Salaam wakuu!
Nina wazo hapa, hivi founder na moderators hamuwezi kuanzisha Jamii forum sport FC ambayo tunaweza alika team yoyote na tukakiwasha hata mara moja kwa mwaka ikaanzishwa Jamii forum bonanza.
Kisha baadhi yetu humu wakachaguana kisha tukasakata kabumbu ka miguu, netball, basketball, volleyball, mbio, kuogelea, n.k
Huu ni ushauri wangu tu na kama ipo basi naomba mwenye wasaa anifafanulie ili nifahamu.
JF Bonanza ni muhimu na itapendeza tutaweza kufahamiana wengi tu humu bila kikwazo hata hapa Dar pale Kijitonyama ground tunaweza sakaka kabumbu na wale wenye biashara zao wanaweza wakafika hapo kuuza ni fursa maridhawa hii.
Nawasilisha wenu Mtundu wa Tech