PostGE2025 Kuhusu Azimio la Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) Kuhusu Tanzania na Mapendekezo Yao

PostGE2025 Kuhusu Azimio la Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) Kuhusu Tanzania na Mapendekezo Yao

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,773
Reaction score
1,174
๐—ง๐—”๐—”๐—ฅ๐—œ๐—™๐—” ๐—ž๐—ช๐—” ๐—ฉ๐—ฌ๐—ข๐— ๐—•๐—ข ๐—ฉ๐—ฌ๐—” ๐—›๐—”๐—•๐—”๐—ฅ๐—œ

๐—ž๐˜‚๐—ต๐˜‚๐˜€๐˜‚ ๐—”๐˜‡๐—ถ๐—บ๐—ถ๐—ผ ๐—น๐—ฎ ๐—•๐˜‚๐—ป๐—ด๐—ฒ ๐—น๐—ฎ ๐—จ๐—บ๐—ผ๐—ท๐—ฎ ๐˜„๐—ฎ ๐—จ๐—น๐—ฎ๐˜†๐—ฎ (๐—˜๐—จ) ๐—ž๐˜‚๐—ต๐˜‚๐˜€๐—ถ๐—ฎ๐—ป๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐—ง๐—ฎ๐—ป๐˜‡๐—ฎ๐—ป๐—ถ๐—ฎ ๐—ป๐—ฎ ๐— ๐—ฎ๐—ฝ๐—ฒ๐—ป๐—ฑ๐—ฒ๐—ธ๐—ฒ๐˜‡๐—ผ ๐˜†๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐˜‡๐˜‚๐—ถ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐—บ๐˜‚๐—ฑ๐—ฎ ๐—ž๐˜‚๐˜€๐—ฎ๐—ถ๐—ป๐—ถ ๐— ๐—ถ๐—ธ๐—ฎ๐˜๐—ฎ๐—ฏ๐—ฎ ๐˜†๐—ฎ ๐—™๐—ฒ๐—ฑ๐—ต๐—ฎ ๐—จ๐—ฏ๐—ถ๐—ฎ ๐—ธ๐˜„๐—ฎ ๐— ๐˜„๐—ฎ๐—ธ๐—ฎ ๐Ÿฎ๐Ÿฌ๐Ÿฎ๐Ÿฑ.
================
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND EAST AFRICAN COOPERATION

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Kuhusu Azimio la Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) Kuhusiana na Tanzania na Mapendekezo ya Kuzuia kwa Muda Kusaini Mikataba ya Fedha Ubia kwa Mwaka 2025

Kama mnavyoona kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari tarehe 26 Novemba 2025, Bunge la Umoja wa Ulaya (EU) limejadili na kupitisha azimio kuhusu kile walichoita โ€œPost-election killings and the deteriorating human rights situation in Tanzania, including the case of imprisoned opposition leader Tundu Lissuโ€ ambalo pamoja na mambo mengine Azimio limetoa wito kwa Kamisheni ya EU kusubiriisha kwa muda utiaji saini wa makubaliano ya Programu ya Ushirikiano baina ya Tanzania na EU kwa Mwaka 2025 (Annual Action Plan โ€“ AAP 2025) yenye thamani ya Euro milioni 156.

Serikali inapenda kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili kama ifuatavyo:

i. Maelezo na ushirikiano wa Azimio la EU
Kama mnavyofahamu, EU ni mmoja wa wadau muhimu wa wabiya wa maendeleo wa muda mrefu wa Tanzania na kwa muda wote wa takribani miaka 50 Tanzania imeendelea kuwa na urafiki mzuri sana na Umoja wa Ulaya na uhusiano huo mzuri umeendelea kushamiri siku hadi siku. Kama mnavyofahamu pia, EU ni Mamlaka huru na inaweza kujiamulia mambo yake kupitia Taasisi mbalimbali ikiwemo Bunge lao kama ambavyo pia Tanzania ni nchi huru inayoweza kushughulikia mambo yake yenyewe kupitia vyombo vyake ikiwemo Bunge letu. Kila upande ni Mamlaka huru (sovereign entity) na hakuna upande wenye Mamlaka ya kuagiza upande mwingine nini cha kufanya.

Hata hivyo, katika spirit ya ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na EU, ni utaratibu wa kawaida kunapokuwapo na mjadala unaohusu upande mwingine ni jambo la busara kusikilizia pia maelezo ya upande wa pili. Hili ni jambo la kawaida hata katika maisha ya mahusiano ya kila siku. Hata hivyo ni muhimu kubainisha kwamba maamuzi kuhusu mambo mbali mbali yanayoendelea hapa nchini na EU sio kiongozi wa upande wa pili kama inavyodhaniwa. EU ipo kama mshirika anayetoa ushauri na kusaidia kifedha kwa mikataba mbali mbali ambayo imekubaliwa baina ya Bunge la nchi husika kwa Tanzania kusikiliza balaa za mwenendo wa majadiliano hayo si suala linaloshughulikiwa na Kamati na Ngazi ya Bunge la Umoja wa Ulaya.

Serikali inalikumbusha Bunge la EU umuhimu wa kutupa nafasi ya kusikilizia kwa kina maelezo ya upande wa pili na kutofanya maamuzi ya haraka yasiyo na mashiko. Ni muhimu pia kuhakikisha maelezo yao na maudhui ni ya kutegemewa kutokana na vyanzo sahihi ambavyo vinazingatia utetezi wenye pande zote mbili wa suala husika Azimio ambalo limetolewa jana.

Tunatumaini wenzetu upande wa Bunge la EU wataona umuhimu wa kufanya hivyo kwa siku zijazo kwa kuzingatia kuwa ni takwa la asili ya haki (natural justice) la upande unaojadiliwa kusikilizwa kabla ya kufanyiwa maamuzi yanayogusa upande huo. Aidha, msingi wa ushirikiano wetu umejengwa katika kuthamini mazungumzo na kusikilizana.

Kwa mantiki hiyo Serikali inakanusha tuhuma zote zilijitokeza wakati wa kuelekezwa kwa Serikali katika majadiliano hayo na pia katika Azimio kwa kuwa hazina chembe yoyote ya ukweli, zimetegemea kwenye simulizi za upande mmoja na hazina uthibitisho wa kuaminika na usiotia mashaka.

ii. Tanzania haifungwi na maamuzi ya Bunge la EU

Kama inavyofahamika, pamoja na ubia na urafiki mzuri tulio nao na EU, bado kila upande ni huru na hauagizwi na upande wowote kwani jambo lolote lile katika mfumo wa kibunge au mfumo wa taasisi zingine za utendaji hutatimiwa kama inayotakiwa. Kila upande una mipaka ya jurisdiction yake. Pamoja na hayo, sisi ni washirika wa kimkakati na kwa muda bado tunatambua na kuthamini common values na common interests.

Na tunapoamua kutekeleza masuala mbali mbali ya kimaendeleo kwa manufaa yetu na urafiki wetu huo, bado tunajadiliana na kutanabahi kuwa jambo muhimu ni kuheshimiana na kukubaliana. Hivyo, hakuna maagizo na maelekezo ya aina yoyote tunayo lazimika kutekeleza katika uhusiano wetu na nchi zote marafiki zetu na wabia wetu wa maendeleo. Hakuna upande unaotoa maagizo kwa upande mwingine kufuata jambo lolote nje ya majadiliano na kukubaliana kwa maslahi ya kila upande.

Ni vizuri pia likaeleweka kwamba, masuala ya kimaushiano kati yetu na Umoja wa Ulaya yanasimamiwa na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya na sio Bunge, hivyo, lolote linaloazimiwa na bunge juu ya utaratibu huo yanapaswa kufanyiwa maamuzi mengine na Kamisheni hiyo ili kama kuna lolote la kufikishwa kwetu kwa ajili ya majadiliano basi yanapaswa kufikishwa kwetu na Kamisheni ya Umoja wa Ulaya kwa kuwa ndiyo chombo rasmi kinachosimamia mahusiano ya kidiplomasia baina ya Tanzania na EU.

Hivyo, Watanzania wapuuze taarifa potofu zinazojaribu kuchukua vipengele vya maazimio ya Bunge la EU kama masharti yanayotuelekezwa kuwa ni kama lazima tuyatekeleze mara moja. Hakuna kitu kama hicho. Ni lazima jambo lolote lifuate mkondo wake kama majadiliano. Kwa msingi huo, Serikali inawahakikishia kuwa kwa Tanzania hakuna dharura ya kufikia. Huu ni utumishi wa kawaida wenye mwelekeo wa kuatamia mazungumzo. Aidha, Serikali imekuwa wazi na inanyenyekea kwa jambo lolote na kufanya kazi kwa weledi zaidi kwa manufaa ya wananchi wake. Hata sisi tunamuomba kadai upande wote kuwa mambo yanaenda kwa utaratibu ambao tayari ajili ya kuyazingatia. Lakini hainaishii ni lazima waweletekee.

iii. Suala la Misaada

Kumekuwepo na taarifa zisizo sahihi kwenye majukwaa mbalimbali ikiwemo mitandao ya kijamii zikitoa maelezo tofauti tofauti kuhusu suala hili wengine wakidai kwamba Umoja wa Ulaya (EU) umefuta kabisa misaada yote kwa Tanzania. Upotoshaji mwingine unaenezwa kuaminisha umma kwamba Serikali itayumba kwa kiwango kikubwa kutokana na kutokutolewa kwa fedha hizo za msaada.

Ni kwa mantiki hiyo Ubalozi unaomba kutoa ufafanuzi na kuweka usahihi wa taarifa kwenye suala hili:
Kwanza, kilichoelezwa na EU Commission wakati wakitoa msimamo wa Kamisheni kwenye Mjadala uliofanyika jana tarehe 26 Novemba 2025 kwenye Bunge la EU ni kuwa wanasubirisha kwa muda utiaji saini kwenye Programu Mpya ya Ushirikiano kati ya Tanzania na EU kwa mwaka 2025 ili kutoa fursa ya mashauriano na Serikali. Suala hapa sio kusitisha misaada yote wala fedha zote za EU. Ni kusubirisha. Wametumia neno "put on hold kueleza uamuzi wao kwenye fedha hizo.

Hivyo, ni wazi kusubirisha jambo na kusitisha jambo ni vitu viwili tofauti. Kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji wa Programu hiyo, baada ya mashauriano ya pande zote kukamilika na kuwasilishwa kwa EU mwezi Septemba mwaka huu, EU Commission ilipaswa kutia saini kuidhinisha Programu hiyo mwezi huu wa Novemba ili mikataba ya Fedha (Joint Financial Agreement) isainiwe baina ya EU na Tanzania mwezi Februari mwakani kuruhusu Programu kuanza.

Tunatumaini tutaendelea kujadiliana na Umoja wa Ulaya ili hatua zilizosalia za utiaji wa saini zikamilike kabla ya Februari mwakani kuruhusu Programu kuanza kama ilivyokuwa imepangwa.
Pili, upotoshaji mwingine unaoendelea ni kuonesha kuwa misaada yote ya EU imesitishwa kwa Tanzania. Hili nalo siyo kweli. Programu zingine za EU zilizokwishasainiwa na zinazoendelea ikiwemo ile ambayo mikataba yake ilisainiwa 2024 kurudi nyuma inaendelea na haijahusishwa na uamuzi huu.

Programu iliyosubirishwa ni ya mwaka huu wa fedha tu. Programu hii ina jumla ya Euro milioni 156 kama ilivyoelezwa hata na Kamati ya AFET na DEVE wakati Kamati hizo zinapigia kura suala hilo. Baada ya Serikali kukamilisha majadiliano na Umoja wa Ulaya kuhusu Programu hii, kwa mujibu wa ratiba ya utekelezaji wake, EU Commission ilipaswa kuwa imetia saini ya kuidhinisha Mpango huu kwa upande wake mwezi huu wa Novemba ili mikataba ya Fedha (Joint Financial Agreement) isainiwe baina ya EU na Tanzania mwezi Februari mwakani kuruhusu Programu kuanza. Sasa utiaji wa saini kuidhinisha Programu hiyo umesubirishwa. Tunatumaini tutaendelea kujadiliana na Umoja wa Ulaya ili hatua zilizosalia za utiaji wa saini zikamilike kabla ya Februari mwakani kuruhusu Programu Februari kuanza kama ilivyokuwa imepangwa.

Suala lingine linalopotoshwa ni kuhusu ukubwa wa madhara ya uamuzi huu, hususani kwenye Bajeti ya Serikali. Usahihi ni kwamba kiasi cha Euro Milioni 156 kwenye Programu ya Ushirikano na EU kwa mwaka 2025 siyo kwa ajili ya Bajeti ya Serikali Kuu (Budget Support), wala hazitarajiwi kuingizwa kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali.
Fedha hizo zinaenda wapi?

Kwa ujumla fedha hizo zimepangwa kwa ajili ya miradi mitatu mikuu kama ifuatavyo.

i. Mradi wa Together4Value

Mradi huo wenye jumla ya Euro milioni 129, unalenga kuimarisha minyororo ya thamani katika sekta za madini na kilimo. Kati ya fedha hizi, ni Euro milioni 13 pekee ndizo ambazo zinakwenda moja kwa moja kwenye taasisi za Serikali (Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji) sawa na asilimia 16 ya mradi wote. Sehemu kubwa ya fedha, takribani Euro milioni 116 zitasimamiwa kupitia utaratibu wa indirect management kupitia mashirika ya nchi wanachama wa EU, taasisi za ndani na za kimataifa na kampuni za ushauri.

ii. Mradi wa Uchumi wa Kidijitali Tanzania na Uunganishaji (Tanzania Digital Economy and Connectivity Initiative (TANTECH) Mradi huo wenye thamani ya Euro milioni 20, ulibuniwa kuchochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali na ubunifu. Kati ya fedha hizi, Euro milioni 1.5 ambazo ni sawa na asilimia 7.5 ya Bajeti yote ndizo tu zimepangwa kwenda moja kwa moja Serikalini kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Fedha zilizobaki takribani Euro milioni 18 zitaelekezwa kupitia mfumo wa indirect management kupitia taasisi za nchi wanachama wa EU, NGOs na sekta binafsi.

iii. Mfuko wa Ushirikiano (Cooperation Facility)
Mradi huo wenye Euro milioni 7, unalenga kuimarisha uratibu wa ushirikiano kati ya Tanzania na EU. Katika mradi huu, Euro milioni 2.5 sawa na asilimia 35 ndizo zimepangwa kwenda moja kwa moja kwa Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango. Kiasi kilichobaki takribani Euro milioni 4.5 kimepangwa kutekelezwa kupitia wataalamu elekezi na taasisi za ndani za kimataifa katika mfumo wa indirect management.

Kwa mnyumbuliko huu, kati ya Euro milioni 156 za AAP 2025, ni Euro milioni 17 tu (sawa na asilimia 10.9%) ndizo ambazo zinakwenda moja kwa moja kwenye miradi Inayotekelezwa na taasisi za Serikali, huku zaidi ya Euro milioni 138.6 (asilimia 89.1%) zikiwa zimepangwa kutekelezwa kupitia mfumo wa indirect management unaohusisha mashirika ya Sekta binafsi kwa kushirikiana na mashirika ya EU, mashirika ya Kimataifa, NGOs, kampuni za ushauri za kimataifa.

Hivyo, ni sehemu ndogo ya fedha hizo itakayoelekezwa kwenye miradi ya baadhi ya taasisi za Serikali. Sehemu kubwa ya fedha hizo zinatarajiwa kuekelezwa kwa wadau mbalimbali nje ya Serikali hususan Sekta Binafsi ya Tanzania kwa ushirikiano na baadhi ya Sekta binafsi ya Ulaya, mashirika ya kimataifa, asasi za kiraia, na taasisi za ndani na za kimataifa za ushauri wa kitaalamu (consultancies).

Kwa hiyo, hatua yoyote ya kuchelewesha kusaini fedha hizi haiathiri Serikali pekee. Inaathiri mfumo mzima wa wadau wa maendeleo, ikiwemo Sekta binafsi za Tanzania na za Ulaya na Taasisi zingine ndani, taasisi za Ulaya zinazotarajiwa kushirikiana nasi katika kutekeleza miradi, mashirika ya kimataifa, wataalamu wa ndani na nje, na hatimaye wananchi wanaotarajiwa kunufaika na miradi iliyopangwa kutekelezwa kupitia fedha hizo.

Ni kwa mantiki hiyo, na kwa kuzingatia manufaa tarajiwa katika programu hii kati ya wadau wa ndani na nje, Serikali pamoja na EU zitaendeleza majadiliano kwa haraka kuwezesha utiaji wa saini wa Programu hizo kufanyika mapema kadri inavyowezekana ili kuepuka athari zinazoweza kujitokeza kwa wadau mbalimbali kama ambavyo nimeeleza hapo juu. Naamini kwa ufafanuzi huu jamii yetu itapuuza taarifa zozote za upotoshaji unaojitokeza katika eneo hili na kwa pamoja kuendelea kuthamini ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Umoja wa Ulaya na pia kuendelea kutumia fursa za kunufaika na ushirikiano huo kwa kadri zinavyojitokeza.

IMG-20251128-WA0055.jpg
IMG-20251128-WA0056.jpg
IMG-20251128-WA0057.jpg
IMG-20251128-WA0058.jpg
IMG-20251128-WA0059.jpg
 
Wamekaza,ni mwendo wa kutumishiana misuri tu,hakuna mnyonge heee.
 
Nani kaandika hiki kipeperushi kimechanganya lugha hata hivyo hawa wenzetu wanapenda kujidanganya na kauli zao za kujita sovereign state hatuingiliwi wala kuingiliwa na mamlaka nyingine, niwakumbushe tu human rights are universal kwenye yale mauaji ya kibali hakuna kitu kama hicho wanachodanganya
 
Kama hamuathiriki mnaomba majadiliano ya nini? Mnadai haki ya kusikilizwa mlishajibiwa nyie mbona haki hio hamuwapi Wana chi wenu? Vichwa maji nyie
 
Back
Top Bottom