Pre GE2025 Kuhusu kupokea fedha za Abdul, kutoka kwa Lissu kuna ukweli kidogo na uongo mwingi

Pre GE2025 Kuhusu kupokea fedha za Abdul, kutoka kwa Lissu kuna ukweli kidogo na uongo mwingi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Naam.

Tufikirie kidhahania.

Muandishi wa habari ukienda kudai haki yako ofisi ya mafao yenye mstari mrefu kwa karani, ukaambiwa na meneja kuwa uache kumuandika vibaya, atakupa hela, ukakataa hela, ila ukasema akusaidie upate fadhila uruke mstari mrefu ili upate mafao yako haraka bila kufuata mstari, hapo hata kama unapata mafao ambayo ni haki yako, ukitumia fadhila ya kuruka mstari inayokupa unfair advantage, hiyo fadhila ni kinyume cha maadili. Ni influence peddling. Ni rushwa.

Lissu namkubali kwenye mengi, moja ya jambo alilosema alitaka watu wam challenge, wamfanyie constructive criticism iki aweze kujifunza mengi na kufanya vizuri zaidi.

Hapa alipotaka kufanya influence peddling ni kitu kibaya, angeweza kufanya vizuri zaidi.

Lissu alitakiwa kukataa pesa za Abdul na kukataa fadhila yoyote. Fadhila nayo ni hongo, hata kama ni fadhila katika kupata haki yako.

Hii hapa ni definition ya influence peddling.

Influence peddling - the use of position or political influence on someone's behalf in exchange for money or favors.
Unatafuta poli la kujitekenya lakini hamta toboa na hoja dhaifu za kipumbafu. Nonsense
 
Pumba, nonsense. Haijalisha kiogozi anatibiwa ndani au nje sheria inasema gharama ya matibabu kwa wabunge na viongozi wa serikali itagharamiwa na seeikali. Tz mahakama zimeingiliwa na muhimili mkuu, majaji wanatii amli kutoka juu

sawa asante kwa kunifahamisha kwamba kuna sheria kwamba “viongozi” watagharamiwa matibabu ndani na nje ya nchi na serikali, sasa ni kwa nini tundu lisu asishitaki kama hiyo sheria ipo? alishawahi kufanya hivyo (kushitaki mahakamani) labda nilipitwa?
 
TUNDU Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Tanzania Bara, alishusha tuhuma kuhusu mtu anayeitwa Abdul, mtoto wa Rais Samia Suluhu Hassan, kwenda nyumbani kwake kumhonga.

Alizungumza kwa mara ya kwanza Iringa Mei 2024 kwenye mkutano wa hadhara. Aliendelea kurejea maneno hayo katika mikutano mingine. Nchi nzima inajua kuwa Lissu alifuatwa kuhongwa fedha na Abdul, akakataa.

Ambacho hakijawahi kusemwa ni kuwa hongo ambayo alitakiwa kupewa lengo lilikuwa nini. Lissu, alishusha tuhuma hizo kipindi ambacho maneno kuwa viongozi wa Chadema “wamelambishwa asali”, yamechukuwa nafasi tangu chama hicho kilipofanya maridhiano ya kisiasa na CCM mwaka 2022.

Mtuhumiwa mkuu wa kulamba asali ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe. Januari 21, 2023, Mbowe akiwa kwenye mkutano wa hadhara, viwanja vya Furahisha, Mwanza, alitetea maridhiano na kueleza kuwa kuna wenzao ndani ya chama hawaungi mkono.

Yupo mtu angeweza kuunganisha alama na kupata majibu kuwa Lissu aliposema alifuatwa na Abdul kuhongwa, akakataa, alitaka kufikisha ujumbe kuwa yeye siyo kama wengine wanaohongeka. Hafanani na “walamba asali”. Ukifika hapo, jina la Mbowe halipo mbali.

Kilichomponza Mbowe ni kuunga mkono maridhiano. Akayavaa kama beji ya heshima. Maridhiano yalifungua milango na madirisha, hivyo kuruhusu hewa mpya kuingia. Kesi za kisiasa zote zilifutwa, mikutano ya hadhara ilifunguliwa, waliokuwa wamekimbia nchi, walirejea. Unawezaje kumsimanga?

Wengi wanasahau. Mbowe alikaa jela miezi saba, kabla ya kuachiwa, hivyo kufungua milango ya maridhiano. Mbowe, alikuwa akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi. Alikamatwa Julai 21, 2021 na kuachiwa huru Machi 4, 2022. Je, alilamba asali ili aachiwe huru na kuunga mkono maridhiano?

Nani hakumbuki? Maridhiano yalifanyika wakati wa uongozi wa Rais Samia. Kabla yake, Ikulu alikuwepo Dk John Magufuli, ambaye hakutaka kutazamana na wapinzani wake wa kisiasa kwa tabasamu. Kesi nyingi za kisiasa, mazingira ya kufanya siasa yalifunikwa na giza, wanasiasa walikimbia nchi. Nani wa kubeza maridhiano?

Turejee kwenye fedha za Abdul. Lissu alisema kulikuwa na jaribio la kumhonga. Yupo mtu hakumtaja, ama alimweka kiporo au alimhifadhi kwa sababu zake. Mbio za uenyekiti Chadema zikafanya Lissu amtaje. Ni Ezekia Wenje, Mwenyekiti wa Chadema, Kanda ya Ziwa.

Nilimsikia Lissu akisema: “Aliyemleta Abdul nyumbani kwangu aje kunihonga, ametangaza kugombea umakamu mwenyekiti na amesema kwa maneno yake mwenyewe anaamuunga mkono Mwenyekiti (Mbowe).” Mtajwa ni Wenje.

Neno “afterthought”, hutumiwa sana na wanasheria kwenye mijadala ya kisheria. Lissu ni mwanasheria. Ni kwa nini siku zote Lissu alilihifadhi jina la Wenje? Je, alikaa nalo kama kifungo ili Wenje asiende kinyume naye? Walikuwa na makubaliano ambayo Wenje ameyakiuka? Hakuwa na mpango wa kumtaja ila amekasirika kuona Wenje anamuunga mkono Mbowe dhidi ya yake?

Hutakuwa mbali na ukweli endapo utasema Lissu kumtaja Wenje ni afterthought, yaani fikra zilizofuata baada ya kuona anamuunga mkono Mbowe, ambaye anashindana naye katika mbio za uenyekiti wa Chadema. Yupo anayeamini leo kuwa Wenje na Lissu wana mengi, wakibanwa, wataeleza.

Nilimsikia Wenje akijibu tuhuma dhidi yake. Kwanza hakukataa, isipokuwa amefafanua ukweli upande wake ambao anadai unapindishwa na Lissu. Ukimsikiliza Wenje, unapata jibu moja; hakukuwa na kuhongwa. Habari ya hongo ni tungo nje ya uhalisia.

Wenje anasema kuwa alikutana na Abdul kama bahati kwenye shughuli moja, na baada ya utambulisho, moja kwa moja alimhoji: “Kwa nini Serikali ya mama yako haitaki kumlipa Lissu fedha zake za matibabu?” Lissu alishambuliwa kwa risasi nyingi Septemba 7, 2017.

Ni tukio baya kwa kipimo chochote. Ajabu, uliibuka mvutano wa fedha za matibabu ya Lissu. Sera ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), inaelekeza rufaa ya matibabu kwenda nje ya nchi kutolewa na Hospitali ya Taifa Muhimbili. Lissu alishambuliwa kwa risasi Dodoma, akapelekwa Hospitali ya Mkoa ya Dodoma. Kisha, akasafirishwa kwa ndege ya kukodi hadi Hospitali ya Aga Khan, Nairobi, Kenya. Hakupita Muhimbili.

Sababu za kutompitishia Lissu Muhimbili zilikuwa zinajitosheleza kabisa. Alishambuliwa, waliomshambulia hawakuwa wamepatikana. Nadharia zilikuwa nyingi. Hofu kuwa waliotaka kumuua wangeweza kumfuata Muhimbili, ndiyo ilisababisha apelekwe Nairobi.

Msimamo wa Serikali haukubadilika. Kwa kutambua kuwa Lissu alihitaji matibabu na hakuwa na bima, iliitishwa michango nchi nzima hadi diaspora. Mwitikio ulikuwa mkubwa. Tatizo ni moja, ulikosekana uwazi wa michango ya matibabu ya Lissu. Ukiacha Sh200 milioni zilizotangazwa na Mbowe Septemba 23, 2017, hakuna taarifa nyingine.

Zaidi, Watanzania hawakuwahi kuambiwa kama fedha walizochanga, zilitosha kugharamia matibabu ya Lissu au kinyume chake. Hivyo, inaleta ukakasi kuona Serikali bado inadaiwa fedha za matibabu ya Lissu. Je, tafsiri ya ile michango ni ipi? Lissu anataka apewe fedha za matibabu ambayo ameshalipiwa na Watanzania? Zingatia, hata Serikali ikilipa ni fedha za Watanzania.

Tusiondoke kwa Wenje; kwa nini alianzisha mada ya fedha za matibabu ya Lissu baada ya kutambulishwa kwa Abdul? Je, Lissu amewahi kumtuma au alijituma mwenyewe? Nilimsikia Wenje akisema fedha za matibabu ya Lissu zinamhusu kwa sababu naye kuna za kwake. Lissu alichangiwa, ina maana Wenje anataka kurudishiwa fedha alizomchangia Lissu kwa ajili ya matibabu?

Wenje anasema Abdul ni muungwana sana, maana alikubali kuongozana naye mpaka Tegeta, nyumbani kwa Lissu. Naunga mkono. Abdul ni muungwana, maana alipaswa kushangaa suala la matibabu ya Lissu kupelekewa yeye ambaye siyo waziri wa afya, katibu mkuu wa wizara hiyo wala mkurugenzi mkuu wa NHIF.

Mtu mmoja Kariakoo kwenye kijiwe cha kahawa, alisema: “Nashindwa nimwamini yupi, Lissu au Wenje?” Jibu langu ni kuwa mkweli ni yule anayezungumza taarifa na siyo fumbo. Wenje, ama kwa ukweli au kumsingizia Lissu, alichokizungumza ni taarifa (statement). Lissu, hoja yake ilikaa kwenye mabano. Ilihitaji kufumbuliwa. Ndiyo maana anavyofumbua inabeba tafsiri ya afterthought.

Swali la jumla ni je, nani anamsingizia mwenzake? Lissu kaamua kumsingizia Wenje kwa sababu ametofautiana naye katika uchaguzi ndani ya chama? Hata hivyo tuhuma za jaribio la kuhongwa alizitoa kabla ya moto wa uchaguzi ndani ya Chadema. Wenje amechagua kumkaanga Lissu ili kujinasua na kashfa? Wazungu husema “time heals all boo-boos” – “muda hutibu majeraha yote.” Tuwape muda.

Nilitazama mahojiano ya Lissu kwenye kituo cha Star TV. Nilimwona na nikamsikia Lissu akisema alifuatwa na “mwana malkia”, huyo “mwana malkia”, aliahidi kumsaidia kupata fedha za matibabu. Lissu akasema: “Nilimwambia yule mwana-malkia, ukinisaidia kupata hizi fedha utakuwa rafiki yangu.”

Rejea mkutano wa hadhara, Singida Juni 8, 2024, Lissu alisema: “Namfahamu mtoto wake mmoja anaitwa Abdul. Aliniletea rushwa nyumbani kwangu, nikamwambia shenzi. Kahonge wanaohongeka.”

Upande mmoja, Lissu anasema, alimwambia Abdul kuwa angemsaidia kupata fedha za matibabu, wangekuwa marafiki. Upande mwingine, Lissu anasema, alimfukuza, akamwambia ‘shenzi’. Lissu yupi mkweli?

Katika mahojiano Star TV, Lissu alisema “watu wema” ndiyo walimpeleka Abdul nyumbani kwake. Alikataa kuwataja hao watu wema. Baada ya Wenje kutangaza kumuunga mkono Mbowe, Lissu hakungoja kuulizwa, alimtaja moja kwa moja.

Kuna mwana-Chadema kutoka Magu, Mwanza, aliniandikia ujumbe unaosema: “Nahisi Lissu na Wenje walikuwa na makubaliano yao, wamegeukana, sasa wanatajana. Upo ukweli zaidi wa kuuchimba ndani ya vifua vyao. Wanachikitoa sasa kina uongo mwingi kuliko ukweli kwa sababu wanakomoana.”

Credit: Luqman MALOTO
Nonsense
 
kuhusu hizo zinazoitwa fedha za matibabu sijawahi kuelewa na mimi siyo mwanasheria, swali langu, ni je, kutibiwa kwa “viongozi” nje ya nchi ni hisani na huruma tu ya serikali au liko kisheria kwamba kuna sheria iliyowekwa inayosema kwamba “viongozi” watalipiwa matibabu nje ya nchi? na kama ni sheria kwa nini tundu lisu asiishitaki serikali mahakamani kudai haki zake za matibabu? kwa nini asianzie hapo kwanza?
Ni sheria.

Kuna njia nyingi za kupata haki moja ni ya kushitaki, lakini pia kuna njia ya kufanya kazi pamoja na serikali. Kudai kulipwa kwenye mfumo wa serikali bila kushitaki.

Moja ya tatizo la kushitaki serikali Tanzania ni kuwa unatengeneza uhasama na serikali na mahakama inaweza kupewa amri kutoka juu iamue vipi.

Tundu Lissu katika hili ameamua kufanya kazi na serikali, amepeleka documents zake wizarani.

Ila naona tatizo ametaka pia kumtumia Abdul ili apate haki yake, this is influence peddling, it is unethical, unfair and a blot on Lissu's reputation especially because he has distinguished himself as someone who stands for fairness and justice.
 
KWA NINI MBOWE HATAKI KUACHIA UENYEKITI WA CHADEMA

Mbowe ni Mwanachama pekee asiye na hasara ndani ya CHADEMA na mnufaika Mkuu japo wengi hawaoni kwa macho ya kawaida na anatumia mbinu zifuatazo;

1. Pesa yake yoyote ile anayoitumia ndani ya CHAMA inaandikwa kama mkopo na CHAMA kikipata fedha kwa njia ama ya Ruzuku, Chadema Digital ama Join the Chain analipwa kama mfadhiri wa chama.

Kama Mbowe yeye kila pesa yake anayoitumia ndani ya CHADEMA analipwa kama deni na anaitwa mfadhiri wa chama; sisi wengine anaotuita wabangaizaji ni nani anatulipa hizo chenji zetu za jero jero ambazo tunaamua kushinda ama kulala njaa ili tuki-support chama?

Hakika haya ni mambo ya aibu sana yasiyovumilika kwa kila mpenda mabadiliko wa nchi hii.

2. Mbowe ndiye Mwanachama pekee wa CHADEMA ama wa upinzani kwa sasa anayeweza kuipinga Serikali ya CCM hadharani; na ASITEKWE wala kuumizwa mwili wake hata kwa rungu ama jiwe na dola hii ya CCM ama huyu Mbowe hajawahi kupata athari yoyote ile kutokana na kukaa kwake gerezani kwa sababu; Mbowe akipelekwa gerezani inakuwa fursa ya kuweka sawa mipango yao na watu wa dola na mipango ikishakaa sawa anatolewa na anaambiwa aandike hasara zake zote alipwe na serikali na kweli analipwa.

Kama ni uongo, Mbowe atoke hadharani akatae kama hajalipwa Mabillioni ya Shilingi na Serikali ya CCM kama fidia ya hasara za kisiasa. Haya yote ni yanatokea hivi kwa sababu; Mbowe ni; mwenzao tangu enzi japo tulipoteza muda wetu mwingi sana kumuamini pasipo kujua.

Tazama Tundu Lissu anavyohangaika kudai hata hayo madai yake ya halali aliyotibiwa kama Mbunge baada ya kumuumiza vibaya sana kwa risasi za moto.

Kwamba, wapo tayari kumhonga Lissu Mabillioni ya Shilingi kupitia kwa Wenje na Abdul, lakini hawako tayari kumlipa gharama zake za matibabu ambazo ni halali yake kwa mujibu wa sheria za nchi.

3. Mbowe ni Mwanachama pekee ndani ya CHADEMA ambaye hajawahi kuishi nje ya nchi kama MKIMBIZI kutokana na usalama wake kuwa hatarini wala familia yake haijawahi kupata msukosuko kama ambavyo tunaona kwa wapinzani wa kweli walio committed kutaka CCM iondoke madarakani kama akina Godbless Lema na huyu Tundu Lissu.

Unahisi ni kwa nini Mbowe na familia yake hawajawahi kupata msukosuko serious wa kuwalazimu kuikimbia nchi ili hali na yeye anaikisoa serikali? Jibu liko Behind the Scene. Tuendelee kunywa mchuzi, nyama ziko chini.

Garatwa Francis,
Sauti ya wasio na Sauti.
29 Desemba, 2024.
 
huna akili kabisa, mwite upya mumeo wenje ajitokeze aseme LISu anamdai shingapi kwasababu wenje alimpeleka abduli ili aone anavyopewa Hela ili walipane madai

LISu kakataa hadaiwi chochote na wenje
Mkuu, waandishi wa habari ndio wanatuangusha. Ile siku akihojiwa, alitakiwa kuulizwa anadai kiasi gani na kwa minajili gani?

Yaani hawa jamaa hawajawahi kujifunza kitu kwa wakili wao Pita Kibatala?

Yeye akikuhoji ukasema, kwa mfano siku hiyo nilienda kwa mjomba, basi hapo hapo swali linahamia kwa mjomba na siku hiyo. Lazima achimbe hadi afikie kigota cha dunia.

Hiyo ndiyo kanuni ya mahojiano yote yenye maana.
 
sawa asante kwa kunifahamisha kwamba kuna sheria kwamba “viongozi” watagharamiwa matibabu ndani na nje ya nchi na serikali, sasa ni kwa nini tundu lisu asishitaki kama hiyo sheria ipo? alishawahi kufanya hivyo (kushitaki mahakamani) labda nilipitwa?
Rais hataki kumlipa na huko mahakamani unakotaka kwenda, unakwenda kukutana na wateule wa rais, hauoni hapo unataka kupoteza muda wako bule
 
MKOA WA MARA,MKOA WA MARA.
RUSHWA YA FEDHA INANUKIA KWA AJILI YA KUWASHAWISHI WAJUMBE WAMCHAGUA MBOWE.

Katibu Wa Mkoa wa Mara Donard mwembe Akishirikiana na m/kiti wa chama wilaya ya Rorya Nyakiriga na katibu wa jimbo la Tarime Mjini Pamba Jana Tarehe.28.12.2024 Waliwatumia kwa makundi makundi Nauli wajumbe wa mkutano mkuu Taifa kutoka kwenye majimbo mbali mbali ya mkoa wa Mara ili waende ofisi ya chama mkoa iliyopo Makao makuu ya mkoa Musoma mjini maeneo ya Nyakato kwa Saa nane,wajumbe hao walipofika waliambiwa kuwa wamuunge mkono mbowe na wampigie kura ili ashinde uchaguzi mkuu utakaofanyika Tarehe.21.01.2024 na adi Leo Tarehe.29.12.2024 ninapoandika ujumbe huu wajumbe bado wanaendelea kuitwa kwenye ofisi izo za chama mkoa wa mara.
Na kiasi cha fedha kilichotengwa kwa ajili ya kuwapa hao wajumbe ni milioni tatu.
DONARD MWEMBE
Ikumbukwe donard mwemba alishinda nafasi ya katibu wa mkoa kwa kutumia Rushwa kubwa sana naona yale yale aliyoyafanya wakati wa uchaguzi wa mkoa ndo anayafanya tena kwenye uchaguzi huu wa ngazi ya Taifa.
OFISI ZA MKOA
Ofisi zetu za chama mkoa ndo leo hii zinatumika kugawa Rushwa za uchaguzi,ofisi zimefanywa chafu zimekuwa ni pango la kutolea Rushwa, hii ni atari sana na aipaswi kufumbiwa macho.
COVID-19
Ester Bulaya na Halima mdee walipokuwa Bunda walimuita katibu wa mkoa na kumkabidhi kiasi cha Tsh.5000,000/=(milion tano)Kwa ajili ya kuhakikisha wajumbe wanaitwa na kupewa fedha ,hawa madada wanasema mbowe akishinda wanarudishwa kwenye chama ivyo wanampambania.
ZOEZI LA KUWAITA WAJUMBE
Zoezi la kuwaita wajumbe linaendelea adi sasa na wanatumia nguvu kubwa sana ya fedha kuhakikisha wanawapata wajumbe,huu uchaguzi umegubikwa na rushwa,umegubikwa na fedha za covid-19.
MKOA MARA
Mkoa wa mara umeonekana ni mkoa mgumu sana ndo maana inatumika nguvu kubwa sana ya fedha kuhakikisha wajumbe wanarubuniwa na kupewa hongo ili wabadili mawazo yao.
Hatuwezi kuwa na viongozi waliyochaguliwa kwa Rushwa pia wanagawa fedha za Rushwa kwa wajumbe ili wakamchague m/kiti kwa Rushwa.
M/KITI WA MKOA WA MARA
M/kiti wa mkoa mwl.Chacha Heche alipotaftwa kuulizwa kama ametoa baraka ofisi za chama zitumike kugawa Rushwa alisema ata yeye anamshangaa katibu wake kwa nini anafanya ivyo anakichafua chama na anafanya ivyo kwa maslahi ya nani.Mwl.chacha heche yupo nje ya nchi kwa sasa.

TUTAKULA MACHAME TUTALALA IKUNGI.

CHUKUWA PESA KURA MPIGIE LISSU
#LISSU WILL FIX IT.
#LISSU M/KITI AJAYE
#NI YEYE
Usifanye makosa Tarehe.21.01.2024
 
Ni sheria.

Kuna njia nyingi za kupata haki moja ni ya kushitaki, lakini pia kuna njia ya kufanya kazi pamoja na serikali. Kudai kulipwa kwenye mfumo wa serikali bila kushitaki.

Moja ya tatizo la kushitaki serikali Tanzania ni kuwa unatengeneza uhasama na serikali na mahakama inaweza kupewa amri kutoka juu iamue vipi.

Tundu Lissu katika hili ameamua kufanya kazi na serikali, amepeleka documents zake wizarani.

Ila naona tatizo ametaka pia kumtumia Abdul ili apate haki yake, this is influence peddling, it is unethical, unfair and a blot on Lissu's reputation especially because he has distinguished himself as someone who stands for fairness and justice.

kama ni hivyo basi serikali yetu inafanya mambo kienyeji sana, kwa maana kwangu kama layman wa sheria kama sheria ipo na haijafwata ni rahisi kushitaki halafu mahakama inatoa hukumu, ikitoa in your favor umeshinda na hapo serikali au chombo chake kitalazimishwa kukulipa ofcourse nimesimplify lkn hili swala la sijui kukutana na kumuomba mtoto wa raisi kwamba mama yake akulipe kwangu mimi limekaa “kimsaada na hisani” zaidi klk sheria na ngumu hata kujitetea hata huko nje kwa watu walio makini, anyway serikali yetu inafanya mambo kienyeji sana kama ndivyo hivyo …
 
Unatafuta poli la kujitekenya lakini hamta toboa na hoja dhaifu za kipumbafu. Nonsense
Naomba tujadili hoja, usinijadili mimi mtoa hoja.

Kumjadili mtoa hoja badala ya hoja ni ad hominem logical fallacy.

Mimi nam support Lissu. Lissu ana mazuri mengi na atasaidia sana. Ila hilo halina maana Lissu hawezi kukosea.

Lissu mwenyewe kasema anapenda watu wanapomkosoa, kwa sababu hapo ndipo anapopata nafasi ya kujirekebisha anapokosea.

Hoja ni kwamba, hata kama unadai haki yako, kutumia fadhila ya mtu aliyetaka kukuhonga pesa nayo ni rushwa, rushwa ya fadhila.

Rushwa si lazima iwe pesa, ndiyo maana kuna rushwa ya ngono.

Lissu alichofanya ni kukataa rushwa ya aina moja (pesa) na kukubali rushwa ya aina nyingine (fadhila).

Lissu kama mtu anayesimamia haki, uwazi, usawa etc, alitakiwa kusimamia kupata haki yake kwa kutumia mfumo rasmi wa kiserikali, si kwa kutumia njia za panya na connections zake za kisiasa.

Hapa kulikuwa na nafasi ya Lissu kutumia tatizo lake kutatua tatizo la kimfumo ambalo lipo kwa watu wengi. Lissu aliweza kuifanya hii issue ni cause yake ya kijamii na kusaidia maelfu ya Watanzania walio na tatizo kama lake ambao hawana connection ya kujuana na Abdul wala Samia.

Instead ametumia mwanya wa rushwa ya fadhila kujipendelea yeye mwenyewe kwenye tatizo lake bila kutatua tatizo la kijamii.

Noblesse oblige. To those who much is given, much shall be required.

Tundu Lissu is given much, trust, leadership, hope.

Much shall be required from him.
 
Mkuu, waandishi wa habari ndio wanatuangusha. Ile siku akihojiwa, alitakiwa kuulizwa anadai kiasi gani na kwa minajili gani?

Yaani hawa jamaa hawajawahi kujifunza kitu kwa wakili wao Pita Kibatala?

Yeye akikuhoji ukasema, kwa mfano siku hiyo nilienda kwa mjomba, basi hapo hapo swali linahamia kwa mjomba na siku hiyo. Lazima achimbe hadi afikie kigota cha dunia.

Hiyo ndiyo kanuni ya mahojiano yote yenye maana.
sahh
 
MITAZAMO YA MAKUNDI (8) NANE YA WATU WANAOMUUNGA MKONO MBOWE NA SABABU ZAO.

Na; Garatwa Francis

Wakati umma unaomuunga mkono Tundu Lissu ukiwaza zaidi juu ya kumpata Tundu Lissu awe M/Kiti wa CHADEMA ili Chama kiweze kuinuka tena na kutoka kwenye mifuko ya CCM na Dola yao walikokificha kwa manufaa yao. Wengine wanawaza zaidi kuhusu tumbo zao na wengine wanawaza kuhusu vyeo vya madaraka wapewe na Mbowe kama walivyozoea. Hii hapa mitazamo na fikra za watu wanaomuunga mkono Mbowe. Mitazamo hii nimeigawa katika makundi (8) manane maana hawafanani mitazamo yao kutoka kundi moja kwenda lingine.

1. Wapo wanaovizia Ubunge wa Viti Maalum wakiamini kwamba; Mbowe ndiye ALFA na OMEGA kwa Mwanamke yeyote yule kuweza kupata Ubunge wa Viti Maalum ndani ya CHADEMA. Hawa huwezi kuwaambia chochote kuhusu Mbowe wakakuelewa maana vipaumbele vyao vyote kwenye chama hiki kuanzia kipaumbele cha kwanza mpaka cha mwisho ni Ubunge wa Viti Maalum tu. Hawa hawataki kujionyesha wako upande upi hata kama hawamtaki Mbowe; wanahisi kama kuna JINI MAKATA linaweza kuwanyima Ubunge wa Viti Maalum kama wakionekana kumuunga mkono Tundu Lissu.

2. Wapo wanaopata MIGAO ya hizo fedha chafu zinazosambazwa na Mama kupitia kwa Kibanda, Balile, Wenje na Abdul. Hawa nao huwaambii kitu. Mfano mzuri sana ni huyo Boni Yai.

3. Covid 19 wanapambana usiku na mchana Mbowe ashinde ili warudi tena kuvuna mafao kwenye SACCOS ya mjomba wao. (Mfano; Mdee, Bulaya, Matiko n.k)

4. Baadhi ya Maafisa na Wakurugenzi wa Makao Makuu ya Chama wanapambana ili Mbowe arudi waendelee kukikamua chama pale Makao Makuu kwa sababu akitoka mirija yote itazibwa na Lissu na fedha zitashuka kwenda kwenye wilaya na majimbo kusaidia shughuli za ujenzi wa chama.

5. Hao CCM wao wanaamini kwamba, Mbowe akiendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA; wanaendelea kunufaika na uporaji wa chaguzi kwa sababu huyu Mbowe wa sasa ni kibogoyo asiye na meno tena ya kung'ata. CCM wanamtetea kwa maneno kwamba; CHADEMA mchagueni tena Mbowe ana hekima na busara 😂

6. Serikali ya CCM nao wanaamini Mbowe akiendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wataipata nafuu ya kupumua hasa kwenye presha ya masuala mazito kama Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi; lakini pia hoja nzito za kuibua mambo ya hovyo wanayoyafanya kwenye serikali yao.

7. Wapo ambao ni wahuni na walevi wanaopenda starehe za Bar (Mfano; Ntobi Emmanuel na Henry Kilewo na Martin Maranja). Kwa hiyo, wao Chama sio kipaumbele ila zile starehe ambazo Mbowe amewazoesha na kuwafanya wabweteke wakidhani maisha washayamaliza.

8. Wapo wanaolipa fadhira kwa Mbowe kwa sababu za kuwasaidia kushinda chaguzi za maeneo yao kutokana na matumizi ya fedha chafu kutoka CCM alizokuwa anazipigia kelele Makamu M/Kiti wa Chama Tundu Lissu kila kuitwapo leo.

Garatwa Francis,
Sauti ya wasio na Sauti.
Dar es Salaam, Tanzania.
29 Desemba, 2024.
 
Ni sheria.

Kuna njia nyingi za kupata haki moja ni ya kushitaki, lakini pia kuna njia ya kufanya kazi pamoja na serikali. Kudai kulipwa kwenye mfumo wa serikali bila kushitaki.

Moja ya tatizo la kushitaki serikali Tanzania ni kuwa unatengeneza uhasama na serikali na mahakama inaweza kupewa amri kutoka juu iamue vipi.

Tundu Lissu katika hili ameamua kufanya kazi na serikali, amepeleka documents zake wizarani.

Ila naona tatizo ametaka pia kumtumia Abdul ili apate haki yake, this is influence peddling, it is unethical, unfair and a blot on Lissu's reputation especially because he has distinguished himself as someone who stands for fairness and justice.
Acha ujinga, kwanza unatakiwa ujue Lissu hakumwita Abdul. Abdul alikwenda kwa nia ya kutaka kumuonga. Lissu akakataa hongo na kusema anaidai serikali na kama Abdul kwali anataka kumsaidia basi amwambie mama yake amlispe staiki yake. Acha kuleta spin za kijinga. PUMBAFU
 
Naam.

Tufikirie kidhahania.

Muandishi wa habari ukienda kudai haki yako ofisi ya mafao yenye mstari mrefu kwa karani, ukaambiwa na meneja kuwa uache kumuandika vibaya, atakupa hela, ukakataa hela, ila ukasema akusaidie upate fadhila uruke mstari mrefu ili upate mafao yako haraka bila kufuata mstari, hapo hata kama unapata mafao ambayo ni haki yako, ukitumia fadhila ya kuruka mstari inayokupa unfair advantage, hiyo fadhila ni kinyume cha maadili. Ni influence peddling. Ni rushwa.

Lissu namkubali kwenye mengi, moja ya jambo alilosema alitaka watu wam challenge, wamfanyie constructive criticism iki aweze kujifunza mengi na kufanya vizuri zaidi.

Hapa alipotaka kufanya influence peddling ni kitu kibaya, angeweza kufanya vizuri zaidi.

Lissu alitakiwa kukataa pesa za Abdul na kukataa fadhila yoyote. Fadhila nayo ni hongo, hata kama ni fadhila katika kupata haki yako.

Hii hapa ni definition ya influence peddling.

Influence peddling - the use of position or political influence on someone's behalf in exchange for money or favors.
Haikidhi vigezo kwa sababu upande wa pili haupati faida ya hisani tarajiwa.

1. Tuseme kinadharia, kibosire huyo asiyefahamika vizuri hadi sasa alitaka kumhonga TAL.

2. Lengo la rushwa hiyo ni kumfumba kinywa TAL.

3. Lakini TAL yeye akachomoa na kudai kilicho halali yake.

Hata kama huyo kibosire atakubali kumsaidia TAL, haiwezi kuwa influence peddling kwa sabau hamna exchange for money or favors kutoka kwa TAL, maana yeye angeendelea na msimamo wake uleule dhidi ya serikali.
 
kuhusu hizo zinazoitwa fedha za matibabu sijawahi kuelewa na mimi siyo mwanasheria, swali langu, ni je, kutibiwa kwa “viongozi” nje ya nchi ni hisani na huruma tu ya serikali au liko kisheria kwamba kuna sheria iliyowekwa inayosema kwamba “viongozi” watalipiwa matibabu nje ya nchi? na kama ni sheria kwa nini tundu lisu asiishitaki serikali mahakamani kudai haki zake za matibabu? kwa nini asianzie hapo kwanza?
 
kama ni hivyo basi serikali yetu inafanya mambo kienyeji sana, kwa maana kwangu kama layman wa sheria kama sheria ipo na haijafwata ni rahisi kushitaki halafu mahakama inatoa hukumu, ikitoa in your favor umeshinda na hapo serikali au chombo chake kitalazimishwa kukulipa ofcourse nimesimplify lkn hili swala la sijui kukutana na kumuomba mtoto wa raisi kwamba mama yake akulipe kwangu mimi limekaa “kimsaada na hisani” zaidi klk sheria na ngumu hata kujitetea hata huko nje kwa watu walio makini, anyway serikali yetu inafanya mambo kienyeji sana kama ndivyo hivyo …
Tatizo la Tanzania serikali haiheshimu hata maamuzi ya mahakama.

Maana yake ni kwamba, unaweza kuishitaki serikali, kwanza serikali inaweza kupiga simu mahakamani kesi iende vipi (Rejea kauli ya Rostam Aziz aliposema mahakama za Tanzania zinaingiliwa maamuzi yake kwa kupigiwa simu za amri kutoka juu).

Lakini pili, hata ukipata jaji anayesimamia haki ambaye haingiliwi na amri kutoka juu, kushinda kesi mahakamani ni kitu kimoja na kupewa hela zako ni kitu kingine tofauti kabisa. Unaweza kushinda kesi na hela usipewe na ukabaki na ushindi wa makaratasini.

Tundu Lissu anajua yote haya ndiyo maana kaamua kuanza kiupole kwa kudai haki yake wizarani tu.

Suala la kumtumia Abdul ni vibaya si kwa sababu ni la kifadhila fadhila tu, bali pia, ukifuata kanuni za maadili vizuri, ike ilikuwa ni aina ya rushwa.

Abdul alitaka kumhonga Lissu pesa ili Lissu asimsakame sana mama yake Abdul rais Samia, Lissu akakataa hongo ya pesa. Mpaka hapo Lissu alikuwa sawa.

Tatizo, baada ya hapo, Lissu akamuomba Abdul amsaidie Lissu kupata haki yake anayodai serikalini. Hapo Lissu alikataa rushwa ya pesa lakini alikubali kupata rushwa ya fadhila.
 
Hivi unailewa rushwa ni nini?
 
Acha ujinga, kwanza unatakiwa ujue Lissu hakumwita Abdul. Abdul alikwenda kwa nia ya kutaka kumuonga. Lissu akakataa hongo na kusema anaidai serikali na kama Abdul kwali anataka kumsaidia basi amwambie mama yake amlispe staiki yake. Acha kuleta spin za kijinga. PUMBAFU
Nani kamuita nani, nani kamfuata nani ni irrelevant.

Kama kuna rushwa, kuna rushwa tu. Bila kujali nani kamfuata nani, nani kamwita nani.

Hoja ya kwamba hata kwenye kudai haki yako, unaweza kupewa rushwa ya fadhila hujaijibu.

Rushwa si lazima iwe pesa, hata ngono inaweza kuwa rushwa, hata fadhila ya kukupa unfair advantage iliyo nje ya mchakato ni rushwa.

Hujaijibu hii hoja, unalazimisha kuniita mjinga lakini hoja yangu hujaijibu.
 
Back
Top Bottom