Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,288
Kwa wanaofuatilia historia ya nchi yetu tangia uhuru, ambapo baada ya uhuru makampuni, viwanda, mashamba makubwa, shule, benki nyingi zilikuwa chini ya sekta binafsi.
Nyerere kwa uelewa wake akataifisha vitega uchumi hivi na kuvifanya mali ya Serikali.
Uchumi wa Tanzania ukayumba sana, viwanda vikafungwa, mashamba makubwa yaliyokuwa yanazalisha chakula kingi yakafa, benki na kampuni nyingi pia vikafa, watu kupata mlo mmoja ikawa ni starehe.
Rais Mkapa ndio Rais aliyekuwa bold kufanya ubinafsishaji wa vitega uchumi, na kuleta uwekezaji wa nje, japo kuna baadhi haukuwa mzuri ila ubinafsishaji ulileta impact kubwa chanya kwenye ukuaji.
Ukianga trend ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, Uchumi wetu ulikuwa kwa kasi kubwa zaidi kipindi cha Mkapa kuliko kipindi chochote kile, makampuni makubwa ya mawasiliano, vinywaji pombe, mabenki ambayo ndio walipa kodi wakubwa katika Tanzania ya sasa yakizaliwa kutokana na sera za ubinafsishaji na uwekezaji wa nje.
So kwenye hili la mwisho ubinafsishaji wa bandari ya Dar, yapaswa tutumie zaidi mantiki kuliko mihemko.
Tukosoe ni kipi kiboreshwe kwenye huo mkataba, umakini upi ufuatwe, na sio kupinga totally kuwa ni kitu kisichofaa.