Kuhudumia Mwanaume Kabla ya Kuoana.

Kuhudumia Mwanaume Kabla ya Kuoana.

banga

Member
Joined
Jul 14, 2011
Posts
9
Reaction score
9
Habari zenu. Nimekumbwa na utata juu ya suala hili, siku hizi wakaka wengi kabla ya ndoa wanataka wahudumiwe kama kwamba tayari wameoa. Tendo la ndoa, Kufua, Kupika, Usafi wiki end na hata katikati ya wiki na mambo mengine kama hayo. Je hiyo ni sawa kwa mila na desturi zetu?
wengine wanafika mbali zaidi wanataka mtoto kwanza ndipo ndoa ije.
Sasa kweli huo ndio upendo? Naomba Mnieleweshe labda mie wa kizamani mno.
 
Mimi naona mara nyingi inakuwa 'nipe, nikupe'! Wakaka nao watalalama kwa kupigwa mizinga.
 
hapo kwenye mtoto hapo mmmh!
Ila kufua na kupika hufanywa in the name of love!
 
Habari zenu. Nimekumbwa na utata juu ya suala hili, siku hizi wakaka wengi kabla ya ndoa wanataka wahudumiwe kama kwamba tayari wameoa. Tendo la ndoa, Kufua, Kupika, Usafi wiki end na hata katikati ya wiki na mambo mengine kama hayo. Je hiyo ni sawa kwa mila na desturi zetu?
wengine wanafika mbali zaidi wanataka mtoto kwanza ndipo ndoa ije.
Sasa kweli huo ndio upendo? Naomba Mnieleweshe labda mie wa kizamani mno.

Mi nadhani wanapenda wenyewe kuhamia. Hawalazimishwi.
Watoto wa kike maadili kwishneiiiii.
 
Sasa ntjuaje kuwa unaweza kukpika, kufua nk?
 
na ndo maana siku hzi hawaoi kama anapata huduma zote za ndoa ataoa akitafuta nini?wadada wote tungewakaushia hawa mabrazameni wangekuwa na adabu.ukikataa wewe mwenzio anahamia fasta kazi kweli kweli

Chukua hatua, Hamia Airtel.
 
hapo kwenye mtoto hapo mmmh!
Ila kufua na kupika hufanywa in the name of love!

Mtoto muhimu sana, wengi wao siku hizi kuzaa taabu kwa sababu ya kuchopoa mimba. Ni muhimu kujaribu uzima, Dunia imekwisha hii ndugu yangu.
 
<br />
<br />

na huvutia zaidi mwanaume ikiwa huzai/matatizo ya sperm cjui Mwanamke akikumwaga bse huwezi kumimbisha inakuaje
 
Habari zenu. Nimekumbwa na utata juu ya suala hili, siku hizi wakaka wengi kabla ya ndoa wanataka wahudumiwe kama kwamba tayari wameoa. Tendo la ndoa, Kufua, Kupika, Usafi wiki end na hata katikati ya wiki na mambo mengine kama hayo. Je hiyo ni sawa kwa mila na desturi zetu?
wengine wanafika mbali zaidi wanataka mtoto kwanza ndipo ndoa ije.
Sasa kweli huo ndio upendo? Naomba Mnieleweshe labda mie wa kizamani mno.

Labda tungewauliza na upande wa pili nao kwa nini wanapenda kuhudumiwa kama wanawake walioolewa wakati bado? Kuishi nyumba moja na mwanaume, kupewa pocket money, kumfuatilia jamaa kujua yuko wapi, anafanya nini wakati gani na nani, amerudi saa ngapi nyumbani, kwenda outing etc. Kwa ufupi ni biashara ya nipe ni kupe tu ndiyo inayoendelea maadili kwishney.
 
kuna kitu mnatoa hata?unakuta mdada ana kazi yake ila anaishi tu na mwanaume bila ndoa matumizi anaafford naona ni maadili tu kushnei
 
kwani unaoa mtu wa kupika na kufua? kuna mashine siku hz

Hayo ni marupurupu ya kuoa bebii na kwa taarifa yako japo wengine hawasemi kwa uwazi wengi tunapenda kuoa mke anayejua kupika, kufua, kupiga pasi, kumpangia mume maji ya kuoga na kuihudumia familia japo tunajua wengi wakishaolewa hawayafanyi hayo tena. Hasa house girl akishaingia ndani ya nyumba. Mke anayejua hayo siyo tu anaweza kumsimamia vyema housegirl bali anampa mume comfort ya kujua kuwa hata kama housegirl hayupo maisha yataendelea kama kawaida au kwa ubora zaidi. Kuna kina mama house gilr akiondoka wanapata stress na kuanzisha ugomvi usiokuwa na mpango na mume ili kuficha ukweli kuwa wana mapungufu kunako ile idara ya jikoni na mambo ya nyumbani.
 
Jamani si tumetoka kumjibu jamaa aliyeoa akakuta mkewe ana tattoo ya aliyembikiri, tukasema alikosea kuoa bila kuonja. Sasa huyu hapa anaona si sahii kuonja kabla tunakwenda wapi sasa?! Tunatakiwa kuonja tena vyote, mapishi, kufua, kutunza nyumba, kuzaa nk. hivi ndio vyenye uhakika, kudumu kwa ndoa si uhakika sana siku hizi.
 
tafuta housegirl au houseboy?

Ndio maana ndoa nyingi zitaendelea kuvunjika... Haya ni majukumu ya msingi kwa mwanamke yeyote na hata kama wote tumeajiriwa Houseboy/girl anasuppliment tu na iko siku nitataka wewe unipikie na pia sio busara hao wengine wakanifulia nguo zangu katika mazingira ya kawaida. Hapa ndipo maendeleo na uzungu unapotumislead!! I stand to be criticised!
 
Back
Top Bottom