Kuhusu fedha za likizo kwa waalimu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu!

Kuhusu fedha za likizo kwa waalimu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu!

Mwamgunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
247
Reaction score
48
Tulijaza fomu za kuomba kulipwa fedha za likizo tangu mwezi wa 11 mwaka jana, mpaka leo hakuna kitu kilichofanyika, hata wale walioomba malipo hayo mwezi wa sita mwaka jana hakuna malipo waliyopewa. Tunafungua shule trh 13 yaani wiki ijayo, je tukigoma kuingia madarasani kufundisha hali itakuwaje? Nikuombe tu afisa elimu wilaya ya Busega ndg Yasini usije ukathubutu kufika shuleni ninakofundisha na kuniomba scheme of work kabla sijalipwa fedha hizo, vinginevyo utajuta kunifahamu. Sikutishii ila huo ndio uhalisia! Siku njema kwenu waalimu, tuamke na kuikataa serikali kandamizi ya kifisadi ya CCM!
 
Duh, hata huku kwetu Shinyanga Vijijini bado, sijui tatizo ni nini tu.
 
na sio kwamba pesa hazipo laah! zote znaenda kwa mifuko ya wachache ndo mana utakuta maisha magumu secta ya ualim ni kwa walio chni tu yaan kuanzia walimu wa kawaida tubadirike walimu kwa kupgia debe serikal itayojal maslai ya kila mwananch Walimu tz polen sana kwa serikal ya kiundugu, kwa iyo likizo mshahara aujaingia?
 
Hata huku chunya toka mwezi wa sita fedha za likizo hazijalipwa na tumeisha fungua muhula mpya jumatav wiki hii.
 
huku wilaya mpya ya Kaliua mkoa wa Tabora hali ni
hiyo hiyo ila wanadai watalipa 40%,sijui tunaelekea wapi?Kwa upande wangu sirudi kituo cha kazi mpaka nipate haki yangu..nikiulizwa utetezi sina nauli..
 
Ualimu ni wito. Mkifukuzwa kazi mtaenda wapi?
 
Back
Top Bottom