenzako 6 nao wameshavalishwa pete, jamaa atajilia mzigo kwa ulaini akitosheka anakuachia manyoya. wake up usiwe mjinga.
Yaani mkuu unakwenda na mstari na hata sina haja ya kukuuliza umri maana najuwa wewe ni wamakamo yangu, sio wa level ya usharobaro, maana kuna wakati demu anaweza akakugeuza wewe ndio dingi mapenzi kidogo mizinga mingi.Nilidhani tunazungumzia mahusiano ya kabla ya ndoa....ambayo kimsingi yanakuwa na imbalances (mpini/makali) za kila namna. Pale mwanzo ndio maana nikasema kuna 'nipe, nikupe' (compromises) nyingi tu katika kujaribu kutengeneza mahusiano ambayo baadae yanaweza kwenda kwenye hatua ya ndoa.
Binafsi kabla sijaoa, nimepita kwenye similar situation lakini ilikuwa ni kwa ridhaa ya binti mwenyewe bila kumshurutisha na hata mimi kuna mambo nilikuwa namfanyia bila kushurutishwa ambayo hayakuwa majukumu yangu from a strict point of view.
<br /><span style="font-family: comic sans ms">Ndio maana ndoa nyingi zitaendelea kuvunjika... Haya ni majukumu ya msingi kwa mwanamke yeyote na hata kama wote tumeajiriwa Houseboy/girl anasuppliment tu na iko siku nitataka wewe unipikie na pia sio busara hao wengine wakanifulia nguo zangu katika mazingira ya kawaida. Hapa ndipo maendeleo na uzungu unapotumislead!! I stand to be criticised!</span>
Mi napita tu hapa wajameni, ila kama kuna mdada atataka kuhamia kwangu akaribie tu niko free, aje tutambuane
Ni tatizo sana nowdayz, hasa kwenye issue ya zaa kwanza ndo tuoane?! sasa huwezi pata mtt ww si mke? ndoa nyingi wanawake vitumbo mbele, kama hawajishikishi ili waolewe basi ni condition aliyopewa na mkaka, kufua poa tu as huwezi kwenda kwa mshikaji mkalalia mashuka machafu, or mkapitia chipsi unapika kidogo. Ila kuhamia kwa mkaka bila ndoa wont advice.
Yaani mkuu unakwenda na mstari na hata sina haja ya kukuuliza umri maana najuwa wewe ni wamakamo yangu, sio wa level ya usharobaro, maana kuna wakati demu anaweza akakugeuza wewe ndio dingi mapenzi kidogo mizinga mingi.
Mi napita tu hapa wajameni, ila kama kuna mdada atataka kuhamia kwangu akaribie tu niko free, aje tutambuane
Habari zenu. Nimekumbwa na utata juu ya suala hili, siku hizi wakaka wengi kabla ya ndoa wanataka wahudumiwe kama kwamba tayari wameoa. Tendo la ndoa, Kufua, Kupika, Usafi wiki end na hata katikati ya wiki na mambo mengine kama hayo. Je hiyo ni sawa kwa mila na desturi zetu?
wengine wanafika mbali zaidi wanataka mtoto kwanza ndipo ndoa ije.
Sasa kweli huo ndio upendo? Naomba Mnieleweshe labda mie wa kizamani mno.
Sina tatizo na kukufulia na kukupikia 365 days a year, tatizo linakuja kuwa sote tumekuwa waajiriwa, katika maisha ya leo. Kwa hiyo wote tunaingia nyumbani kuanzia saa moja na nusu jioni (tulio na bahati mbaya ya kukaa maeneo ya pembezoni mwa mji). Naamini kwa muda huu kuingia jikoni na kuanza kujipikilisha, na uchovu wa kazini (ambao nina hakika na wewe mwenzangu unao) tutalazimika kumuajiri msaidizi. Kwa hiyo sidhani kama ni uzungu ndugu yangu, bali ni suala la sisi wenyewe kuwa considerate kwa wenza wetu. Kama niko tu nyumbani, naamini hayo hayawezi kushindikana.
Imagine tumeingia wote nyumbani, unadai chai, maji ya kuoga, chakula to name a few....jamani hata kumfikiria mwenzio kuwa naye alikuwa kazini, au kazi zako tu ndio zinachosha?
Tukirudi kwa wakaka wanaotaka huduma hizi kabla hata ya kuoa, nafikiri mara nyingi akina dada nao wanafanya hivyo kwa kujiona wako insecured na mostly on the loosing side. Kama alivyosema mdau mmoja, wewe ukigoma anakuja mwingine fasta na kufanya huduma zote hizo si ajabu na hela ya matumizi akaacha (haa haa..) Lakini the bottom line ni kuwa unaweza kuvunja mgongo kufua, kupika, usafi mpaka ukalima na bustani ya mboga nje, lakini mwisho wa siku inawezekana kabisa kuna mwingine pembeni ambaye hasumbuliwi kwa namna yoyote ile na anatengeneza kucha mwanzo mpaka mwisho wa wiki (hazigusi maji zaidi ya anayoogea), ambaye ndiyo akaolewa kwa shangwe zote! Na wewe 'employee of the year' ukabaki unasoma namba...tafakari na chukua hatua.
Mimi napinga kabisa mwanaume anayetoa masharti kama ya kupikiwa na kufuliwa ndio akuoe. Ila nakubali kabisa wife material lazima atafanya hivyo vitu bila kushurutishwa. Kwa hiyo kwa mtazamo wangu mwanaume anayetoa masharti sijuhi upike, ufue, upate mimba ndio nakuoa si husband material. Na mwanamke anasiyefanya hizo kazi pale anapomtembelea mpenzi wake gheto si wife material.
Unajua hata kama sisi wanawake wa kileo tuko busy na kazi na mafoleni bado kuna tofauti kati ya nyumba ya mwanamke asiyejua kazi za ndani na mwanamke anayezijua ila hana nafasi. Kumbuka kuwa mahousegirl wengi si profesional kwa kazi za ndani wanahitaji kufundishwa maana wametoka bush kwa mfano most of them hawajawahi hata kutumia vyoo vya ndani wala kuvisafisha. Sasa kama mama mwenye nyumba hajuhi kupika jua fika hata housegilr hataweza pika chakula kizuri; nani atamfundisha??? Kama mama hajuhi kufua wala usafi wa ndani jua nyumba itakuwa chafu hata kama mna housegirl watatu kwani mkeo hatakuwa anaona kasoro.
Hata makazini supervisor mzuri ni anayejua kazi. Kwa hiyo hata kama hatufanyi kazi za ndani very often we are good supervisors because we know them. Mimi housegirl hakiacha kazi naona mme wangu anavyokuwa na furaha maana ananotice difference ndani katika kila nyanja. Bahati mbaya siwezi hacha kazi.
Nina shemeji yangu alikuwa na girlfriend wake wa muda mrefu saana mdada anakuja gheto kwa shem anampikia afu anaacha vyombo kibao kwenye sink anatimua mpaka nyumba inatoa harufu. Mwisho wa siku jamaa hakuoa japo am sorry kwani alikuja mzalisha dada wa watu. Ila washikaji wote walikuwa wanamwambia jamaa ukioa hapo umevaa mkenge.