Mkuu Naona hujapata hata Uelewa wa kile ulichouliza, Zaidi ya Wadau kukwambia Utatapeliwa n.k
Ukweli ni kwamba Mercury zipo sema biashara yake Imekua na Usiri Mkubwa!
Mercury Zipo za Powder na Liquid..... Mercury zipo za Kiwandani na Natural...
Natural zinazopatikana Tanzania ni Red, Black, Silver, Yellow na White Mercury.....
Natural Mercury zinapatikana kwenye Mountain Caves hasa Mountains ambazo zina chanzo cha maji toka juu asilimia kubwa kuna Mercury....
Kama kuna Biashara inaongoza kwa Utaperi na uhuni na uharamia wa Kila namna Basi ni Biashara ya Mercury..... Ili uipate Natural Red Mercury au nyingine lazima uitoe Vijijini au Mashambani, huko Wazee ndo ama Wanazo ndani ama Huwa wanaenda (Kugema mapangoni) 90% ya Natural Mercury toka kwa Caves ili uweze kuitoa unatakiwa uwe mtu mzito kidogo, hapo ndo watu wengi waliolazimisha kwenda kuchota Mercury kisa wameambiwa inatoka kwenye Pango ambalo lipo mbele yake wamepotelea Mapangoni.
Kwa sababu ya Demand yake imefanya watalaam Watengeneze Mercury fake (90%) hutokea Kenya) na kuingiza Sokoni, na Sokoni kwenyewe means inapelekwa Mashambani huko Vijijini then Wazee wanarudi mjini na kuanza kutangaza kuna Mzee au Wazee wake huko Shamba Wana Mercury.... Kumbuka Mercury ina Vipimo vyake, Local na vya Vifaa vya kisasa, so hata fake inasoma Vipimo japo kwa Masaa kadhaa tu..... Wengi ambao hawataki hata kuisikia hii biashara waliibiwa hapo, coz waliingia Kichwa kichwa...
Kingine watu wa Kijijini kwa sababu ya uhitaji mkubwa wakawa wanatengeneza Mazingira ya pesa, kwamba Tuma nauli nilete mzigo Dar au nilete mzigo Mkoani uje unipokee mtu anatuma 50,000 ama 100,000 au Zaidi na unakua umetapeliwa...
Pia Wana style nyingine kwamba Babu anayo kama chupa ya Fanta, (ukisikia mtu anakwambia Mercury imejaa kwenye chupa ya Fanta ni Taperi) ila hatoi mzigo mpaka apewe hela kidogo coz hakujui wewe, so watasema Babu anataka 500,000 ukituma Umeliwa.
All in all wapo watu Vijijini wana Mercury ila nao Wameibiwa Sana na watu wa mjini kiasi ambacho hawana wa kumwamini, Wameibiwa wakileta Mercury mjini ama fake buyers wakienda huko Vijijini...
Brother wako watu Magomeni, Kariakoo na Posta, Wana Matumbo makubwa na Magari makubwa kazi kusubiri Mercury toka Vijijini wawaibie watu.
Iko Hivi wao (50%) wanatumika na Buyers, yani ni middle men, kama Wewe leo ukawa na Mercury hapo ulipo utaenda kumuuzia nani? Unamjua buyer gani? Means utaanza kuuliza, na katika kuuliza utaunganishwa na middle man ambaye ana buyer, huwezi kufika kwa buyer wake mpaka upitie kwake, hapo ndo ama utaibiwa na ukiwa na Uzoefu na Wizi na Utaperi wa Mercury ama Atakupeleka kwa Buyer ukafanya Biashara au uka Cancel deal.
Buyers ni Whites na Waarabu.... Wamewekeza kwenye Biashara zingine but Wananunua Mercury kwa Siri.
Ila ni Biashara ambayo ipo na watu wanafanya ila wengi Wameibiwa ama na Seller ama na wanaojifanya Buyer!