Kuhusu Deni la Nchi yetu Tanzania

Kuhusu Deni la Nchi yetu Tanzania

S.M.P2503

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2008
Posts
2,421
Reaction score
4,344
Ndugu Mheshimiwa Rais, Mama Samia, najua unasomoga humu, au kama husomagi najua wapo wanaokusomeaga comments za humu za watapika nyongo.
Niende moja kwa moja kwenye kichwa cha habari hapo juu...

1. Anzisha utaratibu mpya wa ku-service deni la taifa bila kusibiri liive ndio tuanze kutafutana kama nchi... kwa mfano, weka kodi maalum ya Tsh 5 kwa kila lita ya petrol, diesel, mafuta ya taa, magfuta ya kula, bia, soda, sigara, juice na kila aina ya bidhaa na makololo mengine ili tuweze kujikwamua ( self sufficeint huko mbeleni katika matrilion haya tuliyokopa tangu enzi na enzi.
2. Anzisha utaratibu mwingine wa kodi ya miundombinu ya Tsh 5 kila kitu kinachonunuliwa ili tuweze kujikamalisha katika miundombinu , iwe ya barabara, afya, maji etc, na tuweke utaratibu kwamba ndani ya miaka 30- 50 haya mambo ya mikopo yawe historia.

3. Anzisha oversight commitee ya wenye weredi wa kusimamia ukusanyaji, uratibu na matumizi ya kodi hizi maalumu.

4. Tuweke vipaumbele vya nini cha kufanya ili tuwe self sufficient ndani ya miaka 40 toka sasa kwenye vitu muhimu mf. chakula, afya, miundombinu etc.

5. Tuendelee kupoka na kuyafanya yote yaliyokusidiwa kwa maslahi mapana ya nchi yetu.

6. Kwa wote wataopatikana na ubadhirifu wa mali ya umma ikiwemo fedha, adhabu yake iwe direct bila chenga chenga- kifo au jela ndefu. Ndivyo wenzetu huko duniani wanavyo fanya bila kupepesa macho.

7. Usije sema hukuambiwa, hukusoma, hukusomewa wala kutafakali namna ya kujikwamua na madeni haya ya Matrilion.

8. Tukubaliane kwamba muda ukifika haya madeni tutayalipa tu, tutake tusitake... hivyo tujipange sasa na tusisubiri yaive ndio tukabane mashati...

Ni hayo tu ndugu zangu, Povu ruksa bila matusi...
 
Mbona unahema hivi, tulia

Halafu ni Weledi siyo weredi
 
Shida pesa zetu zinaliwa hatupewi mrejesho zimekusanywa kiasi gani na zimetumikaje. Kwani saivi tunapewa mrejesho wa tozo???
 
Back
Top Bottom