Kuhusu hospital ya wilaya ya Ubungo, ni propaganda au Rais kapotoshwa na RC?

Kuhusu hospital ya wilaya ya Ubungo, ni propaganda au Rais kapotoshwa na RC?

Mkuu maswala ya mavazi hayana mipaka hata wewe ungeweza vaa Yale magwanda yetu ya kikamanda na ukaa viti vya mbelembele hakuna Ambaye angekuzuia.
Ko tujifunze ku control hasira binafsi
Muulize yule diwani mbishi wa cdm kule kigoma!! Kwenye mkutano wa waziri mkuu, nini kilitaka kutokea sema uzuri yule jamaa ni mbishi kweli kweli ndio kilichomsaidia!!wao kuvaa wanaona ni halali ila wengine ni kosa!!!
 
Atapotoshwa vipi kama mwenyewe 'hataki kupotoshwa'? Mambo mengine muwe mnatumia akili kuyaelewa.
 
Hao wapinzani kina Boniface kutwa kumtukana raisi na kugomea Bajeti bungeni,

Mikutano ya Serikali hamtokei , halafu mnataka Rais awasaidie ,ili kwenye kampeni mdanganye wananchi


Shwain
raisi hana cha kumsaidia mtu yoyote yeye ndiye anayesaidiwa na watanzania kuanzia nguo anazo vaa kitanda na shuka analo jifunika ni msaada kutoka kwa watanzania. hivyo kila kitu anacho fanya ni wajibu sio hisani. elewa dogo na jaribu kufikiri kabla ya kukomenti.
 
Makonda yupo hapo kumfanyia JIWE udalali wa ushirikina; ndio maana sio anaogopa kumtumbua tu bali anaogopa hata kumuondoa Dar!!
 
Ungekuwa unahudhuria ingerahisi kwako kujibu hoja papo kwa papo. Kususa kwako ndiko Kuna wagharimu. Sasa humu anasoma nani? Kwani mzee yupo humu au wanaomoelekea

Hawezi kupata nafasi ya kujibu huo utumbo hata angekuwepo mkutanoni kwani ratiba ya nani azungumze wanaithibiti wao!!! Huoni Bashite aliambiwa atumie dakika mbili kuzungumza yeye akatumia robo saa!!! Jiwe na watu wake sio tu kuwa wamo JF, isipokuwa wanalala humu kwahiyo ujumbe wa Meya wameupata!!
 
[Siasa kamchezo kachafu mno humu duniani, ila bila kukacheza mambo hayaendi ng'o.QUOTE="chuuma, post: 33270701, member: 296970"]
Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli,leo nimekusikia ukimjibu Makonda kuwa Unatupatia watu wa Ubungo pesa za Kiasi cha Tsh Billioni 1.5 za Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya baada ya yeye binafsi Kukuomba.

Mheshimiwa nakukumbusha wewe na Wasaidizi wako wote kuwa Mwaka huu 2019 Mwezi wa 2 Tarehe 28 Baraza la Manispaa Ubungo lilipitisha Kiasi cha Tsh billioni 84 kuwa bajeti yake ya 2019/2020.

Katika Bajeti hiyo Sisi Manispaa tulitenga kiasi cha Tsh Millioni 250 kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya,na tukaiomba serikali kupitia Ruzuku za Miradi ya Maendeleo mnazotushushia mtuletee kiasi cha Tsh Billioni 1.5

July 2019 Bunge likapitisha Bajeti ya TAMISEMI ikiwemo maombi ya pesa zote mbili ,ile ya Wilaya na zile za mapato ya Halmashauri.

Na July hiyohiyo wakati tunafunga Mkutano Mwisho wa Mwaka 2018/2019 katika Baraza la Madiwani nikakushukuru wewe Binafsi na Serikali kuu kutushushia kiasi cha Billioni 3 Pesa za Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri,Billioni 1 ya Ujenzi wa kituo cha Afya Kimara Mwisho, na hizo billioni 1.5 za Ujenzi wa Hospitali ya wilaya.

Ila kosa lake Mkuu wa Mkoa nililelile ulilosema wakati Ufunguzi wa Kiwanda Cha Mabomba,ulisema anajishughulisha na Mambo yasiyo ya Msingi na ajui Miradi yoyote katika Mkoa wake,

leo si unaona kakuomba tena kitu kilekile ulichokuwa tayari umeshakifanyia kazi na kukipatia Ufumbuzi,!!

Akiendelea hivyo kuna Siku atakuomba Pesa za Ujenzi wa Flyover Ubungo,Asijue kuwa Mradi upo asilimia 50.

MWISHO
Sisi Viongozi wa Upinzani,Mwanzo tulikuwa tunashiriki Vizuri Mikutano yako tukiamini ni kwa Maslahi ya Taifa,

ila kwa Sasa hatuji tena katika Mikutano yako,ambayo tunajua Mkuu wa Mkoa atashiriki,kwa Sababu amekuwa akitumia Mikutao yako kutudhalilisha Viongozi wenzie mbele yako

Na wewe tunasikitika ujawahi kumkemea hata Mara Moja, kiasi tunafikiria wakati mwingine anatumwa kufanya hivyo au Viongozi wetu Mnafurahia Udhalilishaji huo kwa viongozi wenzie,
Nasisi hatuji kuepusha Shari Mkuu!!

Boniface Jacob
Mstahiki Meya Ubungo
[/QUOTE]
 
Paulo Makonda aka Albert Bashite unamdhalilisha sana Rais, lakini kwa vile umemfunga kwa nguvu za Giza basi haoni wala hasikii tena juu ya upumbavu wowote ufanyao.
Sasa kumbe mambo yamesha zungumzwa baraza LA madiwani, bajeti imeshapita na serikali kuu kupitia bunge imepitisha fedha za mradi huo, sii ni kumdhihaki Rais mbele ya watu wenye akili?
Na nyie washauri wa Rais fedheha za namna hiyo mnaziona bado hamu muonyi Rais kuwa hili zigo la Dar ni furushi la uchafu kubeba kichwani ni kujichafua? Au na nyie nguvu hizo za Giza zimewaathiri hivyo tumkodie Rais kampuni kama Net Group Solution kuwa washauri wa Rais?
Makonda acha kumpoteza maboya Rais, ujue unaikosea nchi yote.
Tumia muda wako kusoma makabrasha ya mkoa wako acha kuishi kishambenga kama kina Steve Nyerere au Le mutuz.
Mkuu huyo mwenyewe ndiye mtengenezaji wa sinema zile. Alishamuandaa kuwa aanzeje naye amalizeje. Wote ni wa kuwaogopa kama ukoma. Ni meza na miguu yake. Ukiondoa mguu mguu meza haitaweza simama.
 
Muulize yule diwani mbishi wa cdm kule kigoma!! Kwenye mkutano wa waziri mkuu, nini kilitaka kutokea sema uzuri yule jamaa ni mbishi kweli kweli ndio kilichomsaidia!!wao kuvaa wanaona ni halali ila wengine ni kosa!!!
Jaribu kuelezea japo kwa ufupi kilichomutokea kwa faida ya hata wale ambao hawakuweza kufuatilia Hilo tukio lakini unapoishia kusema jamaa alikuwa mbishi hatutaelewa ubishi unaousemea mkuu.
 
Jaribu kuelezea japo kwa ufupi kilichomutokea kwa faida ya hata wale ambao hawakuweza kufuatilia Hilo tukio lakini unapoishia kusema jamaa alikuwa mbishi hatutaelewa ubishi unaousemea mkuu.
Kulikuwa kuna mkutano wa waziri mkuu na viongozi wa mkoa/halimashauri kigoma ccm wakaja wamevaa sale zao kama kawaida, na yule diwani wa chadema naye akavaa za cdm na shingoni akatundika skafu ya chadema, wakaja viongozi wa mkoa eti wanataka kumtoa kwenye ule mkutano kuwa hauruhusiwi kuvaa vile, ilikuwa vurugu hadi ikabidi wamuache tu. Aliwaambia mbona hao wa ccm wamevaa, ila mimi tu ndio kosa na sio kikao cha chama chenu? Siku hizi kila mkutano umekuwa ni wa kisiasa tu, kuzindua mradi u chama
 
raisi hana cha kumsaidia mtu yoyote yeye ndiye anayesaidiwa na watanzania kuanzia nguo anazo vaa kitanda na shuka analo jifunika ni msaada kutoka kwa watanzania. hivyo kila kitu anacho fanya ni wajibu sio hisani. elewa dogo na jaribu kufikiri kabla ya kukomenti.
Bila shaka wewe Ni baba wa familia na naomba nikuulize maswali machache tu hata Kama usipoyajibu wewe Ila nafsi yako itakujibia;
Je Watoto wako wanasomea shule za Maana au wapo shule za kata?
Je una investment yeyote uliyowaandalia Watoto wako ukiwa Kama baba Yao?
Je familia yako inapata mahitaji yote mhimu matatu ya familia ipasavyo?
Je huwa unawasaidia ndugu zako wanapohitaji msaada kutoka kwako?

NOTE; Maswali yote hayo yanahusu wajibu wa baba katika familia japo ukweli Ni kwamba siyo kila Aitwaye baba huwa anauwezo wa kutimiza wajibu wake katika familia na baba anaetimiza inatakiwa apongezwe na kushukuliwa kwa Kazi na juhudi zake alizonazo.

Likewise; Siyo kila Rais anauwezo wa kutimiza wajibu wake kwa Wananchi, Marais wapo wengi Sana lakini wanaotimiza wajibu wao wapo Wachache hivyo Basi ikitokea akawepo Rais anaetimiza wajibu wake kwa Wananchi Hana budi kupewa sifa na kuombewa mazuri kwa jitihada zake.

Mwisho;Mkuu inatakiwa tu utambue yakuwa wewe Ni baba na Mo dewj Ni baba lakini utafauti wako na Mo Ni kuwa Mo anatimiza wajibu wake kwa familia Kama baba Ila wewe Ni baba Ambaye hujatimiza wajibu wako kwa familia yako.
Lakini pia usisahau kujibu maswali yangu hapo juu.
 
Kulikuwa kuna mkutano wa waziri mkuu na viongozi wa mkoa/halimashauri kigoma ccm wakaja wamevaa sale zao kama kawaida, na yule diwani wa chadema naye akavaa za cdm na shingoni akatundika skafu ya chadema, wakaja viongozi wa mkoa eti wanataka kumtoa kwenye ule mkutano kuwa hauruhusiwi kuvaa vile, ilikuwa vurugu hadi ikabidi wamuache tu. Aliwaambia mbona hao wa ccm wamevaa, ila mimi tu ndio kosa na sio kikao cha chama chenu? Siku hizi kila mkutano umekuwa ni wa kisiasa tu, kuzindua mradi u chama
Hapo sawa.
lakini suala la Wana CCM kuvaa sare zao kwenye uzinduzi wa mirad ya kitaifa Ni sawa kabisa kwasababu hata ilani inayotumika kukamilisha hizo Miradi Ni ilani Yao ya CCM kwa hiyo pale serikali inapotekeleza suala lolote ambalo lipo kwenye ilani Yao lazima wakiwakilishe chama Chao kwa Wananchi kuwa walichokiahidi wakati wa kunadi ilani Yao ya chama amaboyo ndo kiongozi wa shughuli za kiserikali imetimia. Au mkuu hujui kama serikali haina ilani ya kuleta maendeleo?
Labda tu nikusaidie serikali huwa inatumia ilani ya chama kuleta maendeleo kwa Wananchi wake. Ko chama fulani kinapokuwa madarakani ndo kinakuwa kiongozi wa Miradi yote ya kitaifa na ndo Maana unaona kila mradi unaozinduliwa kitaifa lazima watu waliovaa sare za CCM wawepo maana ndo maboss wenye ilani inayoongoza hizo Miradi ya kitaifa
 
Sasa kwani Makonda kafanya kosa gani? Kumbe kakumbushia mliokuwa mnayaomba kila leo?
Kakumbushia kwani Rais ndio mtekelezaji wa budget ya serikali? Mbona mnakuwa wajinga kiasi hiki?
Kweli kila fedha iliyo bajetiwa lazima rais akumbushwe ndio itoke? Ni serikali ya namna gani hiyo hapa duniani? Maana hata tawala za kifalme sivyo zilivyo. Mumechemsha
 
Ungekuwa unahudhuria ingerahisi kwako kujibu hoja papo kwa papo. Kususa kwako ndiko Kuna wagharimu. Sasa humu anasoma nani? Kwani mzee yupo humu au wanaomoelekea
Kwa hiyo wangekuwepo wangeanza kusutana? Akili matope bwana!
 
Nyie maboya kwanini hamtaki kujifunza, fedha za Serikali sio mali ya RAIS ni fedha inayotokana na kodi za wananchi na zinatakiwa zitumike kwa maendeleo yao. Kazi ya kugawa fedha za maendeleo sio kazi ya EXECUTIVE ni kazi ya Bunge!! JIWE KUJIFANYA anagawa fedha kiholela ni kukosa nidhamu ya usimamizi wa fedha za umma.
Mkuu kuna wakati unaweza kukufuru kuwa hawa watu waliumbwa na akili za punda kubeba mizigo na sio kwa manufaa ya ustawi wa binadamu.
Nadhani hata wale wachache wa ccm wenye akili wanajisikia aibu kuwa na mifugo ya aina hii
 
Bila shaka wewe Ni baba wa familia na naomba nikuulize maswali machache tu hata Kama usipoyajibu wewe Ila nafsi yako itakujibia;
Je Watoto wako wanasomea shule za Maana au wapo shule za kata?
Je una investment yeyote uliyowaandalia Watoto wako ukiwa Kama baba Yao?
Je familia yako inapata mahitaji yote mhimu matatu ya familia ipasavyo?
Je huwa unawasaidia ndugu zako wanapohitaji msaada kutoka kwako?

NOTE; Maswali yote hayo yanahusu wajibu wa baba katika familia japo ukweli Ni kwamba siyo kila Aitwaye baba huwa anauwezo wa kutimiza wajibu wake katika familia na baba anaetimiza inatakiwa apongezwe na kushukuliwa kwa Kazi na juhudi zake alizonazo.

Likewise; Siyo kila Rais anauwezo wa kutimiza wajibu wake kwa Wananchi, Marais wapo wengi Sana lakini wanaotimiza wajibu wao wapo Wachache hivyo Basi ikitokea akawepo Rais anaetimiza wajibu wake kwa Wananchi Hana budi kupewa sifa na kuombewa mazuri kwa jitihada zake.

Mwisho;Mkuu inatakiwa tu utambue yakuwa wewe Ni baba na Mo dewj Ni baba lakini utafauti wako na Mo Ni kuwa Mo anatimiza wajibu wake kwa familia Kama baba Ila wewe Ni baba Ambaye hujatimiza wajibu wako kwa familia yako.
Lakini pia usisahau kujibu maswali yangu hapo juu.
kwanza uwezo wako wa kufikiri na wa kujenga hoja ni duni. pia ulinganisho wako na hoja unayo jaribu kujenga haviendani. ila kwa vile umeonyesha nia ya kutaka kuelewa nitakujibu maswali yako japo kuwa hunijui na wala huwezi kujuwa kama nimekujibu kweli au la. swali la kwanza unataka kujuwa kama mimi ni mzazi. mimi ni mzazi wa wawili na ni mzazi ninaye timiza wajibu wangu kwa asilimia mia wanangu wote wako private school za uhakika. pili kuwa mzazi anaye wajibika sio lazima uwe na hela kama mo au tajiri
 
Primitive politics! Some people are a disgrace to public office. Lilliputs are running down our system of government. Is there no one to stop this nonsense? Not even the party in government? Nadhani katiba mpya itakapoandikwa kuna mambo ya msingi ya kuvitaka vyama vya siasa viyazingatie kwenye katiba zao.
 
Back
Top Bottom