Kuhusu kesi ya Elizabeth Michael; Luquman Maloto, kama humjui Mungu dunia itakutesa!

NA JASHO LA NITIRIRIKA KWA AYA YAKO YA MWISHO

KUWA MUBABE ULE YA DUNIA/HAKI NI MBINGUNI
 
KAMA HUMJUI MUNGU DUNIA ITAKUTESA!

Kwa Kanumba yule nimjuaye mimi. Na Lulu yule ninayemfahamu. Doooh! Ningekuwa Jaji wa kesi ya Lulu, ningekuwa nasikiliza kesi kama simulizi fulani ya mapenzi ili kuongeza ufahamu wa visa vya walimwengu.

Hata hivyo, mwisho kabisa wakati wa kutoa hukumu ningemwachia Lulu huru bila kuzingatia ni ushahidi kiasi gani unamtia hatiani.

Kwa ka-Lulu kale na li-Kanumba lile. Aisee, nini kumdondosha chini, hata kumtikisa apepesuke Lulu asingeweza, acha kuanguka na kifo juu.

Ukiliangalia li-Kanumba lile na ukakaangalia ka-Lulu kale, unajua tu kuwa siku ziliwadia. Na zikifika ni Mungu tu anayejua.

Ni hapo ndipo ubabe wa Mungu unapoonekana. Ka-Lulu kale kamekuwa sababu ya kifo cha li-Kanumba lile bila silaha. Halafu miuaji ile mizezeta na mi-SMG yao na risasi zao 40, imeshindwa kumuua Lissu ambaye hakuwa amevaa bulletproof.

Kama humjui Mungu hii dunia itakutesa sana.

Ndimi Luqman MALOTO
Inabidi ufungiwe maisha.

Ni kosa kubwa sana kumdhihaki marehemu.

Cc:jamiiforums

Active moderator
 
Inabidi ufungiwe maisha.

Ni kosa kubwa sana kumdhihaki marehemu.

Cc:jamiiforums

Active moderator

Nakukumbusha watu walimdhihaki hata Yesu pale msalabani itakua Kanumba tena kafa kwenye uzinzi na ulevi,ukifa na hadithi yako imeisha hauna tena jipya acha waliobaki waendelee na maisha wakisubiri siku yao.
 
Hahaha
Mkuu kwani huwa hushuhudii Lori kubwa linamshinda Dereva?
Kwahyo kanumba alijidondosha mwenyewe?
Hakuna dereva aliyewahi kutokea duniani akaangusha gari. Gari huanguka lenyewe kwa sababu mbalimbali. Yaweza kuwa njia mbaya, makorongo, mlima au mteremko mkali pasina uhimili madhubuti au hitilafu ya sehemu katika gari hilo.
 
KAMA HUMJUI MUNGU DUNIA ITAKUTESA!

Kwa Kanumba yule nimjuaye mimi. Na Lulu yule ninayemfahamu. Doooh! Ningekuwa Jaji wa kesi ya Lulu, ningekuwa nasikiliza kesi kama simulizi fulani ya mapenzi ili kuongeza ufahamu wa visa vya walimwengu.

Hata hivyo, mwisho kabisa wakati wa kutoa hukumu ningemwachia Lulu huru bila kuzingatia ni ushahidi kiasi gani unamtia hatiani.

Kwa ka-Lulu kale na li-Kanumba lile. Aisee, nini kumdondosha chini, hata kumtikisa apepesuke Lulu asingeweza, acha kuanguka na kifo juu.

Ukiliangalia li-Kanumba lile na ukakaangalia ka-Lulu kale, unajua tu kuwa siku ziliwadia. Na zikifika ni Mungu tu anayejua.

Ni hapo ndipo ubabe wa Mungu unapoonekana. Ka-Lulu kale kamekuwa sababu ya kifo cha li-Kanumba lile bila silaha. Halafu miuaji ile mizezeta na mi-SMG yao na risasi zao 40, imeshindwa kumuua Lissu ambaye hakuwa amevaa bulletproof.

Kama humjui Mungu hii dunia itakutesa sana.

Ndimi Luqman MALOTO
Mkuu umesahau kuwa Daudi alimuua Goliati
 
Kwa bahati mbaya sheria huwa haiangalii Mungu anasemaje ila inangalia Katiba inasemaje!
 
Back
Top Bottom