Pre GE2025 Kuhusu kupokea fedha za Abdul, kutoka kwa Lissu kuna ukweli kidogo na uongo mwingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Manyanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
16,464
Reaction score
35,629
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, alishusha tuhuma kuhusu mtu anayeitwa Abdul, mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwenda nyumbani kwake kumhonga.

Alizungumza kwa mara ya kwanza Iringa Mei 2024 kwenye mkutano wa hadhara. Aliendelea kurejea maneno hayo katika mikutano mingine. Nchi nzima inajua kuwa Lissu alifuatwa kuhongwa fedha na Abdul, akakataa.

Ambacho hakijawahi kusemwa ni kuwa hongo ambayo alitakiwa kupewa lengo lilikuwa nini. Lissu, alishusha tuhuma hizo kipindi ambacho maneno kuwa viongozi wa Chadema “wamelambishwa asali”, yamechukuwa nafasi tangu chama hicho kilipofanya maridhiano ya kisiasa na CCM mwaka 2022.

Mtuhumiwa mkuu wa kulamba asali ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Januari 21, 2023, Mbowe akiwa kwenye mkutano wa hadhara, viwanja vya Furahisha, Mwanza, alitetea maridhiano na kueleza kuwa kuna wenzao ndani ya chama hawaungi mkono.

Yupo mtu angeweza kuunganisha alama na kupata majibu kuwa Lissu aliposema alifuatwa na Abdul kuhongwa, akakataa, alitaka kufikisha ujumbe kuwa yeye siyo kama wengine wanaohongeka. Hafanani na “walamba asali”. Ukifika hapo, jina la Mbowe halipo mbali.

Kilichomponza Mbowe ni kuunga mkono maridhiano. Akayavaa kama beji ya heshima. Maridhiano yalifungua milango na madirisha, hivyo kuruhusu hewa mpya kuingia. Kesi za kisiasa zote zilifutwa, mikutano ya hadhara ilifunguliwa, waliokuwa wamekimbia nchi, walirejea. Unawezaje kumsimanga?

Wengi wanasahau. Mbowe alikaa jela miezi saba, kabla ya kuachiwa, hivyo kufungua milango ya maridhiano. Mbowe, alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi. Alikamatwa Julai 21, 2021 na kuachiwa huru Machi 4, 2022. Je, alilamba asali ili aachiwe huru na kuunga mkono maridhiano?

Nani hakumbuki? Maridhiano yalifanyika wakati wa uongozi wa Rais Samia. Kabla yake, Ikulu alikuwepo Dk John Magufuli, ambaye hakutaka kutazamana na wapinzani wake wa kisiasa kwa tabasamu. Kesi nyingi za kisiasa, mazingira ya kufanya siasa yalifunikwa na giza, wanasiasa walikimbia nchi. Nani wa kubeza maridhiano?

Turejee kwenye fedha za Abdul. Lissu alisema kulikuwa na jaribio la kumhonga. Yupo mtu hakumtaja, ama alimweka kiporo au alimhifadhi kwa sababu zake. Mbio za uenyekiti Chadema zikafanya Lissu amtaje. Ni Ezekia Wenje, Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Ziwa.

Nilimsikia Lissu akisema: “Aliyemleta Abdul nyumbani kwangu aje kunihonga, ametangaza kugombea umakamu mwenyekiti na amesema kwa maneno yake mwenyewe anaamuunga mkono Mwenyekiti (Mbowe).” Mtajwa ni Wenje.

Neno “afterthought”, hutumiwa sana na wanasheria kwenye mijadala ya kisheria. Lissu ni mwanasheria. Ni kwa nini siku zote Lissu alilihifadhi jina la Wenje? Je, alikaa nalo kama kifungo ili Wenje asiende kinyume naye? Walikuwa na makubaliano ambayo Wenje ameyakiuka? Hakuwa na mpango wa kumtaja ila amekasirika kuona Wenje anamuunga mkono Mbowe dhidi ya yake?

Hutakuwa mbali na ukweli endapo utasema Lissu kumtaja Wenje ni afterthought, yaani fikra zilizofuata baada ya kuona anamuunga mkono Mbowe, ambaye anashindana naye katika mbio za uenyekiti wa Chadema. Yupo anayeamini leo kuwa Wenje na Lissu wana mengi, wakibanwa, wataeleza.

Nilimsikia Wenje akijibu tuhuma dhidi yake. Kwanza hakukataa, isipokuwa amefafanua ukweli upande wake ambao anadai unapindishwa na Lissu. Ukimsikiliza Wenje, unapata jibu moja; hakukuwa na kuhongwa. Habari ya hongo ni tungo nje ya uhalisia.

Wenje anasema kuwa alikutana na Abdul kama bahati kwenye shughuli moja, na baada ya utambulisho, moja kwa moja alimhoji: “Kwa nini Serikali ya mama yako haitaki kumlipa Lissu fedha zake za matibabu?” Lissu alishambuliwa kwa risasi nyingi Septemba 7, 2017.

Ni tukio baya kwa kipimo chochote. Ajabu, uliibuka mvutano wa fedha za matibabu ya Lissu. Sera ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), inaelekeza rufaa ya matibabu kwenda nje ya nchi kutolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Lissu alishambuliwa kwa risasi Dodoma, akapelekwa Hospitali ya Mkoa ya Dodoma. Kisha, akasafirishwa kwa ndege ya kukodi hadi Hospitali ya Aga Khan, Nairobi, Kenya. Hakupita Muhimbili.

Sababu za kutompitishia Lissu Muhimbili zilikuwa zinajitosheleza kabisa. Alishambuliwa, waliomshambulia hawakuwa wamepatikana. Nadharia zilikuwa nyingi. Hofu kuwa waliotaka kumuua wangeweza kumfuata Muhimbili, ndiyo ilisababisha apelekwe Nairobi.

Msimamo wa Serikali haukubadilika. Kwa kutambua kuwa Lissu alihitaji matibabu na hakuwa na bima, iliitishwa michango nchi nzima hadi diaspora. Mwitikio ulikuwa mkubwa. Tatizo ni moja, ulikosekana uwazi wa michango ya matibabu ya Lissu. Ukiacha Sh200 milioni zilizotangazwa na Mbowe Septemba 23, 2017, hakuna taarifa nyingine.

Zaidi, Watanzania hawakuwahi kuambiwa kama fedha walizochanga, zilitosha kugharamia matibabu ya Lissu au kinyume chake. Hivyo, inaleta ukakasi kuona Serikali bado inadaiwa fedha za matibabu ya Lissu. Je, tafsiri ya ile michango ni ipi? Lissu anataka apewe fedha za matibabu ambayo ameshalipiwa na Watanzania? Zingatia, hata Serikali ikilipa ni fedha za Watanzania.

Tusiondoke kwa Wenje; kwa nini alianzisha mada ya fedha za matibabu ya Lissu baada ya kutambulishwa kwa Abdul? Je, Lissu amewahi kumtuma au alijituma mwenyewe? Nilimsikia Wenje akisema fedha za matibabu ya Lissu zinamhusu kwa sababu naye kuna za kwake. Lissu alichangiwa, ina maana Wenje anataka kurudishiwa fedha alizomchangia Lissu kwa ajili ya matibabu?

Wenje anasema Abdul ni muungwana sana, maana alikubali kuongozana naye mpaka Tegeta, nyumbani kwa Lissu. Naunga mkono. Abdul ni muungwana, maana alipaswa kushangaa suala la matibabu ya Lissu kupelekewa yeye ambaye siyo waziri wa afya, katibu mkuu wa wizara hiyo wala mkurugenzi mkuu wa NHIF.

Mtu mmoja Kariakoo kwenye kijiwe cha kahawa, alisema: “Nashindwa nimwamini yupi, Lissu au Wenje?” Jibu langu ni kuwa mkweli ni yule anayezungumza taarifa na siyo fumbo. Wenje, ama kwa ukweli au kumsingizia Lissu, alichokizungumza ni taarifa (statement). Lissu, hoja yake ilikaa kwenye mabano. Ilihitaji kufumbuliwa. Ndiyo maana anavyofumbua inabeba tafsiri ya afterthought.

Swali la jumla ni je, nani anamsingizia mwenzake? Lissu kaamua kumsingizia Wenje kwa sababu ametofautiana naye katika uchaguzi ndani ya chama? Hata hivyo tuhuma za jaribio la kuhongwa alizitoa kabla ya moto wa uchaguzi ndani ya Chadema. Wenje amechagua kumkaanga Lissu ili kujinasua na kashfa? Wazungu husema “time heals all boo-boos” – “muda hutibu majeraha yote.” Tuwape muda.

Nilitazama mahojiano ya Lissu kwenye kituo cha Star TV. Nilimwona na nikamsikia Lissu akisema alifuatwa na “mwana malkia”, huyo “mwana malkia”, aliahidi kumsaidia kupata fedha za matibabu. Lissu akasema: “Nilimwambia yule mwana-malkia, ukinisaidia kupata hizi fedha utakuwa rafiki yangu.”

Rejea mkutano wa hadhara, Singida Juni 8, 2024, Lissu alisema: “Namfahamu mtoto wake mmoja anaitwa Abdul. Aliniletea rushwa nyumbani kwangu, nikamwambia shenzi. Kahonge wanaohongeka.”

Upande mmoja, Lissu anasema, alimwambia Abdul kuwa angemsaidia kupata fedha za matibabu, wangekuwa marafiki. Upande mwingine, Lissu anasema, alimfukuza, akamwambia ‘shenzi’. Lissu yupi mkweli?

Katika mahojiano Star TV, Lissu alisema “watu wema” ndiyo walimpeleka Abdul nyumbani kwake. Alikataa kuwataja hao watu wema. Baada ya Wenje kutangaza kumuunga mkono Mbowe, Lissu hakungoja kuulizwa, alimtaja moja kwa moja.

Kuna mwana-Chadema kutoka Magu, Mwanza, aliniandikia ujumbe unaosema: “Nahisi Lissu na Wenje walikuwa na makubaliano yao, wamegeukana, sasa wanatajana. Upo ukweli zaidi wa kuuchimba ndani ya vifua vyao. Wanachikitoa sasa kina uongo mwingi kuliko ukweli kwa sababu wanakomoana.”

Credit: Luqman MALOTO
 
Lissu hakukataa hongo.

Alikataa hongo ya pesa akakubali hongo ya fadhila ya Abdul kumsaidia apate mafao yake.

Kwa maneno yake mwenyewe.

That was influence peddling.

Lissu should do better than that.
 
Umechambua vizuri na critically, ndivyo jf ilipaswa kuwa .

Kama ulivyosema kuna kitu zaidi lati ya Wenje na Lissu kilichowafarakanisha ambacho umma haukijui bado ila ipo siku tutakuelewa.

Pia ipo haja,matibabu yote ya Lissu gharama zake ziwekwe wazi na vyanzo vya hizo gharana kwa maana pesa,iliyolipwa na makundi mbalimbali ichanganuliwe ili tujue kati ya hizo Lissu anadai nini, je anataka double payment? Maana hata mimi nilimchangia kupitia akaunti ya CRDB tuliyopewa.
 
Yaani mnara wa babeli unanaguka bila mapambio
 
kuhusu hizo zinazoitwa fedha za matibabu sijawahi kuelewa na mimi siyo mwanasheria, swali langu, ni je, kutibiwa kwa “viongozi” nje ya nchi ni hisani na huruma tu ya serikali au liko kisheria kwamba kuna sheria iliyowekwa inayosema “viongozi” watalipiwa matibabu nje ya nchi? na kama ni sheria kwa nini tundu lisu asiishitaki serikali mahakamani kudai haki zake za matibabu? kwa nini asianzie hapo kwanza?
 
Maneno mengi pumba tupu. Wanasema kuna rekodi ya hicho kikao cha Lissu kuthibitisha madai yake, kwanini hawataki kuitoa hiyo rekodi tujionee wenyewe nani ni mkweli na nani ni muongo
 
Kati ya kauli ya Abdul ya kumfanikishia LISSU stahiki zake na kauli ya kumhonga ni ipi ilianza kumtoka Abdul?
 
Hongo ya fadhira ambayo ni haki yake
Naam.

Tufikirie kidhahania.

Muandishi wa habari ukienda kudai haki yako ofisi ya mafao yenye mstari mrefu kwa karani, ukaambiwa na meneja kuwa uache kumuandika vibaya, atakupa hela, ukakataa hela, ila ukasema akusaidie upate fadhila uruke mstari mrefu ili upate mafao yako haraka bila kufuata mstari, hapo hata kama unapata mafao ambayo ni haki yako, ukitumia fadhila ya kuruka mstari inayokupa unfair advantage, hiyo fadhila ni kinyume cha maadili. Ni influence peddling. Ni rushwa.

Lissu namkubali kwenye mengi, moja ya jambo alilosema alitaka watu wam challenge, wamfanyie constructive criticism iki aweze kujifunza mengi na kufanya vizuri zaidi.

Hapa alipotaka kufanya influence peddling ni kitu kibaya, angeweza kufanya vizuri zaidi.

Lissu alitakiwa kukataa pesa za Abdul na kukataa fadhila yoyote. Fadhila nayo ni hongo, hata kama ni fadhila katika kupata haki yako.

Hii hapa ni definition ya influence peddling.

Influence peddling - the use of position or political influence on someone's behalf in exchange for money or favors.
 
Usichoelewa Nini hapo bandiko refu bila pointing

Lissu alitaka hela yake halali asaidiwe kulipwa

Sasa huyu Abdul na wenje walienda na gear ya kumpatia fedha nje ya malipo yake ili anyamaze aache kumsema vibaya mama ambayo lissu anasema ni rishwa

Baada ya kuona mpangango wao umejulikana ndo wameanza kudai walienda kumsaidia kulipwa stahiki zake ambao ni uongo

Nikusaidie tu Kijana simple critical analysis, mkweli ni yule aliyejitokeza wa kwanza kwenye public

Na muongon ni yule aliyekuja wa pili na maelezo yasiyo eleweka
 
kuhusu hizo zinazoitwa fedha za matibabu sijawahi kuelewa na mimi siyo mwanasheria, swali langu, ni je, kutibiwa kwa “viongozi” nje ya nchi ni hisani na huruma tu ya serikali au liko kisheria kwamba kuna sheria iliyowekwa inayosema kwamba “viongozi” watalipiwa matibabu nje ya nchi? na kama ni sheria kwa nini tundu lisu asiishitaki serikali mahakamani kudai haki zake za matibabu? kwa nini asianzie hapo kwanza?
Pumba, nonsense. Haijalisha kiogozi anatibiwa ndani au nje sheria inasema gharama ya matibabu kwa wabunge na viongozi wa serikali itagharamiwa na seeikali. Tz mahakama zimeingiliwa na muhimili mkuu, majaji wanatii amli kutoka juu

Majaji ni wateule wa rais na hawawezi kumkaraisha
 
Umechambua vizuri na critically, ndivyo jf ilipaswa kuwa .

Kama ulivyosema kuna kitu zaidi lati ya Wenje na Lissu kilichowafarakanisha ambacho umma haukijui bado ila ipo siku tutakuelewa.

Pia ipo haja,matibabu yote ya Lissu gharama zake ziwekwe wazi na vyanzo vya hizo gharana kwa maana pesa,iliyolipwa na makundi mbalimbali ichanganuliwe ili tujue kati ya hizo Lissu anadai nini, je anataka double payment? Maana hata mimi nilimchangia kupitia akaunti ya CRDB tuliyopewa.
Kuna sehemu Lissu amesema ana kudai?
 
1. ANAZUNGUMZA KWA MAFUMBO. Kuna mtu alisema ni mbinu ya siasa ambapo hutakiwi kuchomoa silaha zote pwaaa! kwa wakati mmoja. Hii ni mbinu nzuri ya kumchanganya mpinzani wako.

2. WAZO LA BAADAYE (HAKUWA NA LENGO LA KUMUUMBUA WENJE): Kwa sababu huenda alijua angemuunga mkono kwenye azma yake ya mabadiliko chamani, na ndipo ghafla bin vuu akaona jamaa anakuja kumvaa kwenye nafasi yake ileile ya umakamo mwenyekiti. Si na yeye akaamua kuwachenjia!

3. WALIKUWA NA MAKUBALIANO, ILA WAMEGEUKANA: Lakini hii haiondoi msingi wa hoja kuhusu harufu ya hongo kutoka kwa mtu anayetajwa kama kibosire.

4. UKIMSIKILIZA WENJE (MTU MMOJA KARIAKOO ALINIAMBIA...): Sasa hapo umeamua ukweli wako utokanane na Wenje au ^mtu wa Kariakoo!^ Hakuna ukweli hapo, bali ni hisia tu.

5. MTU MKWELI HAONGEI KWA MAFUMBO: Seriously? Kwa hiyo JK fundi wa kurusha mafundo na mafumbo mepesi, madogo, saizi ya kati, makubwa na tata kila siku majukwaani, unamchukuliaje kwa mfano?
 
Back
Top Bottom