Kuhusu mgogolo wa Mahindi tunaomba mtuelewe tulio kinyume na spika Tulia

Kuhusu mgogolo wa Mahindi tunaomba mtuelewe tulio kinyume na spika Tulia

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Wandugu. Umofia kwema?

Siku za hivi karibuni tumepata mashambulizi makali kutoka kwa Genge la Bashe. Baadhi ya watu ambao ninaamini huenda ni wanaume wa Dar wamekuwa wakishadadia kile kinachoendelea dodoma wakiwa hawajui hali halisi ya mashambani. Naomba kutoa ufafanuzi kwa hoja zifuatazo.

1. Hali ya wakulima ni mbaya

Ndugu. Kilimo ni kazi ngumu hasa kwa hali ya hewa ya miaka hii. Tunavyo zungumza leo huko njombe mahindi yanapimwa kwa Tsh 2000 kwa debe bila huruma. Baadhi ya wabunge wanajaribu kuona huruma na kudhibiti hali hii lakini spika na bashe hawajali hawasikii.

2. Hatumaanishi mipaka ifunguliwe.
Sisi hapo mwanzo ndio tulio mshauri Bashe afunge mipaka na kudhibiti soko la ndani ila hakuelewa. Bei ya chakula ilipaa kwa kiwango cha kumfaidisha mkulima akadhani amefanikiwa. Kwanza ieleweke Bashe hakukuta mahindi yakiwa bei chini hivi hapana ila hali ilikuwa ni ya wastani. Na hatumshindikizi afungue mipaka hapana ila tunataka tumshauri namna ya kuwasaidia wakulima ambao kwa sasa hali yao ni mbaya. Spika haelewi kazi yake kukumbatia tuu serikali. Bashe haelewi.

3. Si rahisi kwa wakulima kuuza kwenye maghara ya serikali.
Ndugu. Si rahisi kuyafikia maghara ya serikali kwani yapo mbali mno. Wanao yafikia ni madalali ambao wamechangamkia fursa hii kwa kuwalangua wakulima na kwenda kuuza kwenye maghara ya serikali. Bibi kikongwe atoke kijijini uhambule na debe zake mbili kwenda njombe mjini kuuza mahindi zaidi ya km 300 sijui kama inaingia akilini?

4. Halikuwa jukumu la mh spika. Kazi ya spika ilikuwa kuwaruhusu wabunge waongee. Amewafanyia unyanyasaji. Tuliwahi kuwa na bunge la viwango wakati ule ila bunge hili ni la hovyo. Tunashindwa kumuelewa kama ajuza huyu ni mtoto wa masikini wa Rungwe au ni msomali tuu.

Mwisho. Kwa nchi hii ilipo fikia kinacho hitajika ni kunji tuu
 
Wewe ni mfanyabiashara, acha tamaa....chakula bado hakitoshelezi nchini, alafu wewe unataka kupekekwa Kenya?


Ungekuwa makini baada ya kauli ya Mama Samia kule Mwanza ya kushauri wakulima kutokuuza vyakula nje, usingechukua mzigo mkubwa. Kauli ya Rais ni amri/agizo hata akisema Kwa upole au ushauri.

Pambana uzungushe huo mzigo humu humu ndani. Bado Kuna mikoa mahindi ni almasi. Au hifadhi mpaka mwezi wa kumi na moja/mbili utauza Kwa faida.
 
Wewe ni mfanyabiashara, acha tamaa....chakula bado hakitoshelezi nchini, alafu wewe unataka kupekekwa Kenya?


Ingekuwa makinii baada ya kauli ya Mama Samia kule Mwanza ya kushauri wakulima kutokuuza vyakula nje, usingechukua mzigo mkubwa. Kauli ya Rais ni amri/agizo hata akisema Kwa upole au ushauri.

Pambana uzungushe huo mzigo humu humu ndani. Bado Kuna mikoa mahindi ni almasi.
Mimi na wazazi wangu ni wakulima. Na nimebahatika kuwa na ndugu maeneo yote yenye mahindi. Songea wakulima wanalia.. njombe wanalia.. mbozi mtu anapima mahindi anauza huku machozi yanamtoka. Serikali gani hii itaongoza watu wenao nung'unika siku zote? Hatumaanishi afungue mipaka hatujasema hilo ila hali ya mikoani ni mbaya mbaya sana. Huwezi kuuza gunia kwa elf 20 wakati mwezi ulio pita ilikuwa laki na kumi huu ni uuaji mkubwa.

Mimi si mfanya biashara kwani wanao nufaika na mchezo wa bashe ni wafanya biashara
 
Back
Top Bottom