jestina; wanawake tusikubali na hii mifumo dume mpaka kny relationship.......
nguo zake afue mwenyewe,kupika tutapika wote alternative days........kuweni real jamani mapenzi gani hayo yanayomfanya mwanamke awe mtumwa wa kumpikia na kumfulia mwanaume under wajibu disguise........???eti utasikia mapenzi mapenzi gani hayo ya upande mmoja??kwa nini isiwe kufuliana..kupikiana bali iwe kumpikia mume,kumfulia mume etc?
Jestina mambo ya kupika, kufuliwa nguo mwanaume haulazimishwi dada, ni wewe tu kujiamulia na kumwambia huyo mchumba wako/mumeo/Bf kuwa mpeane zamu za kupika, kufua nguo, kupiga deki nk. Akikubali basi, ni jambo jema endelea na furahia mahusiano yako. Akikataa endelea kutafuta huyo anayekubali hayo masharti kwa maana haitakuwa shida huko mbeleni maana utakuwa umempa taarifa mapema. Nadhani ni culture na nature. Sijaona kwenye bible ambapo mwanaume kazi yake mojawapo ni kupika, kufua nk zaidi ya kuhudumia familia na kuhakikisha inapata mahitaji. Tukija kwenye culture yetu sisi waafrica kupika ni kazi ya mwanamke japo mara moja moja mwanaume ukijisikia kuingia jikoni siyo mbaya lakini siyo wajibu.
Ukisema uchukue mfumo wa wenzetu wanaosema wameendelea (Western countries) basi inawezaku kula kwako kutokana na hilo gamba wanaume waa kiafrika waililolivaa la kutenganisha kazi za mwanaume ni zipi na za mwanamke ni zipi. Hata huko pia (in western countries) wanawake wa kutoka africa bado wanapika pia japo mfumo wa fastfood umetawala. Labda kufua ndo wanatumia hizo mashine.
Hapo kwenye Nyekundu sijakupata point yako ni ipi ya mwanaume wa kiafrica kuwa real maana najuwa walivyo ndivyo uanaume wa kiafrica. Asipotimiza wajibu wake wa kuhudumia familia na kui-protect inabidi umkalishe chini umuulize kwa nini hatimiza wajibu wake kama yeye anavyotoka huko kazini na kukuliza chakula kiko wapi japo mara nyingi kitatengwa bila hata kuuliziwa.