Kuhusu idadi ya wachezaji wa kimataifa, najiuliza hili

Kuhusu idadi ya wachezaji wa kimataifa, najiuliza hili

Orketeemi

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
5,063
Reaction score
12,866
Et nimesikia baadhi ya klabu zinadai kuwa wachezaji watano tu wa kimataifa hawatoshi kuipa timu
uwezo wa kupambana na timu kubwa Afrika mfano TP Mazembe.,. Hii hoja ina mantiki kweli?

Hebu tujiulize hao watano tu waliopo ni yupi anaweza kupata namba kirahisi Tp Mazembe?
Mbona wengi wao hata benchi la Tp Mazembe hawawezi kulipata?
Hivi unaweza kuchukua wachezaji woote wa kigeni wanaocheza bongo ukaunda kikosi hatari nkinachoweza kuitoa Tp Mazembe klabu bingwa?

Nachelea kusema kwamba ukiunda first eleven ya maproo watupu waliopo Ligi ya Bongo waunde tim moja na ishiriki ligi kuu ya vodacom haiwezi kuchukua hata nafasi mbili za juu.
 
safari hii ni kumi acha watano tatizo wabongo wanapocheza mechi za kimataifa wanapanic hawatulii
 
Ni muhimu kuongeza wachezaji wa kigeni,wachezaji wa nje wana radha yake tofauti na wa kibongo...hebu jiulize ni mchezaji gani wa kibongo wa kumfananisha na mbuyu twite au okwi
 
ni muhimu kuongeza idadi ya wageni ili kuwafanya wenyeji wajitume kuipata namba ndio tutakuwa na timu nzuri za kupambana na etoile du sahel..
 
Emmanuel Okwi mgeni kutoka uganda unamfananisha na mchezaji gani wa kibongo!!

Pasca Wawa mgeni kutoka ivory coast utamfananisha na Hasan Isiaka wa simba!!

Hamis Tambwe utamfananisha na Maguli!!!

Haruna Niyonzima raia kutoka Burundi utamfananisha na kiungo gan wa kibongo!!!!

Vipi umewasahau akina kipre tchetche, michael balou, mbuyu twite, didier kavumbagu, chidiabere wa stand united, brian majwega!!!?

Idadi iongezwe hawa wabongo wetu wamekuwa mdobwedo sana...
 
safari hii ni kumi acha watano tatizo wabongo wanapocheza mechi za kimataifa wanapanic hawatulii

Mimi kinachoniuzi kuhusu wachezaji wa Kitanzania ni Kutokuwa na self awareness and determination sijui ni watu gani wasiokuwa na wivu wa maendeleo HENCE KUJITUMA KWA NGUVU ZAO ZOTE.
 
Mimi kinachoniuzi kuhusu wachezaji wa Kitanzania ni Kutokuwa na self awareness and determination sijui ni watu gani wasiokuwa na wivu wa maendeleo HENCE KUJITUMA KWA NGUVU ZAO ZOTE.

Fikiria kama Boban angekuwa na nidhamu na kujituma kama Twite? Ulaya alienda akaendekeza ujinga wa Bongo akarudi.
 
idadi ya wachezaji kumi wa kigeni ni muhimu sana kwa timu zetu..japo timu za simba na yanga ndio zinaharibu utaratibu huu kwa kusajili mapro wasiojua mpira lengo ni kupiga hela...nadhan ni wakati sasa wa tff kuweka masharti ya kumleta mchezaji wa kutoka nje...sio kusajili tu ilimradi anatoka njee ya nchi
 
Ligi ikiwa na wachezaji wazawa tupu inapooza na kupoteza mvuto. Pia hata ile sura ya professional league inatoweka.

Wachezaji wetu pia hawatapata changamoto mpya. Tutacheza mpira ule ule kwa mtindo ule ule.

Leo hii Yanga na Simba zinaposajili mapro, Thobias Kifaru anapata namna ya kuhamasisha timu yake iwakamie hawa vigogo na hivyo kuongeza ladha ya ligi. Viwango vya wachezaji vinapanda pale wanapopanga mikakati ya jinsi ya kuwazuia kina Okwi na Tambwe. Ni muhimu sana hata kwa mechi za kimataifa baadaye.
 
Halafu kitu kingine cha Kujiuliza, ni nchi ngapi ambazo zimewahi kufanikiwa kwa kubadili ligi za ndani zisiwe na wageni? Kwa nini lakini tunajidanganya kuwa timu zetu zikiwa na wazawa tupu ndio tutafanikiwa kucheza world cup? Au ACN?

Tatizo la msingi tunalikwepa kwa makusudi kabisa! Tusitarajie kwamba akina Msuva na Singano watakuja kuwa match kina Yaya Toure. Eti sentahafu Nadir Harub amuweke kati Wilfred Bony.

Kama hatuingizi vijana wetu kwenye advanced leagues, tutaendelea kupiga siasa za soka mpaka mwisho wa dunia. Nadhani bado kidogo tu tuzuie na makocha wageni.

Hebu jifunze jambo : yu wapi mfungaji bora wa ligi yetu? Kaenda kujaribiwa kwenye timu ya kawaida tu huko bondeni lakini mpaka leo kiza kinene.

Tuache siasa kwenye soka tutafute majibu ya maswali magumu.
 
Back
Top Bottom