Kuhusu chanjo ya COVID-19: Tuijue dhana ya "moving target"

Kuhusu chanjo ya COVID-19: Tuijue dhana ya "moving target"

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Wazungu wenyewe wanakiri kuwa corona virus is a moving target. Kwa maneno mengine ni kwamba kirusi cha corona ni shabaha inayotembea.

Ili kuielewa dhana hii nitatumia mfano rahisi. Tufananishe kirusi cha corona kama nyoka mkubwa sana na mkali. Huyo nyoka ulimwona mahali fulani mwaka 2019, na tangu ulipomwona ukaanza kutafuta bunduki na risasi utakayoitumia kumlenga huyo nyoka mahali pale pale alipokuwa mwaka 2019!

Kwa bahati nzuri ukafanikiwa kuipata bunduki na risasi mwaka 2021. Swali: Je, mwaka 2021ukitumia bunduki na risasi kumlenga huyo nyoka mahali alipokuwa mwaka 2019 je utafanikiwa kumpiga na kumwua? Jibu ni hapana! kwa sababu nyoka huyo hatakuwa sehemu hiyo hiyo alipokuwepo mwaka 2019, atakuwa ameenda sehemu nyingine!

Ndivyo ilivyo kwa corona virus. Hii chanjo inayopigiwa debe sasa ililenga kudhibiti corona virus kama alivyokuwa mwaka 2019. Lakini kwa leo sehemu kubwa ya corona imebadilika, kwa hiyo chanjo itakutana na corona tofauti na hakuna uhakika kama itamdhibiti!

Wazungu wanajua hivyo! Lakini kwa kuwa tayari wameshaingia gharama wanalazimisha nchi zote zichangie hiyo gharama huku wakijua hii chanjo imeshapitwa na wakati tayari. Ukikubali kuchukua tu hiyo chanjo utalazimika kuingia mkataba wa kuchangia katika mfuko wa covax unaogharimia chanjo kwa nchi zinazoendelea!! Japo wanakuambia hiyo chanjo ni bure. Hakuna kitu cha bure kwa mzungu!! Nimesoma vizuri masharti ya kunufaika na chanjo za covax!! Ingia kwenye mtandao usome!

Pamoja na kuwa target imeshahama lakini hata kama ingekuwa haijahama, hakuna chanjo salama inayoweza kupatikana kwa mwaka mmoja.. Mwaka mmoja hautoshi kubaini madhara ya muda mrefu kwa mwanadamu. Kinachofanyika kiuhalisia ni kuwa bado hiyo chanjo iko kwenye majaribio. Na walengwa wa majaribio ni waafrika!! Yawezekana kabisa huko Ulaya wanapewa placebo (yaani maji tu), isiyokuwa na madhara! Halafu waafrika wakaikubali eti kwa sababu na wazungu wamechanjwa.

Tusidanganyike! Ni suala la muda tu kila kitu kitadhihirika, wazungu wamedungwa placebo, na hawatakuwa na ujasiri wa kuachana na tahadhari maana wanajua kuwa hawajachanjwa bado! Watukome!
 
Hizi porojo za reja reja ni za watu wasio na elimu (hata kama wamesoma), wasiojua kabisa misingi ya kisayansi, na wasio na uwezo wa kusoma habari/ taarifa/ mijadala makini duniani.

Hakuna aliyelazimishwa kupokea chanjo ya covid-19 wala kuchanja. Tanzania tumeikataa na hakuna aliyetubana kwa uamuzi wetu huo hata kama una mushkeli. Hakuna mtu anayeweza kukugawia vieite halafu akulazimishe ulipokee. Una uhuru wa kukataa. Mipasho haihitajiki.
 
Nimejaribu kusoma ni uharo mtupu, hakuna aya, uandishi mbovu, hoja mbovu, uharo uharo.

Kwamba wazungu/watu weupe wote Duniani watengeneze chanjo fake kwa watu wao ili tu kuwaaminisha waafrika lakini chanjo hiyo inalenga kuwaondoa waafrika wote hapa Duniani.

Hawa ndio wasomi wa nchi hii.
 
Summarize kazi yako katika paragraph moja
Kisha utume tena. Hii ni barua.
 
Kama umemaliza, basi geuza ubavu mwingine uvute na shuka mpaka utosini ili uendelee kuuchapa usingizi wa pono.
 
Mambo ya civics na historia unaleta kwenye sayansi?

Hiki ni kipande cha hadithi kisicho na sayansi, unakaa unafikiri na kuota then unakamilisha kuwa ndivyo ilivyo leta kitu with substantial evidence/facts tafadhali. Kwa heshima na taazima.

Wenzio wanakesha maabara kutafuta facts, wewe uko kitandani unaota facts. What a gape?
 
Nimejaribu kusoma ni uharo mtupu, hakuna aya, uandishi mbovu, hoja mbovu, uharo uharo.

Kwamba wazungu/watu weupe wote Duniani watengeneze chanjo fake kwa watu wao ili tu kuwaaminisha waafrika lakini chanjo hiyo inalenga kuwaondoa waafrika wote hapa Duniani.

Hawa ndio wasomi wa nchi hii.
CHANGIA hoja! Hoja ni kwamba "corona virus is a moving target!" Jinsi ilivyokuwa 2019 sivyo jinsi ilivyo 2021. Kwa kiasi kikubwa imebadilika through mutation!! Kwa maana hiyo chanjo inayotengenezwa 2021ili kukabili corona ilivyokuwa 2019 itaambulia patupu!! haina uhakika wa kudhibiti hao new corona virus variants!! Upo hapo?
Ndio maana south africa wameshindwa kutumia chanjo waliyonunua maana imeshindwa kudhibiti aina mpya ya corona iliyozuka nchini mwao.
 
Hizi porojo za reja reja ni za watu wasio na elimu (hata kama wamesoma), wasiojua kabisa misingi ya kisayansi, na wasio na uwezo wa kusoma habari/ taarifa/ mijadala makini duniani.

Hakuna aliyelazimishwa kupokea chanjo ya covid-19 wala kuchanja. Tanzania tumeikataa na hakuna aliyetubana kwa uamuzi wetu huo hata kama una mushkeli. Hakuna mtu anayeweza kukugawia vieite halafu akulazimishe ulipokee. Una uhuru wa kukataa. Mipasho haihitajiki.
Jibu hoja ya corona virus is a moving target! Kama huwezi pita kimya!
 
Watu wa aina hii ndio wanaosababisha watanzania tuonekane tuna IQ ndogo.
 
Badilisha hilo jina andika "kuzimukwetu" hakuna watu wenye akili ndogo hivyo mbinguni
 
Kama nawaona maajenti wa Kinjekitile Ngwale walivyokuwa wakiyatolea ufafanuzi Maji yanayoaminika kuwa na dawa ya kuzuia risasi na Mizinga na kuyapamba kama Leo tunavyoipamba Nyungu
Ghafla maiti zikaanza kujaa kwenye battlefield
Sasa hivi maiti hazionekani kwa wingi ila kila Mkoa na kila Wilaya kila kitongoji watu wanaangamia
 
Uamuzi upo nao hivyo usitoe thread kuhimiza wengine utafute wa kufa naye au kukufariji
 
Back
Top Bottom