Kuhusu Arsenal, wenye kumbukumbu mnakumbuka

Kuhusu Arsenal, wenye kumbukumbu mnakumbuka

FATHER OF REALITY

Senior Member
Joined
Nov 3, 2014
Posts
123
Reaction score
100
Mwanzoni mwa msimu mwa msimu wa ligi wa 2016/2017 tuliona ujio wa makocha Antonio Conte na Pep Gurdiola katika ligi ya England wakiongeza chachu ya makocha wenye washindani kama vile Jose Mourinho, Jugern Klop, Portchetino na Arserne Wenger.

hapa hapa jamii forums nilianzisha mabishano ya kisoka ili kusaidiana uchambuzi wa mchezo huu pendwa kwa wadau kama sisi, ubishani wangu nilianzisha kwa kusema, "UJIO WA MAKOCHA WASHINDANI EPL WENGER HATARINI KUTOINGIA TOP FOUR" basi wenye kumbukumbu, mnakumbuka nilivyoshambuliwa na wapenda soka wengi huku wengi wao wakiwa mashabiki wa timu yao pendwa ya Arsenal.

Uchambuzi wangu ulikuwa kweli wa kisoka pasipo upendeleo, maana sikudai eti Arsenal isingeingia top four, hapana ila nilitahadharisha kwamba huenda wakaisikia mbombani, si kama walivyozoea, maana tangu mwaka 1996 timu hii haikuwahi toka katika top four hadi ilipotolewa msimu wa 2016/2017 ambapo dalili zipo pia by 90% kutoingia top four 2107/2018. Huu haukuwa uchawi au utabiri wa mang'amung'amu kw mfuatiliaji na mchambuzi mzuri wa soka la ulaya au EPL, kwa upekee.

Hoja zangu zilikuwa hivi.
1. UJIO WA MAKOCHA SHINDANI WENYE HADI YA TIMU KUBWA.
Muda wote ambao Arsenal chini ya Wenger amesimama ndani ya nne bora, makocha washindani wa kiwango chake walikuwa wachache, yaani hawakuzidi watatu juu yake. Uwepo wa makocha hawa na kufikia wanne, automatically katika muda niliofuatilia soka la ulaya na EPL kw upekee, mimi, sikuona nafasi ya Wenger top four.

2. KUKOSA KIKOSI SHINDANI
Baada ya mwaka 2007 kuja juu, kikosi cha Arsenal kimekosa dira kabisa katika medani ya ushindani yakinifu wenye tija. Kumbuka ushindani unaoonyeshwa na timu kama Juve UEFA, samahani sizungumzii kuchukua ubingwa tuu, hapana yaani kutia chachu ya kikubwa, yaani ile sifa ya timu kubwa.

3. KUFILISKA KWA MBINU ZA KOCHA.
Nilianza kuifuatilia ligi ya Uingereza kwa kina mwaka 1997, ubora wa Arsenal ulikuwa wa kutisha na hata viwango vya wachezaji wake vilikuwa vya juu, huku master Wenger, Prof, akitamba na kipaji hatari cha kujua mchezaji gani acheze wapi na amtumieje, mfano, Emanuel Petit mda wote wa soka alijijua kama namba 3 kwa sababu ya kutumia mguu wa kushoto, lakini wenger anambadilisha na kumweka no. 6, ahaa, anakuwa bora kabisa, pia Henry toka 11 hadi 9, akimfanya Anelka kuwa hatari zaidi n.k.

Kocha huyu amefilisika mbinu hasa baada ya kusumbua EPL, makocha wakamtafutia dawa na yeye hakubadilika. hili nililiona mwaka 2005 na kulisema sehemu fulani, nikaishia kutukanwa, Wenger angekuwa na mbinu mbadala, alikuwa ktk peak 2001 hadi 2007, hapa angetorka na ubingwa mmoja mkubwa au hata kuingia fainali kadahaa kama si kuchukua, alikuwa na kikosi bora.

4. MANENO YA SIR ALEX FERGUSON.
Kumbuka kocha huyu, alidominate ligi ya Uingereza kwa muda mrefu, yaani toka 1992 hadi 2003, akibeba ubingwa mara 9 katika miaka 11. huyu kocha katika mahojiano yake alidai yeye na Wenger wamekuwa wakipokezana kombe kwa sababu ya ushindani mdogo toka ndani, na kipimo chake kilikuwa ugumu ambao wao hukutana nao nje ya uingereza katika mashindano mbalimbali ya ulaya ikiwemo UEFA Champion League. NIKAJIFUNZA JAMBO.

5. UBOVU WA MAKOCHA WAZAWA NA WALE WALIOJIFUNZIA KUFUNDISHA SOKA ENGLAND.
Hoja hii siku za nyuma sana niliwahi kuipa mashiko pale nilipokuwa nikichambua ubora wa soka na league ya Uingereza nikifananisha na Uhispania. nilidai makocha wa uingereza yaani wazawa na hata wale walioanzia kufundisha soka huko, wanadumaza soka ya Englad, nilionya ule utamaduni wa kuamini ati timu fulani mara nyingi ahiifungi timu fulani, au kukazania soka la kibishi na nguvu nguvu zisizo na tija kuliko soka la kifundi, hili lilimpa nafasi wenger miaka yote kubaki top four na Wenger kounekana bora.

6. TAKWIMU ZA LIGI YA PREMIER
Takwimu ilionyesha toka mwaka 1992 hadi 204 kombe la ligi lilichukuliw ana Man U mara, Arsenal mara , na blackburn mara 1, alikuja kuvuruga Morinho kocha asiye na utamaduni wa soka ya Uingereza, na kila alipokuja kocha mwingine basi Wenger hukaa nyuma ya hao nguli.

Kumbuka 2004/2005 bingwa chelsea na Arsenal ya 2 na ya 3 Man U. tokea hapo kukawa na Ferguson, Benitez, Mourinho, baadaye, Acnceloti, Mancini, Pelegrin, Raniel na sasa Guardiola, Mou, Klopp, Conte, Potchetino sasa wao tu watano alafu Wenger atakaa wapi.

Msimu wa 2015 na 2016 tumeshuhudia Arsenal inarudi katika nafasi ya pili (2) iliyoipata mara ya mwisho mwaka 2005. hii ilitokana na kudorola kwa timu vinara na kutokea mshindani mmoja akamzidi Wenger na kuchukua ubingwa, huyu si mwingine bali ni mzee Claudio Raniel aliyeipa ubingwa Leicester City kisha kupotea kama si kupotezwa.

7. SERA ZA WENGER NA KUTOSOMA ALAMA ZA NYAKATI.
Sera za babu huyu zimekuwa mapato na matumizi bora ya klabu huku akisifiwa kwa uchumi mzuri, ni kweli hilo ni bora, lakini kama ni hivyo kwa nini timu isivunjwe na kuanzishwa supermarket kubwa iitwayo Arsernal, mbona ingekuwa poa, kuliko kijiita klabu ya soka afu kila siku mafanikio ni kwamba klabu haina madeni na ina hela, tazama madrid wana madeni ila ni klabu iwezayo mnunua yeyote inayomhitaji duniani na ina mafanikio.

Pia hili limemfanya Wanger kujikita kwa wachezaji wa bei rahisi afu wakishindane na kina messi au ronaldo au vidal au gustavo n.k, babu amesahau hata mafanikio yake yalikuwa chini ya manguli wa soka kiviwango, hata kama wengine akiwakuza, alikuza wachezaji wenye vipaji kamili. maoni yangu babu huyu kafilisika mbinu ili watu wasishtuke anajua hata akinunua wachezaji wazuri hawezi fanya nao kitu cha maana.

Hili la nyakati,
Fergie aliliona, ha! akastaafu ghafla.
Mourinho aliliona msimu uliopita hakupigania top four kaingia UEFA njia ya panya kwa kuwa iko wazi.

Pia nawakumbusha wale waliokuwa wanamhitaji Pep EPL amekuja. Mmemuona?
JAMANI SOKA NI HOBI YETU SISI HATUPIGI RAMRI HAYA HUJIONYESHA HADHARANI.
 
Fans wa man u utawajua tu
Hapana mkuu, usiwe kama wanasiasa, kila asemaye ukweli usioupenda ni adui, hapana, mkuu mi ni pure Madrid fani nisiye na timu EPL, kwa kiasi fulani naikubali ligi ya EPL, kwa kujitangaza ila ni mdau wa majadiliano ya kwamba EPL si bora kuliko La liga, niliwahi pia kutupia nyuzi za uchambuzi wa kina humu. Mi ni pro soka bora. Man U wana uwanja wa kujitamba ila si kwa timu nguli nje ya EPL.
 
Back
Top Bottom