Kuhusu madaraja ya leseni na magari yake

Kuhusu madaraja ya leseni na magari yake

Mkuu umenena sawa ila je kuna chuo chochote tanzania kinatoa cheti cha leseni daraja B naomba muongozo
Vyuo vyote vilivyo sajiliwa kufundisha/kuzalisha maderea Tz vinatoa cheti cha daraja B.
Daraja bii ndi la kuanzia kujifunzia gari, hutumuka kuendesha magari kundi la hatbak na saloon car, (baby waker) tofauti ya B na C3 ni usajili tu. B namba njano (nyumbani) na C3 namba nyeupe ( bishara/Tax)
 
Alaf kwa lesen ya gar ni kila baada ya miaka mitatu
Mwaka wa 3 ndi unaoruhusiwa kubadili, yaani baada ya miaka 2 kupita, ule wa 3 unarudusiwa kupanda.
Kuwa mwalimu/kumfundisha mtu kwa vitendo sio lazima kwenda chuoni, ila utaratibu ni kwamba, mwanafunzi awe na lena na gari atakayofundishiwa ibandikwe zila alama za L nyekundu kwa vipimo vyake nyuma na mbele ktk gari, kama mwalimu atakua na daraja kubwa kuliko la mwanafunzi, mwalimu atamfudisha bila sharti, lakini kama mwanafunzi atakua na daraja sawa na mwalimu wake, eg. Mwalimu ana daraja C2 na mwanafunzi C2, hapa mwalimu atalazimika daraja laje liwe lishafikisha mwaka 01, tofauti na hapo haruhusiwi kuwa mkufunzi kwa daraja alilonalo.
 
Chief karibu kwenye tasnia hii ya udereva

Madaraja ya leseni na maelezo kama ifuatavyo:

Daraja A,A1,A2 NA A3 NI kwa ajili ya pikipiki.

Daraja B NI MAGARI MADOGO YOTE AMBAYO HAYAJASAJILIWA KIBIASHARA YANI HAYANA PLATENAMBA NYEUPE.

DARAJA D NI MAGARI MADOGO NA MPAKA MWISHO YENYE UKUBWA WA TANI TATU NUSU MFANO CANTER PLATE NAMBA ZISIWE NYEUPE

DARAJA C1,C2,C3 HIZI NI KWA AJILI YA KUBEBA ABIRIA MFANO C1 NI COSTA NA EACHER ZINAZO BEBA ABIRIA PLATE NAMBA ZAKE NI NYEUPE

DARAJA C NI MABASI YA MKOA AU GARI INAYO BEBA ABIRIA KUANZIA 30 NA KUENDELEA

DARAJA E MAGARI MAKUBWA YA MIZIGO KUANZI TANI TATU NA NUSU MPAKA NAKUENDELEA

UTANISAMEHE KWA MUANDIKO MBOVU MANA NATUMIA KITOCHI SO EDITING NYINGI NAONA UVIVU

THANKS
Tofauti kati ya D na B ni ipi?
 
Naomba tukumbushane kitu, hivi utaratibu wa ku renew leseni ukoje sasa bado wana ule ujinga kwa kudai vyeti?
Kama ulisha hakikiwa na barua ya RTO kutoka Polisi unayo, cheti hawana shida nacho, ila kama hauna barua cheti kinahitajika.
Kama una madaraja B,D hawana shida na cheti chako, na kama una madaraja ya abiria, mizigo na mitambo, halafu hayapo ktk cheti chako, wanachokifanya ni kukuondolea hayo madaraja na kukuachia madaraja yako yanayoonekana ktk chei chako tu.
 
Tofauti kati ya D na B ni ipi?
Kiufupi. B, ni gari za nyubani, jamii ya hatbag na saloon car, yaani baby waker (namba za njano)
D, ni suv car na pic-up, panoja na gari ndogo za mizigo zisizozidi 3.5t na isizidi urefu wa 18ft. (namba za njano)
Ukiwa na fuso ikiwa na 3.5t kwa urefu wa 30ft, hapo D haikusaidii, unatakiwa uwe na E kwa ajili ya mizigo.
 
Tofauti kati ya D na B ni ipi?
Mkuu tofauti ni hii
daraja B ni magari binafsi madogo ambayo hayaja sajiliwa kubeba mizigo ya kibiashara wala haziruhusiwi kubeba abiria plate namba ni ya njano (yani magari binafsi ya kutembelea na hizi gar hazi zidi tani mbili capacity)

Na daraja D ni magari madogo ya mizigo mfano townace suzuki carry na canter zile au gar yeyote ilio kaa kwa ajili ya kubebea mizigo (kibiashara) ila gari isizidi tani tatu na nusu na haziruhusiwi kubeba abiria na pia plate namba zake ni za njano.
 
Kama ulisha hakikiwa na barua ya RTO kutoka Polisi unayo, cheti hawana shida nacho, ila kama hauna barua cheti kinahitajika.
Kama una madaraja B,D hawana shida na cheti chako, na kama una madaraja ya abiria, mizigo na mitambo, halafu hayapo ktk cheti chako, wanachokifanya ni kukuondolea hayo madaraja na kukuachia madaraja yako yanayoonekana ktk chei chako tu.

Hivi ule uhakiki bado unaendelea tu?
Maaana licence yangu na daraja AB,C2,D,E
Na sijawahi kupeleka cheti toka watangaze
 
cheti chakuzaliwa vipi?namba ya nidaje?
Boss TIN NO ina taarifa zako zote hivyo hawahitaji wanavipata kupitia hiyo TIN NO.

Vinavyohitajika ni hivi.

1.TIN NO.(Nenda TRA iliyo karibu nawe watakupa buree)au hata wewe mwenyewe unaweza itengeneza online kupitia website ya TRA na bila hii hupati leseni maana ndiyo namba inayotumika kwa mlipa kodi.

2.CHETI CHA UDEREVA KUTOKA CHUO

Na sio kitu kingine.
 
Boss hata TIN no. Huifahamu kweli,
Iko hivi vinavyohitajika.

1.TIN NO.(Nenda TRA iliyo karibu nawe watakupa buree)au hata wewe mwenyewe unaweza itengeneza online kupitia website ya TRA na bila hii hupati leseni maana ndiyo namba inayotumika kwa mlipa kodi.

2.CHETI CHA UDEREVA KUTOKA CHUO

Na sio kitu kingine.
Asante mkuu.nilikuwa nampango wakwenda veta kujifunza ilinichukue leseni mana udereva naujua nimejifunza mtaani lakini leseni ndio Sina

nilikuwa nahisi cheti chakuzaliwa kinahitajika namimi Sina na plosesi yakukifatilia ningumu mana mkoa niliozaliwa nimbali na dar
 
Cheti cha kuzaliwa nenda RITA pale POSTA ni rahisi kama umezaliwa mkoani kukipa kuliko aliyezaliwa DAR.

Pia Leseni haihitaji hivyo vitu zaidi ya Cheti cha udereva na TIN no.
 
Sina certificate mkuu

Wakihakiki kuna document unapewa?
Ambayo utakuwa unaonesha trafick
Ndio.
Unapewa baru ya RTO inayothibitisha kukaguliwa.
Pia unaweza kuwa na cheti cha chuo ambacho hakija sajiliwa kutoa daraja husika, ikala kwako.
Kua na cheti kabla ya leseni ni uhuni na sio utaratibu, unapokua na lena maanayake unaomba leseni, kisheria Polisi/ Vehicle Inspector ndie aliepewa mamlaka ya wewe kukupa daraja unaloomba au kukupa la chini yake au asikupe kabisa kwa mujibu wa drivig yako, baada ya V/INSP kukuthibitishia daraja linalokufaa hio ndio leseni ya udereva, hapo utarudi chuo ulichosoma ili wakutengenezee cheti kwa mujibu wa leseni yako/daraja lako, na itamaliza muda wake baada ya miezi 2 7bu hujalipia kodi leseni hiyo, ndio hapo sasa utaenda kulipia kodi ya leseni ya udereva ya miaka mi 5 ya Tsh- 70,000/= TRA na watakupa kadi inayoonyesha daraja alilokupa Polisi/V.INSP na muwa wa ku expire wa miaka mi 5.
TRA hutoa leseni ila siyo ya udereva.
Wengi hatuna elimu kuhusu upatikanaji sahihi wa leseni za udereva na kuamini TRA ndio wanatoa leseni za udereva, TRA wanakusanya kodi tu ya dereva husika. Ndio maana uhakiki unafanyika Polisi ndio wenye mamlaha na leseni za udereva.
Kupata cheti chuoni bila kua na leseni na ukaenda TRA ukalipa na kupewa kadi, ni nani aliekuthibitisha wewe kua dereva? Siku ukipata ajali na ukakutana na wajuaji mahakamani wakidai uthibitisho wa wewe kua dereva ndio utafurahi, baada ya kukosa sirio namba ya PF ya polisi. Unagongwa na kosa la kughushi/kufoji nyaraka za serekali.
NB. Nenda Veta ua NIT utapata leseni kiurahisi na isio na mashaka maana NIT pale walimu wengi ni ma Polisi/V.INSPECTOR wenyewe, hivyo wanakuthibitisha wenyewe na kila kitu kinaishia pale.
VETA pia wanao ma V.INSP wao.
 
cheti chakuzaliwa vipi?namba ya nidaje?
Cheti cha kuzaliwa hakihusiki.
Namba ya nida ni lazima kwa Zanzibar, maana za kule zinatumika ichi za sadec hivyo kadi ya leseni ni lazima ionyeshe vitu V3 vya msing
1) Wewe ni raia wa taifa gani.
2) Group lako la damu.
3) Una kikwazo gani barabarani. Eg. Unatakiwa kuvaa miwani ya macho au la au leseni yako umezuiliwa kuendesha baadhi ya vyombo kwa muda fulani na mahakama au la, Mfano, umefungiwa daeaja "C" kwa mwaka m1 ila unarugusiwa kuendesha daraja "C2,Ç3 na E" na kama hauna kikwazo wanaandika NONE
Huku kwetu bara sio lazima nida na wakikufungia daraja kwa muda fulani wanafungia leseni yote maana wanachukua kadi hadi muda wa adhabu uishe, kadi zetu hazionyeshi pa kuzuiliwa daraja.
 
Ndio.
Unapewa baru ya RTO inayothibitisha kukaguliwa.
Pia unaweza kuwa na cheti cha chuo ambacho hakija sajiliwa kutoa daraja husika, ikala kwako.
Kua na cheti kabla ya leseni ni uhuni na sio utaratibu, unapokua na lena maanayake unaomba leseni, kisheria Polisi/ Vehicle Inspector ndie aliepewa mamlaka ya wewe kukupa daraja unaloomba au kukupa la chini yake au asikupe kabisa kwa mujibu wa drivig yako, baada ya V/INSP kukuthibitishia daraja linalokufaa hio ndio leseni ya udereva, hapo utarudi chuo ulichosoma ili wakutengenezee cheti kwa mujibu wa leseni yako/daraja lako, na itamaliza muda wake baada ya miezi 2 7bu hujalipia kodi leseni hiyo, ndio hapo sasa utaenda kulipia kodi ya leseni ya udereva ya miaka mi 5 ya Tsh- 70,000/= TRA na watakupa kadi inayoonyesha daraja alilokupa Polisi/V.INSP na muwa wa ku expire wa miaka mi 5.
TRA hutoa leseni ila siyo ya udereva.
Wengi hatuna elimu kuhusu upatikanaji sahihi wa leseni za udereva na kuamini TRA ndio wanatoa leseni za udereva, TRA wanakusanya kodi tu ya dereva husika. Ndio maana uhakiki unafanyika Polisi ndio wenye mamlaha na leseni za udereva.
Kupata cheti chuoni bila kua na leseni na ukaenda TRA ukalipa na kupewa kadi, ni nani aliekuthibitisha wewe kua dereva? Siku ukipata ajali na ukakutana na wajuaji mahakamani wakidai uthibitisho wa wewe kua dereva ndio utafurahi, baada ya kukosa sirio namba ya PF ya polisi. Unagongwa na kosa la kughushi/kufoji nyaraka za serekali.
NB. Nenda Veta ua NIT utapata leseni kiurahisi na isio na mashaka maana NIT pale walimu wengi ni ma Polisi/V.INSPECTOR wenyewe, hivyo wanakuthibitisha wenyewe na kila kitu kinaishia pale.
VETA pia wanao ma V.INSP wao.
Mkuu umemwaga madini yote [emoji120]
 
Back
Top Bottom