Sina tatizo na kukufulia na kukupikia 365 days a year, tatizo linakuja kuwa sote tumekuwa waajiriwa, katika maisha ya leo. Kwa hiyo wote tunaingia nyumbani kuanzia saa moja na nusu jioni (tulio na bahati mbaya ya kukaa maeneo ya pembezoni mwa mji). Naamini kwa muda huu kuingia jikoni na kuanza kujipikilisha, na uchovu wa kazini (ambao nina hakika na wewe mwenzangu unao) tutalazimika kumuajiri msaidizi. Kwa hiyo sidhani kama ni uzungu ndugu yangu, bali ni suala la sisi wenyewe kuwa considerate kwa wenza wetu. Kama niko tu nyumbani, naamini hayo hayawezi kushindikana.
Imagine tumeingia wote nyumbani, unadai chai, maji ya kuoga, chakula to name a few....jamani hata kumfikiria mwenzio kuwa naye alikuwa kazini, au kazi zako tu ndio zinachosha?
Tukirudi kwa wakaka wanaotaka huduma hizi kabla hata ya kuoa, nafikiri mara nyingi akina dada nao wanafanya hivyo kwa kujiona wako insecured na mostly on the loosing side. Kama alivyosema mdau mmoja, wewe ukigoma anakuja mwingine fasta na kufanya huduma zote hizo si ajabu na hela ya matumizi akaacha (haa haa..) Lakini the bottom line ni kuwa unaweza kuvunja mgongo kufua, kupika, usafi mpaka ukalima na bustani ya mboga nje, lakini mwisho wa siku inawezekana kabisa kuna mwingine pembeni ambaye hasumbuliwi kwa namna yoyote ile na anatengeneza kucha mwanzo mpaka mwisho wa wiki (hazigusi maji zaidi ya anayoogea), ambaye ndiyo akaolewa kwa shangwe zote! Na wewe 'employee of the year' ukabaki unasoma namba...tafakari na chukua hatua.