Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Watu wanadhani kwamba kufanikiwa ni kuwa na mali nyingi kuna ukweli katika hili jambo? kwamba mtu aliyefanikiwa ni yule mwenye mali nyingi na wote wasionazo hawajafanikiwa? sidhani kama kuna ukweli katika hili jambo. Maisha yamekuwa magumu kwasababu ya watu kutokuridhika na kile walichonacho kwasababu wanaamini kufanikiwa ni kuwa na mali nyingi. Ni muhimu kujiuliza sababu haswa ya kuwepo kwetu hapa duniani tukijua ndio tutakuwa tumefanikiwa tutakuwa huru. Maisha ni fumbo ambalo linahitaji kufumbuliwa. Kumjua Mungu na kuwa na ushirika nae ndio mafanikio ya kweli.