Kuhusu kuanzisha Jamii forum sports FC

Mtundu wa Tech

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Posts
642
Reaction score
609
Salaam wakuu!
Nina wazo hapa, hivi founder na moderators hamuwezi kuanzisha Jamii forum sport FC ambayo tunaweza alika team yoyote na tukakiwasha hata mara moja kwa mwaka ikaanzishwa Jamii forum bonanza.

Kisha baadhi yetu humu wakachaguana kisha tukasakata kabumbu ka miguu, netball, basketball, volleyball, mbio, kuogelea, n.k

Huu ni ushauri wangu tu na kama ipo basi naomba mwenye wasaa anifafanulie ili nifahamu.

JF Bonanza ni muhimu na itapendeza tutaweza kufahamiana wengi tu humu bila kikwazo hata hapa Dar pale Kijitonyama ground tunaweza sakaka kabumbu na wale wenye biashara zao wanaweza wakafika hapo kuuza ni fursa maridhawa hii.

Nawasilisha wenu Mtundu wa Tech
 
Wengine tupo Champions League huko, unataka tukacheze na kina ukikaidi utapigwa2 wenye miguu miwili ya kushoto.
 
. Kufahamiana ni kuharibu jamii forum
 
Haya, yetu macho
 
Maoni yako hayatekelezeki ....yabakie maoni tu na tuishi...

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
. Kufahamiana ni kuharibu jamii forum
Mkuu humu majina yetu yapo kicode codes sasa hata tukifahamiana hakuna haja ya kuelezana majina tunayotumia humu.

Siku tukionana kila mmoja ana uhuru wa kutumia jina analopenda hata kama utataja real name kwa majina ya humu yatabaki humu humu
 
Mkuu humu majina yetu yapo kicode codes sasa hata tukifahamiana hakuna haja ya kuelezana majina tunayotumia humu.

Siku tukionana kila mmoja ana uhuru wa kutumia jina analopenda hata kama utataja real name kwa majina ya humu yatabaki humu humu

Nimekusoma, lakini ku ratibu haya na namba za simu na mawasiliano? Ni jambo jema, ila utekelezaji kwa kuficha profile ni ngumu kidogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…