Kuhusu bam & gs ktk mtaala wetu wa elimu ya a-level

Kuhusu bam & gs ktk mtaala wetu wa elimu ya a-level

Brother James

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
233
Reaction score
172
Wana JF, mmewahi kufikiria kuhusu wanafunzi wetu wa A-Level wanavyopotezewa muda wao juu ya masomo ya Basic Applied Mathematics (BAM) na General Study (GS)???
Kwa mchango mkubwa wa masomo haya mawili kwa wanafunzi wetu wa A-Level nilidhani labda mtaala wa kitanzania ungeweza kuthamini michango mikubwa ya haya masomo lakini imekuwa kama sehemu ya watu kupotezewa muda wao kwani wanafunzi wengi wamekuwa wakipoteza muda wao mwingi tu kujisomea masomo yasiyo na tija kwao.
Masomo haya hayana tija wala thamani kwa mtaala wa Kitanzania kwa sababu Serikali haijaweka motivation katika performance kwa wanafunzi wote wanaosoma masomo haya ndio maana mwisho wa siku wanafunzi wetu huwa hawafuatiliii kwa karibu kwenye masomo husika na kusababisha failure nyingi sana, mfano ni matokeo ya BAM na GS kwa kidato cha Sita mwaka 2013.
GS na BAM ni masomo yanayojitegemea sawa sawa kabisa na masomo kama Kiswahili, Physics, Math, Geog etc....na kwa sababu ya umuhimu wake serikali inayaita Compulsory subjects lakini hayathaminiwi, eti ukifeli BAM hata kama una Div. I unarushwa hadi Div. III, kama cut points za vyuo vikuu huangaliwa ktk majors/combinations za masomo je hapo GS na BAM itaonekanaje kuwa inaumuhimu??
USHAURI:
1. Kama serikali inaona BAM na GS ni muhimu basi mtaala wetu uyathamini na kuhakikisha kuwa inakuwa na grades kwa mtu anayeyachukua na kumuongezea credits katika combination zake sawa sawa kabisa na masomo ya comb. Au mwanafunzi akifeli basi yaonyeshekuwa yana negative effects kwa mhusika kiasi kwamba hata uwezekano wa kupata Vyuo uwe mdogo sana.
2. Kama hayana msaada wala tija kwa taifa kama yanavyofanywa kwa sasa, ni bora yafutwe au yaingizwe kwenye combinations zilizopo au yatengenezewe combination nyingine mpya ili wanafunzi wasomee, kwani kwa sasa wanafunzi wanapewa mzigo mzito wa kuyasoma na mwisho wa siku hayawafaidishi.

JE WEWE MWANA JF UNA MAWAZO GANI JUU YA HAYA MASOMO.........................!!!!!!!!!!!!!!!!!!
3.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
nakubaliana nawe yawekwe kama core na ukipata a waweke a siyo s,yawe muhmu.
 
Dan36,
Nadhani hata wewe utakuwa umepoteza muda mwingi sana kuyaangaikia hayo masomo kama uliyachukua A-Level lakini mwisho wa siku hayana faida wala msaada wowote katika ufaulu wako
nakubaliana nawe yawekwe kama core na ukipata a waweke a siyo s,yawe muhmu.
 
Back
Top Bottom