Kuhusu Mafanikio

Kuhusu Mafanikio

Shayu

Platinum Member
Joined
May 24, 2011
Posts
608
Reaction score
1,655
Watu wanadhani kwamba kufanikiwa ni kuwa na mali nyingi kuna ukweli katika hili jambo? kwamba mtu aliyefanikiwa ni yule mwenye mali nyingi na wote wasionazo hawajafanikiwa? sidhani kama kuna ukweli katika hili jambo. Maisha yamekuwa magumu kwasababu ya watu kutokuridhika na kile walichonacho kwasababu wanaamini kufanikiwa ni kuwa na mali nyingi. Ni muhimu kujiuliza sababu haswa ya kuwepo kwetu hapa duniani tukijua ndio tutakuwa tumefanikiwa tutakuwa huru. Maisha ni fumbo ambalo linahitaji kufumbuliwa. Kumjua Mungu na kuwa na ushirika nae ndio mafanikio ya kweli.
 
Mwanzo umeanza vizuri tu ila mwisho ndio umebadili kabisa maana ya ulichokuwa una hitaji kukijua mkuu kwani waamini mungu wote huamini ukiwa unasali sana ndio umefanikiwa na je hawa viongozi wa dini wenye mali nyingi wao hawajafanikiwa?

kufanikiwa ni ile hali ya kufikiwa malengo fulani uliokuwa umeyapanga na sio tu kusema umwamini muungu ndio umefanikiwa mkuu..

hayo ndio mawazo yangu juu ya mafanikio.
 
Back
Top Bottom