The Bourne
JF-Expert Member
- Aug 24, 2017
- 1,077
- 1,321
KAMA HUMJUI MUNGU DUNIA ITAKUTESA!
Kwa Kanumba yule nimjuaye mimi. Na Lulu yule ninayemfahamu. Doooh! Ningekuwa Jaji wa kesi ya Lulu, ningekuwa nasikiliza kesi kama simulizi fulani ya mapenzi ili kuongeza ufahamu wa visa vya walimwengu.
Hata hivyo, mwisho kabisa wakati wa kutoa hukumu ningemwachia Lulu huru bila kuzingatia ni ushahidi kiasi gani unamtia hatiani.
Kwa ka-Lulu kale na li-Kanumba lile. Aisee, nini kumdondosha chini, hata kumtikisa apepesuke Lulu asingeweza, acha kuanguka na kifo juu.
Ukiliangalia li-Kanumba lile na ukakaangalia ka-Lulu kale, unajua tu kuwa siku ziliwadia. Na zikifika ni Mungu tu anayejua.
Ni hapo ndipo ubabe wa Mungu unapoonekana. Ka-Lulu kale kamekuwa sababu ya kifo cha li-Kanumba lile bila silaha. Halafu miuaji ile mizezeta na mi-SMG yao na risasi zao 40, imeshindwa kumuua Lissu ambaye hakuwa amevaa bulletproof.
Kama humjui Mungu hii dunia itakutesa sana.
Ndimi Luqman MALOTO