Kuhusu Luis Miquissone, Je Simba na Yanga zinaweza kukamilisha dili lake na kumshusha bongo?

Kuhusu Luis Miquissone, Je Simba na Yanga zinaweza kukamilisha dili lake na kumshusha bongo?

DullyJr

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
13,983
Reaction score
11,857
Kuhusu Luis Miquissone

Klabu ya Abha Club inayonolewa na Kocha Roel Coumans ililipa zaidi ya Milioni 700 kama Loan fee kumpata Luis Miquissone kutoka Al Ahly.

Kwa sasa thamani ya Luis Miquissone imeshuka kutoka Usd 300k (Tsh.700m) mpaka 200k (Tsh.466m) na mkataba wa mkopo wa Luis Miquissone pale Abha Club unatamatika June 30,2023.

Luis akiwa Simba alikua analipwa Usd 10,000 (Tsh Milioni 23) kwa mwezi na alipohamia Al Ahly alikuwa akilipwa $500k (zaidi ya bn 1.16) kwa mwaka, sawa na Milioni 95 kwa mwezi.

Kumbuka mkataba wa Luis Miquissone na Al Ahly ni miaka minne yaani mkataba wake na Al Ahly utaisha August 21,2025

Akiwa Abha Club ameendelea kulipwa Milioni 95 ambazo Abha Club na Al Ahly wanachangia kumlipa.

Kulingana na mkataba wake ulivyo,Al Ahly walipaswa kumuongezea mshahara kila Mwaka kutokana na performance yake uwanjani ila ameshindwa kuonesha kiwango bora na ameendelea kupokea pesa ya kwenye Mkataba.

Kuhusu kurejea Tanzania..
Kwa mujibu wa Simon Mimbir,Boss wa Kampuni ya SM-Desporto E Selvicos kutoka Ureno inayomsimamia Luis Miquissone kupitia kwa Djibril Cante (Head of Scouting) ni kwamba kwa Klabu itakayomhitaji Luis itabidi wakae chini na Al Ahly hata hivyo amebainisha kwamba makubaliano ya uhamisho ni kati ya Klabu na Klabu lakini mshahara ni makubaliano ya timu na mchezaji na hawako tayari kupunguza mshahara wa Luis Miquissone.

Kama Klabu itafikia makubaliano na Klabu ya Al Ahly na kuwa tayari kulipa Milioni 95 kwa mwezi Luis atarudi Bongo dirisha kubwa lijalo (mwisho wa mkopo).

Sospeter Ilagila.
FB_IMG_1670575603469.jpg
 
Back
Top Bottom